Vyombo vya Ulinzi na Usalama duniani hutumia nguvu kiasi kudhibiti fujo na kupambana na uhalifu kulingana na pingamizi, kiburi na ukaidi wa wahalifu

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Kwa kawaida, kazi ya mwanzo na muhimu sana ya vyombo vya ulinzi na usalama ni kulinda amani na utulivu wa watu, mali na makazi yao, bila kutumia nguvu.

Vyombo vya ulinzi na usalama duniani kote, mara nyingi hufikia hatua ya matumizi ya nguvu kiasi, matumizi ya silaha nyepesi na nzito baada ya kujiridhisha kupitia taarifa za kiintelijensia na kwa kutegemea resistance na mazingira ya ubishi wa muhalifu.

Kujizatiti kwa muhalifu, mathalani kwa silaha nzito za moto au baridi, asili ya kiburi au jeuri ya muhalifu na ukaidi wa kutii sheria kwa hiari bila shuruti.

Kukataa au kugoma kwa makusudi kufuata maelekezo, makatazo muhimu ya kiusalama, maonyo au ilani za kiusalama ambazo watuhumiwa wa kihalifu wengi hukaidi kuzitekeleza..

Na hapo ndipo, vyombo vya ulinzi na usalama huchukua hatua ikiwa ni pamoja na kujihami wao wenyewe na kutumia nguvu kidogo kuwakabili watuhumiwa kwa kuwadhoofisha au kuwanyong'onyeza kidogo ili wasilete matata zaidi, kuwadhibiti, na hatimae kuwatia nguvuni kwa upekuzi na mambo mengine ya kisheria hufuata..

Ndugu mwananchi na raia mwema wa Tanzania, kwa usalama na amani tii sheria bila shuruti kuepuka kukabiliana na nguvu ya vyombo vya ulinzi na usalama..🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Sisi tunasoma habari za Balozi wa USA sio hutu tu propaganda twako kwa maagizo ya Lumumba.
 
sasa si ungeendelea kusoma zaidi kwa balozi, na akusaide kabisa upate urai wa US?

unakuja manga manga na kubabaika na nini sasa pande hii ambayo inahitajika urilax tu, na kama huna fikra mpya au mawazo mbadala, unapita tu kimya kimya lakini kwa kasi ya mwendo wa ngiri? 🐒
 
Wakati mwingine unaweza kuamka na kuanza kulaani kwanini ulizaliwa Afrika, kwanini ulizaliwa Tanzania.
Kwa mujibu wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini adui nambari moja anayechunguzwa ni Mtanzania anayefuata siasa za upinzani.
Ukiwa mwanachama wa upinzani au ukawa kiongozi hapo umekuwa job card ya watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama. Watakufuatilia kama gaidi.
Hizi nguvu zingehamishiwa ukanda wa bahari kuzuia magendo tungeokoa mabilioni kila mwaka.
Hali hii imepelekea kila mfanyabiashara, msanii au mtu yeyote maarufu kujiunga na chama tawala ili kuepuka kashkashi za walinzi wa nchi.
Ukiwa chama tawala ruksa kufanya magendo, ukishikwa mtamalizana juu kwa juu.
 
Inasikitisha sana
 
huu ni upotoshaji na uchochezi chuki usio na madhara dhidi ya vyombo imara na vya kisasa vya ulinzi na usalama nchini..

ni muhimu kuepuka ukaidi na kujitenga kujihusisha na magenge ya kihalifu popote nchini, utabaini tu na utatiwa nguvuni...

visingizio dhaifu na vinavyotegemea huruma kama hivi ni useless linapokuaja suala la kulinda umoja, amani na utulivu wa waTanzania 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Inasikitisha sana
masikitiko makubwa zaid ni katika kukaidi maelekezo, amri au ilani za kiusalama zinazotolewa na vyombo vya ulinzi, aisee mbona muhalifu kaidi na mbishi utakiona chamtema kuni, Lazima ulazimishwe kutii sheria kwa shuruti sasa🐒
 
Kwa kawaida, kazi ya mwanzo na muhimu sana ya vyombo vya ulinzi na usalama ni kulinda amani na utulivu wa watu, mali na makazi yao, bila kutumia nguvu.

Vyombo vya ulinzi na usalama duniani kote, mara nyingi hufikia hatua ya matumizi ya nguvu kiasi, matumizi ya silaha nyepesi na nzito baada ya kujiridhisha kupitia taarifa za kiintelijensia na kwa kutegemea resistance na mazingira ya ubishi wa muhalifu.

Kujizatiti kwa muhalifu, mathalani kwa silaha nzito za moto au baridi, asili ya kiburi au jeuri ya muhalifu na ukaidi wa kutii sheria kwa hiari bila shuruti.

Kukataa au kugoma kwa makusudi kufuata maelekezo, makatazo muhimu ya kiusalama, maonyo au ilani za kiusalama ambazo watuhumiwa wa kihalifu wengi hukaidi kuzitekeleza..

Na hapo ndipo, vyombo vya ulinzi na usalama huchukua hatua ikiwa ni pamoja na kujihami wao wenyewe na kutumia nguvu kidogo kuwakabili watuhumiwa kwa kuwadhoofisha au kuwanyong'onyeza kidogo ili wasilete matata zaidi, kuwadhibiti, na hatimae kuwatia nguvuni kwa upekuzi na mambo mengine ya kisheria hufuata..

Ndugu mwananchi na raia mwema wa Tanzania, kwa usalama na amani tii sheria bila shuruti kuepuka kukabiliana na nguvu ya vyombo vya ulinzi na usalama..🐒

Mungu Ibariki Tanzania

Hata Sendeka alikuwa na mawazo kama yako hadi siku ile ...
 
Back
Top Bottom