Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Kwa kawaida, kazi ya mwanzo na muhimu sana ya vyombo vya ulinzi na usalama ni kulinda amani na utulivu wa watu, mali na makazi yao, bila kutumia nguvu.
Vyombo vya ulinzi na usalama duniani kote, mara nyingi hufikia hatua ya matumizi ya nguvu kiasi, matumizi ya silaha nyepesi na nzito baada ya kujiridhisha kupitia taarifa za kiintelijensia na kwa kutegemea resistance na mazingira ya ubishi wa muhalifu.
Kujizatiti kwa muhalifu, mathalani kwa silaha nzito za moto au baridi, asili ya kiburi au jeuri ya muhalifu na ukaidi wa kutii sheria kwa hiari bila shuruti.
Kukataa au kugoma kwa makusudi kufuata maelekezo, makatazo muhimu ya kiusalama, maonyo au ilani za kiusalama ambazo watuhumiwa wa kihalifu wengi hukaidi kuzitekeleza..
Na hapo ndipo, vyombo vya ulinzi na usalama huchukua hatua ikiwa ni pamoja na kujihami wao wenyewe na kutumia nguvu kidogo kuwakabili watuhumiwa kwa kuwadhoofisha au kuwanyong'onyeza kidogo ili wasilete matata zaidi, kuwadhibiti, na hatimae kuwatia nguvuni kwa upekuzi na mambo mengine ya kisheria hufuata..
Ndugu mwananchi na raia mwema wa Tanzania, kwa usalama na amani tii sheria bila shuruti kuepuka kukabiliana na nguvu ya vyombo vya ulinzi na usalama..π
Mungu Ibariki Tanzania