Mkuu...ungemwelewa
CreativityCode alipouongelea msingi wa imani ya wakristo ungekiri kuwa waislamu na wakristo ni tofauti kabisa. Waislamu kumtambua Yesu kama nabii haitoshi kuwafanya hawa watu washirikiane katika kujenga madhabahu zao. Wanamtambua kama nabii lakini wanasema "alikufa na hakufufuka". Je utasemaje hizi imani mbili ziko sawa?
Sidhani kama kuna kanisa la kipentekoste limeshiriki katika huo mchango na kama lipo narudia kusema wanaosali katika kanisa hilo wajichunguze mara mbili mbili kama wako katika mstari stahiki wa imani ya Yesu Kristo.