Umefanya vizuri kutoa la moyoni. Ila ukweli ni kwamba kwa kazi za wana usalama, hilo ni jambo dogo. Kwamba fulani kasema? Ana haki ya kuongea anachokitaka. Kwani ni wapi kadai waha warudi Rwanda? Unadhani Rwanda hakuna waha? Watu weusi walifikaje Marekani? Au wazungu walifikaje South Africa?
Kwa umri wako, ni utoto unaokusumbua. Hata kila mhamiaji aliyepo nchini unadhani hajulikani? Siku ajitose kuleta vurugu, ndo utajua hivyo vyombo vinafanya kazi.
Ushabiki wa kinafiki hauna maana. Kwani akidai waha ni wa Rwanda, akaomba hao waha warudi kwao, unapungukiwa nini? Hao waha, leo hii ukiwambia rudini kwenu, wataenda?
Hata yeye ni binadamu, kuongea tofauti na uhalisia ni jambo la kawaida. Kama lina uzito, ulisikia serikali inatoa jibu lake kuhusu hilo? Acha utoto.