Vyombo vya usafiri vinavyoongoza kwa vurugu barabarani

Malori wastaarabu sana, wangekuwa kama bodaboda au bebi woka tungekufa sana
hakuna wavumilivu km wenye Malori, angalia ule moto wa Msamvu Morogoro, Tanker liliogopa Bodaboda iliyokatiza mbele yake bila ya kufuata sight
Bajaj zinaongoza jamani, yaani mpo keep-left atapenya hadi mbele yako tena wrong site akae mbele tako na akifika mbele hana mwendo atang'ang'ania akae katikati ya barabara, kweli wawekewe Line yao au wasiruhusiwe kwenye Highway
 
Nikiri tu mara mbili tatu nishaovateki mbele bodaboda inakuja nanyoosha tu namwachia kasehemu kadogo apishe
 
Hiyo mamba 2 wanaņchi waishio mbezi ya kimara wanaonewa sana kwa nauli na barabara ndio wao wanaongoza kwa kusababisha ajali yaani ikifika jioni saa moja unusu kuanzia manzese darajani hadi mbezi barabara yote ni fujo bora wangerudisha daladala ziwe zinaishia magomeni
 
Mkuu hii listi ni kwa dasalama au na huku mikoani inahusika!!!
 
Ha ha ha wanakera anapenya halafu anakaa mbele huku speed 25kph
 
Nikiri tu mara mbili tatu nishaovateki mbele bodaboda inakuja nanyoosha tu namwachia kasehemu kadogo apishe
Hahah hili lipo, hata mimi nikiendesha gati nafanya hivyo pia.

Ugomvi wangu na ST SU ni kuwa wao ni every time. Washawahi kunibana kwenye daraja la mizani ya mikese, washawahi kunikaba pale gairo wakati barabara inatengenezwa, washawahi kuniforce nje ya barabara kwenye haya mawimbi kati ya Ruvu na Chalinze, yani jamaa hawaachi nafasi. Yani ile mita moja tu ya kunitosha mimi kupita hawaiachi wanakula baravara nzima mpaka kwenye mstari wa mwisho wa barabara wa upande wangu
 
Kuna sehemu bajaj ndio kama daladala nauli 500/- wanapanda abiria hadi watano
 
Duh wanahisi barabara mali yao
 
Exactly. Hata kama una gari bado watakuletea ubabe wao vile vile. Wanatunishia misuli mpaka mabasi ya mkoa.
Kwenye foleni hapa mjini huwa wanatanua ili uwapishe. Huwa sipishi, kuna siku nilikomaa nikagoma kupisha gari ina namba W.....
Eti amekwepa foleni analazimisha mimi ambae niko kwenye upande wangu niingie kwenye dimbwi nimpishe yeye, siku hio alilazimika kurudi upande wake
 
Vyote viwili harufu na mwendo wao wanapokuwa na gari empty!. Utadhani wanaendesha kifaru!.
Hawa wanakera kusimama katikati ya barabara kuu wakizoa taka hawajali chochote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…