Vyombo vya Usalama vichunguze tuhuma za Uhalifu wa Mo Dewji na Genge lake kudukua mawasiliano ya watu/wafanyakazi wake

Tangu lini mhindi akamthamini mwafrika. Mo ni wale wale tu.
 
Uzi hautaki kuyajadili hayo mkuu.

Uzi unajadili uwezekano wa Jinai kufanyika hapo katika udukuzi. Tungejikita hapo.

Mijadala ya Mo+Babra vs Manara ipo Mingi
Nimetetea hoja yangu tu inaweza kuwa kweli amedukuliwa au anapiga porojo.

Hatuwezi hukumu moja kwa moja mpaka ithibitishwe kuwa ni kweli
 
Hahahahaha mnaloooooo mwaka huuu,umedukuliwa hujadukuliwa sisi inatuhusu nini,mbona usiseme wakati hujaondoka Simba?
 
wale mapira kitengo cha cyber crime ukiwapa hela kiduchu tu unapata details kibao cha umtakaye kwa maana ya kuwapa namba ya mtu halaf anafuatiliwa.Watu hutoa pesa then wenzi wao wadeni wao n.k wanafuatiliwa kuona wanendaga wapi na wanakuwa na akina nani.Kuna demu yupo kwenye hicho kitengo anapiga hela kinoumer kwa issue hizo. matajiri wengi wanafuatilia sana watu. kwa mtu kama mo hiyo ni kawaida sana. wakati nipo chuo kuna dent mmoja muhindi alikuwa na wivu sana na manz wake so alikuwa analipa hela then analetewa mkeka printed wa meseji incoming na outgoing za manzi wake. yaani mkeka ka bank statement vile!!!!
 
Manara ni muongo mkubwa anasema "Mo Dewji alinipigia simu akaniambia eti kwanini ninamzidi umaarufu wakati mimi nimekuzidi hela"? Huu ni uongo. Ni kitu kisichowezekana ila mashabiki vilaza wa Simba wataamini huu uongo.
Mkuu, uongo mwingine, anadai ile mechi ya Dar, alinyimwa tiketi. Akaangalia mpira nyumbani kupitia runinga. Kisha sahau kuwa alifiwa na bibi yake, na aliaga kupitia humu mitandaoni kuwa anakwenda kilioni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…