Vyombo vya Usalama vinamhujumu Rais kutokana na matendo maovu kushika kasi

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Matukio ya uovu yamezidi kushika kasi kipindi hiki kwa namna ambayo inaonesha dhahiri kuwa kuna hujuma inafanyika kwa ndugu Rais Samia Suluhu Hassan.

Matendo haya ya uovu ubaya zaidi yanafanywa na vyombo vinavyotakiwa kulinda wananchi. Matokeo yake sasa ndo vinahusishwa na kuteka na kuua wananchi.

Wananchi wanaendelea kupotea wakiwa mikononi mwa polisi na kuuawa wakiwa mikononi mwa polisi au wanajeshi. Je, haya si makusudi kutaka kumpima Rais?

Aonekane ni dhaifu hawezi wakemea au kuwa yeye hajali wananchi wa huku?

Haya mambo yasiachwe hivi hivi lazima hatua zichukuliwe.
 
Orodhesha hayo matendo. Aidha unapowaambia polisi wasitumie nguvu wape basi tehcnics mbadala za wenzetu nchi zilizoendelea wanaofanya bila kutumia nguvu je wafanye nini?
 
Unawezakuta hachafuliwi rais ila wanachafuliwa wakuu wa vitengo vya usalama hasa polisi.
 
Matukio ya uovu yamezidi kushika kasi kipindi hiki kwa namna ambayo inaonesha dhahiri kuwa kuna hujuma inafanyika kwa ndugu Rais Samia Suluhu Hassan.

Matendo haya ya uovu ubaya zaidi yanafanywa na vyombo vinavyotakiwa kulinda wananchi. Matokeo yake sasa ndo vinahusishwa na kuteka na kuua wananchi.

Wananchi wanaendelea kupotea wakiwa mikononi mwa polisi na kuuawa wakiwa mikononi mwa polisi au wanajeshi. Je, haya si makusudi kutaka kumpima Rais?

Aonekane ni dhaifu hawezi wakemea au kuwa yeye hajali wananchi wa huku?

Haya mambo yasiachwe hivi hivi lazima hatua zichukuliwe.

8D612394-BA7B-48C8-B60D-5F6FFA692227.jpeg
 
Kwenye baraza la fisi
Kondoo hasemi neno
Kwani yeye atahisi
Fisi watatoa meno
Hata wanaponajisi
Lazima atoe tano
 
Acha maneno mengi, kama unahisi mama anahujumiwa you're wrong, rais anajihujumu yeye mwenyewe, kwani yeye hayupo ndani ya nchi anayoiongoza hasipate taarifa yaatukio kwa wananchi wake!?? Yeye anatakiwa asimame na akemehe lakini kama umemsikia leo anasema hawezi fukuza wasaidizi wake wanaokosea utasemaje anahujumiwa!?.
 
Matukio ya uovu yamezidi kushika kasi kipindi hiki kwa namna ambayo inaonesha dhahiri kuwa kuna hujuma inafanyika kwa ndugu Rais Samia Suluhu Hassan.

Matendo haya ya uovu ubaya zaidi yanafanywa na vyombo vinavyotakiwa kulinda wananchi. Matokeo yake sasa ndo vinahusishwa na kuteka na kuua wananchi.

Wananchi wanaendelea kupotea wakiwa mikononi mwa polisi na kuuawa wakiwa mikononi mwa polisi au wanajeshi. Je, haya si makusudi kutaka kumpima Rais?

Aonekane ni dhaifu hawezi wakemea au kuwa yeye hajali wananchi wa huku?

Haya mambo yasiachwe hivi hivi lazima hatua zichukuliwe.
Matenda hayo hayo machafu ya polisi ndiyo yaliyompa kuwa makamu wa rais 2020. Hivyo hawezi kuwafanya lolote la maana
 
Muhimu ni kuwa angalia Watanzania walioathirika na matendo ya polisi. Hata polisi wakiamua kuua kila siku mtanzania 1, bado Samia ata endelea kuwa Rais mpaka CCM wakiamua wenyewe.
 
Matukio ya uovu yamezidi kushika kasi kipindi hiki kwa namna ambayo inaonesha dhahiri kuwa kuna hujuma inafanyika kwa ndugu Rais Samia Suluhu Hassan.

Matendo haya ya uovu ubaya zaidi yanafanywa na vyombo vinavyotakiwa kulinda wananchi. Matokeo yake sasa ndo vinahusishwa na kuteka na kuua wananchi.

Wananchi wanaendelea kupotea wakiwa mikononi mwa polisi na kuuawa wakiwa mikononi mwa polisi au wanajeshi. Je, haya si makusudi kutaka kumpima Rais?

Aonekane ni dhaifu hawezi wakemea au kuwa yeye hajali wananchi wa huku?

Haya mambo yasiachwe hivi hivi lazima hatua zichukuliwe.
POLISI Wameamua Kuua na kupora Mali za RAIA badala ya Kulinda RAIA na Mali zao

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
sidhani kama ni hujuma, hao jamaa ndio tabia na maisha yao kitambo...

haya mengine yakina Barke Pesa aka Barke bank na akina Jonnsina bouncer ni jamii tu kukengeuka na kuparamia maujinga..
 
Acha maneno mengi, kama unahisi mama anahujumiwa you're wrong, rais anajihujumu yeye mwenyewe, kwani yeye hayupo ndani ya nchi anayoiongoza hasipate taarifa yaatukio kwa wananchi wake!?? Yeye anatakiwa asimame na akemehe lakini kama umemsikia leo anasema hawezi fukuza wasaidizi wake wanaokosea utasemaje anahujumiwa!?.
yaani Kuna watu walikuwa watimuLiwe siku anaapishwa kwa kuwa ni waongo wa taifa kwa mfano ;-
MAKOSA YA KATELEFONI
Alitudanganya kuwa
(1)kuwa marehemu yupo anachapa KAZI nyie watz mlitaka aende magomeni
(2)Tanzania tuna umeme wa kutosha kuwagawia wawekezaji kutoka nje ya nchi
(3)huko Kwa kina katelefoni walizusha hii ni serikali ya mpito Tu AwaMu ya sita inakuja
(4) Leo 14 January 2022 ni siku ya 40 ya mwaka mpya 2022.
 
Matukio ya uovu yamezidi kushika kasi kipindi hiki kwa namna ambayo inaonesha dhahiri kuwa kuna hujuma inafanyika kwa ndugu Rais Samia Suluhu Hassan.

Matendo haya ya uovu ubaya zaidi yanafanywa na vyombo vinavyotakiwa kulinda wananchi. Matokeo yake sasa ndo vinahusishwa na kuteka na kuua wananchi.

Wananchi wanaendelea kupotea wakiwa mikononi mwa polisi na kuuawa wakiwa mikononi mwa polisi au wanajeshi. Je, haya si makusudi kutaka kumpima Rais?

Aonekane ni dhaifu hawezi wakemea au kuwa yeye hajali wananchi wa huku?

Haya mambo yasiachwe hivi hivi lazima hatua zichukuliwe.
Yalikuwepo toka kitambo ila tofauti ya Sasa ni kwamba watu ni wepesi kutoa taarifa na pia mitandao ya kijamii inachangia Sana..

On top of that Rais karuhusu watu wafunguke tofauti na enzi za Giza.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Yaani Polisi wakiuke maadili ya kaz zao iwe hujuma??Enzi za Kikwete haikuwahi kutokea Polisi kuua na kupora?Enzi za Magufuli Polisi walimpora muuza madini huko Arusha ilikuwa hujuma?
Professor Maeda aliporwa milioni 100 na Polisi huko Arusha enzi za Magufuli ilikuwa hujuma?
Wacheni uzushi wa kuzua kila jambo ni hujuma.Matukio yatatokea tu kwa sababu kuna wasiofuata sheria.
Jamii ya Utopia kwamba kila kitu ni perfect haipo na wala haitokuwepo.
 
Matukio ya uovu yamezidi kushika kasi kipindi hiki kwa namna ambayo inaonesha dhahiri kuwa kuna hujuma inafanyika kwa ndugu Rais Samia Suluhu Hassan.

Matendo haya ya uovu ubaya zaidi yanafanywa na vyombo vinavyotakiwa kulinda wananchi. Matokeo yake sasa ndo vinahusishwa na kuteka na kuua wananchi.

Wananchi wanaendelea kupotea wakiwa mikononi mwa polisi na kuuawa wakiwa mikononi mwa polisi au wanajeshi. Je, haya si makusudi kutaka kumpima Rais?

Aonekane ni dhaifu hawezi wakemea au kuwa yeye hajali wananchi wa huku?

Haya mambo yasiachwe hivi hivi lazima hatua zichukuliwe.
Rais alipoingia madarakani aliwabana sana Hawa watu wa vyombo vya usalama wa raia na madawa ya kulevya pia Ila Sasa naona wanajifanyia wanayotaka tu.

Simon Sirro amelalamikiwa sana kwamba hafai kuendesha jeshi la polisi sababu hakuna matokeo chanya katika mabadiliko ya utendaji wa polisi.

Polisi hawabadilishi mifumo ya utendaji kazi, wao ni walewale wa miaka ya 60 hakuna jipya. Najiuliza wameshindwa kuform kitengo Cha maendeleo na mabadiliko ya jeshi ikiwemo kuweka mipango mikakati kujenga vituo vipya, mahabusu, upatikanaji wa chakula kwa mahabusu na askari wawapo kazini nk?

Jeshi linatumia vitendea kazi vya kizamani na tactics za kizamani ingali dunia imeshabadilika na uhalifu umeadvance sana tunategemea kabisa kupata majibu ya upelelezi kwa haraka?

Polisi hawapewi laptop, hakina mfumo mpya wa kisasa wa kurejista mahabusu, kesi zinazofunguliwa, askari wa zamu nk yani mpaka leo unategemea lile kaunta book lao wanalopiga mistari na kuandikaandika mule?

Rejista zinakuwa manual yani ukichana page ushahidi umepotea wanakwama wapi kutengeneza mfumo wa computer wenye kupokea taarifa hizo kwa usahihi na zikatumzwa makao makuu hata kesho tukitaka kujua aliyepo zamu leo kituo cha polisi Nkasi ni Nani?

Sirro ameshindwa kazi mno jeshi limepoa na limepwaya sana askari wamegeuka majambazi na Sirro anatoa macho yake tu na kushinda kwenye vikao kila siku

Yeye kila siku utasikia tumekuta watu wa usalama wa maziwa makuu kujadili namna ya kukomesha uhalifu wanamuweka busy na vikao vya kijinga huku askari wanageuka majangili wakubwa.

Sirro it's time to go. Polisi imekushinda kakae na Yule mwanao mvuta bangi umkanye tu labda itakusaidia kwa huu muda mchache uliobaki hapa duniani otherwise ukifa kabla haijabadilika utakuwa umetuachia mtoto wa hovyo sana.
 
yaani Kuna watu walikuwa watimuLiwe siku anaapishwa kwa kuwa ni waongo wa taifa kwa mfano ;-
MAKOSA YA KATELEFONI
Alitudanganya kuwa
(1)kuwa marehemu yupo anachapa KAZI nyie watz mlitaka aende magomeni
(2)Tanzania tuna umeme wa kutosha kuwagawia wawekezaji kutoka nje ya nchi
(3)huko Kwa kina katelefoni walizusha hii ni serikali ya mpito Tu AwaMu ya sita inakuja
(4) Leo 14 January 2022 ni siku ya 40 ya mwaka mpya 2022.
Hiyo ya kwanza mbona hata yeye mama Samia alisema Magufuli anawasalimia Sana siku moja kabla ua kutangaza kifo
 
Back
Top Bottom