Rais alipoingia madarakani aliwabana sana Hawa watu wa vyombo vya usalama wa raia na madawa ya kulevya pia Ila Sasa naona wanajifanyia wanayotaka tu.
Simon Sirro amelalamikiwa sana kwamba hafai kuendesha jeshi la polisi sababu hakuna matokeo chanya katika mabadiliko ya utendaji wa polisi.
Polisi hawabadilishi mifumo ya utendaji kazi, wao ni walewale wa miaka ya 60 hakuna jipya. Najiuliza wameshindwa kuform kitengo Cha maendeleo na mabadiliko ya jeshi ikiwemo kuweka mipango mikakati kujenga vituo vipya, mahabusu, upatikanaji wa chakula kwa mahabusu na askari wawapo kazini nk?
Jeshi linatumia vitendea kazi vya kizamani na tactics za kizamani ingali dunia imeshabadilika na uhalifu umeadvance sana tunategemea kabisa kupata majibu ya upelelezi kwa haraka?
Polisi hawapewi laptop, hakina mfumo mpya wa kisasa wa kurejista mahabusu, kesi zinazofunguliwa, askari wa zamu nk yani mpaka leo unategemea lile kaunta book lao wanalopiga mistari na kuandikaandika mule?
Rejista zinakuwa manual yani ukichana page ushahidi umepotea wanakwama wapi kutengeneza mfumo wa computer wenye kupokea taarifa hizo kwa usahihi na zikatumzwa makao makuu hata kesho tukitaka kujua aliyepo zamu leo kituo cha polisi Nkasi ni Nani?
Sirro ameshindwa kazi mno jeshi limepoa na limepwaya sana askari wamegeuka majambazi na Sirro anatoa macho yake tu na kushinda kwenye vikao kila siku
Yeye kila siku utasikia tumekuta watu wa usalama wa maziwa makuu kujadili namna ya kukomesha uhalifu wanamuweka busy na vikao vya kijinga huku askari wanageuka majangili wakubwa.
Sirro it's time to go. Polisi imekushinda kakae na Yule mwanao mvuta bangi umkanye tu labda itakusaidia kwa huu muda mchache uliobaki hapa duniani otherwise ukifa kabla haijabadilika utakuwa umetuachia mtoto wa hovyo sana.