Nimejaribu kukusoma nikifikiri kuwa labda mwandishi ni mtu mwenye akili na ufahamu fulani nijifunze kupitia andiko lake, lakini sijaona cha maana na kujifunza kwako zaidi kuwa unapiga propaganda zilezile za siasa uchwara za ki - CCM ukidhani utaeleweka na kuhalalisha uvunjaji wa sheria na katiba unaoendelea sasa nchini kwetu unaofanywa na serikali na vyombo vyake vya kulinda na kusimamia sheria hususani Police na TISS...
Ni kweli police, PCCB au chombo chochote cha kisheria kinaweza si tu kufuatilia bali kumlazimisha mtu fulani a - disclose mawasiliano yake kwa lengo la uchunguzi wa kihalifu (crime investigation)...
Lakini tendo hili halifanyiki kienyeji tu kwamba, kwa mfano, Rais Samia leo kaamka vibaya, na kuhisi kuwa, jana Tundu Lissu kampiga nondo ngumu sana kwenye majukwaa yao kisiasa zao huko akitumia taarifa nyeti za siri kuhusu Rais kuhongwa na waarabu wa Oman ili awape ardhi yote ya Ngorongoro na kuwafukuza wamasai au mkataba wa Bandari na DPW. Na kwa sbb hii Rais anatoa maagizo kienyeji tu kwa IGP Camillius Wambura wakailazimishe TIGO au VODACOM au AIRTEL au HALOTEL wa - disclose privacy ya mteja wao huyu ili kuwezesha ku - rack mawasiliano yake, wapate taarifa zake fulani fulani bila kufuata sheria...
Ndugu
Joseph Ludovick, mambo hayaendi hivyo japo vyombo hivi vina mamlaka hayo. Sheria zetu kuhusu mawasiliano ni mbaya lakini hazijaweka mwanya wa mtu fulani mwenye madaraka na mamlaka ya kiserikali kama vile Police, PCCP, Rais, DCI, IGP, au Waziri fulani kujiamulia na kudukua mawasiliano ya watu kienyeji tu bila kufuata sheria....
Sheria ya Cybercrime Act kifungu cha 32 iko very clear kwenye hili, kusema...
Data disclosure when a crime is suspected
"....The disclosure of data for the purposes of a criminal investigation or the prosecution of an offence is dealt with in Section 32 of the Cybercrimes Act. In such instances, a police officer in charge of a police station or a law enforcement officer of a similar rank may issue an order to any person in possession of such data compelling him or her to disclose it. It may happen, however, that there is resistance from the party holding data of evidential value. Similarly, it may be impossible to obtain the data without the use of force. In these circumstances, the law enforcement officer may apply to court for an order of disclosure or preservation..."
Hata kwa mtu binafsi tu, polisi hawawezi kumlazimisha mtu kutoa password ya simu unless otherwise wana amri ya mahakama..
Hiki ndicho kinachoendelea mahakamani sasa kwenye kesi ya Boniface Jacob (Boni Yai) na mapolisi. Boni kawakatalia kuwapa polisi password za simu zake. Na kwa sbb hii, polisi wameiomba mahakama impe amri Boni awape polisi funguo za kufungua waingie kwenye simu zake. Huu ndio utaratibu wa kisheria....
Kwa kesi ya Tundu Lissu vs Tigo, hiyo ni mbaya zaidi. Serikali ilifanya jambo baya mno kuilazimisha kampuni ya TIGO ku - violate privacy policy yao dhidi ya mteja wao Tundu Lissu...
TIGO walikubali kutumiwa na baadhi ya viongozi wa serikali kuvunja sheria kwa makusudi. Na sijui ikawaje kampuni kubwa kama ya TIGO ilikubali kucheza mchezo huu mchafu kabisa wakati walikuwa na nafasi ya kujiweka kwenye "safe side" kuitaka serikali ifuate utaratibu wa kisheria kwa kwenda kupata "court order" ya kuwaruhusu TIGO kumuuza mteja kwa mujibu wa sheria....
Kilichofanyika ni kuwa, badala ya data za mteja wao walizo - disclose kutumika kama ushahidi mahakamani, zikatumika kama njia ya kuondoa uhai wake kwa kupigwa risasi. Huu ni UGAIDI WA KIDOLA ni kosa kubwa sana....
Tendo hili ni TiGO kushiriki mauaji. Hili ni kosa kwa mujibu wa sheria zetu Tanzania ni kosa kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Lazima walipie makosa yao....
Kwa hiyo ndugu
Joseph Ludovick, umechemka sana na kwenye hili umetoa nusu hoja na nusu nyingine umeifungia chumbani kwako kwa sababu unazozijua wewe...!