Vyombo vya Usalama vinaweza kufuatilia mawasiliano kwa kibali halali


Kurukq ruka Kwa maharage ndo kuiva kwake,,, Kwan umeombwa ulete utetezi? Na Kwa nn mlimpiga marisasi baada ya kujua alipo na mawasiliano yake?
 
AFANDE
Tofautisha kwamba

Vyombo vya Dola haviwezi kuwa mahakama ya JMT
 

1. Umejitahidi kueleza kadiri ulivyoweza kuhusu vyombo ambavyo umesema "vinaweza kufuatilia mawasiliano ya watu kwa sababu za kiusalama".
2. Nitachangia kwenye mjadala huu kwa kuweka dhana mbili pamoja: dhana ya haki ya ulinzi wa faragha ya mtu na haki ya kulinda mawasiliano yake binafsi. Kwa maana hiyo, mchango wangu utajikita katika Ibara 2: Ibara ya 16 na ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
3. Umesema vyombo ulivyovitaja vinaweza kuingilia taarifa binafsi za watu kwa sababu za kiusalama.
4. Lakini umesahau kusema kwamba vyombo hivyo ni sharti vifanye hayo kwa mujibu wa sheria. Hii ndiyo 'justification' ya kufanya jambo kwa masilahi ya kiusalama, na masilahi hayo yanatakiwa yawe bayana.
4. Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa mujibu wa sheria na kwenye utawala wa sheria ni muhimu kufahamu kwamba: "Every act of governmental power - every act which affects the legal rights, duties or liberties of any person, must be shown to have a strictly legal pedigree" (Wade, H.W.R. & Forsyth, C.E. (2000). Administrative Law (Eighth Edition) p. 20.
4. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kama iliyofanyiwa marekebisho hadi 2005) inatoa ulinzi kwa haki ya faragha kwenye Ibara ya 16. Ibara ndogo ya (1) inasema: "Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi."
5. Tanzania pia imeridhia mikataba ya kimataifa na inafungwa na mikataba hiyo ili kuendana na matakwa ya mikataba yake, ambayo pia inatoa ulinzi wa faragha ya mtu na mawasiliano yake binafsi.
6. Kama mabalozi wanakuja nchini kuwakilisha mataifa yao na wageni kutoka nchi mbalimbali pamoja na wawekezaji ni kwa sababu wanaamini Tanzania inaheshimu mikataba ya kimataifa inayotoa ulinzi wa faragha na mawasiliano binafsi ya mtu. Katiba kwenye Ibara ya 18(c) inaeleza: "Every person - has the freedom to communicate and a freedom with protection from interference from his communication."
7. Katika Kesi Na 110 ya mwaka 2018 iliyoamliwa mwaka 2019, Mahakama Kuu ya Tanzania (Dar es Salaam) ilisema hivi: "the right to privacy is guaranteed under Article 16(1) of the Constitution of the United Republic of Tanzania of 1977 as amended. Article 16(1) states: Every person is entitled to respect and protection of his person, the privacy of his own person; his family and of his matrimonial life, and respect and protection of his residence and private communication."
8. Mahakama Kuu iliongeza kwamba "the right to privacy is further guaranteed under Article 12 of the Universal Declaration of Human Rights, 1948 which provides: No one shall be subjected to arbitrary interference with his privacy, family home or correspondence...and everyone has the right to the protection of the law against such interference...."
9. Aidha, Mahakama Kuu ya Tanzania ilisema: "Tanzania is a signatory to the International Covenant on Civil and
Political Rights. Article 17(1) guarantees the right to privacy. It states: No one shall be subjected to arbitrary or unlawful interference with his privacy, family, home or correspondence...and everyone has the right to protection of the law against such interference..."
9. Katika kesi hii Mahakama Kuu ya Tanzania ilirejea kesi ya R. Raja Gopal v. State of Tamil Nadu ya mwaka 1995 katika Mahakama ya Juu ya India na kusisitiza vipengele viwili katika haki ya faragha: "1. The general law of privacy which affords a tort action for damages resulting from an unlawful invasion of privacy and; 2. The constitutional recognition given to the right to privacy which protects personal privacy against unlawful governmental invasion."
10. Nisirefushe mjadala, lakini jambo muhimu ni kwamba kama vyombo ulivyovitaja vinaweza kuingilia mawasiliano ya mtu binafsi kwa sababu za kiusalama, ni sharti vifanye hivyo kwa mujibu wa sheria.
11. Ibara ya 30(3) ya Katiba inasema "Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote la sehemu hii ya sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza kufunguka shauri katika Mahakama Kuu."
 
Vyombo vya ulinzi na usalama duniani kote huwa vinafuatilia mawasiliano ya watu wanao washuku kuwa huwenda wana nia ovu ktk nchi husika, ila hufanya ufuatiliaji huo kwa siri na si kisheria. Na hufanya hivyo kwa manufaa ya nchi si kwa ajili ya maslai binafsi ya mtu au kikundi fulani, ila muhusika akigundua kuwa anadukuliwa hata kama ni vyombo halali vya nchi bila ridhaa ya mahakama anaweza akashitaki na kulipwa fidia kwa kuingiliwa uhuru wake wa faragha. Kwa misingi hiyo udukizi huwa unafanywa kwa siri na siyo halali. Nchi zinazo ongoza sana kwa udukuzi ulimwenguni ni Marekani na Israel.
 
Pamoja na ujivuni wako kuwa unauelewa mkubwa, nashangaa kuwa unakosa ufahamu wa msingi na wa kawaida. Hakuna namna yoyote unaweza kuzuia matakwa ya mwenye mamlaka.
Aidha kwenye suala la Tigo, unazoom out big time kuunganisha kushambuliwa kwa Lissu na furnishment ya information kutoka Tigo kwenda serikalini. Kwa visibility ya Lissu na context around shambulizi lake- serikali or whatever hakuhitaji msaada wa TIGO kujua Lissu alikuwa wapi.
Kwa upande wa serikali wao hakika walitaka kujua na mimi nina nia ya kujua Lissu alikuwa anaongea na nani nini na kwa faida ya nani. Hayo by itself hayakumpinga Lissu risasi.
Ukipata mda pia pengine usaidie nI utaratibu upi unatumika kupata order ya kupewa contenT ya mawasiliano ya mtu kwa mjibu wa sheria zetu. Naona wengi wanasema tu lazima kuwa na amri ya mahakama
 
Yako mambo hupaswi kuyachokonoa. Kwa vile technology ya ugunduzi imeanzia majeshini, ni muhimu kuwa mzalendo kabisa kwa nchi yako, maana hatuna Tanzania ya pili zaidi ya hii. Hatuwezi kwa vyovyote kujificha kwa password za Max Mello wa jf. Jifiche popote hata Venezuela utapatikana tu. Japo bado, ni hatari sana kusema ukweli kwa watu corrupt. Ukweli unaodondosha tonge la mtu, mamlaka, nafasi ya mtu fulani, utaitwa majina mabaya yote. Ndio maana wa kale walisema ukitaka kumuua mbwa shujaa/mwema, mpe jina baya.
 
Order ya mahakama inahitajika kwa lengo la ku'restrict' haki za kikatiba iwapo serikali inaona inafanya hivyo kwa sababu za kiusalama au 'manufaa ya umma' kwa mujibu wa Ibara ya 30(2)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (kama ilivyofanyiwa marekebisho hadi 2005)
 
Kw
Kwa hiyo Tigo walikuwa na document maalamu za kimahakama au mamlaka rasmi yenye kufuatilia taarifa za wateja wao ???

Na Kama ndivyo kwanini wamekimbilia kukanusha badala ya kusubiri watoe ushahidi mahakamani ???
 
Pamoja na ujivuni wako kuwa unauelewa mkubwa, nashangaa kuwa unakosa ufahamu wa msingi na wa kawaida.
Wewe kujua kuwa mimi nina uelewa na ufahamu, wala sio swala la "ujivuni". Hata wewe ukiamua kutokuwa "mjinga" kwa hiari yako, utaelewa na hakuna wa kukuona "mjivuni" kwa sbb ya ufahamu na uelewa wako...
Hakuna namna yoyote unaweza kuzuia matakwa ya mwenye mamlaka.
Hatuwezi kuwa taifa/nchi ambayo watu wake tunaishi mithiri ya maisha ya simulizi ya "shamba la wanyama". Kwa hiyo, hii hoja yako sio ya kweli na actually sikosei wala sikutusi kusema, kuwa, fikra hizi ni kwa sbb ya ujinga wako tu wa kukosa ufahamu...

There is Limitation of powers kwa "serikali" au "watu wenye mamlaka na maamuzi......"

Mamlaka yao yamedhibitiwa na katiba na sheria mbalimbali....

Sasa kama wanavunja sheria hizi kwa makusudi, hiyo ni hoja nyingine na ni makosa na ndiyo maana tunajadili hapa....
Hapa hata sijakuelewa unasema nini. Ina maana ktk sehemu ndogo ya taarifa ya Bw. Michael Clifford wewe huamini kuwa TIGO ni mshiriki wa jaribio hilo? Kama wewe unakataa, wenzio TIGO wanakiri waliwasaidia wauaji track mawasiliano ya huyu ndugu kwa kutumwa na kiongozi mkubwa wa serikali na sasa TIGO wanatafuta njia ya kujiponya na kashfa hii...
Kwa upande wa serikali wao hakika walitaka kujua na mimi nina nia ya kujua Lissu alikuwa anaongea na nani nini na kwa faida ya nani.
Ili iweje? Walipata nini sasa? Halafu..?
I completely don't understand. What point are you trying to make here....?
Hayo by itself hayakumpinga Lissu risasi.
Na hapa unamaanisha nini? Maana ungekuwa umeambiwa uandike essay na mwalimu wako, sijui ungepata alama ngapi kwa mtiririko huu wa hoja zako ambao uko very unlogical, hau - make any sense at all....
Ukipata mda pia pengine usaidie nI utaratibu upi unatumika kupata order ya kupewa contenT ya mawasiliano ya mtu kwa mjibu wa sheria zetu. Naona wengi wanasema tu lazima kuwa na amri ya mahakama
Hili nalo ni swali la kuuliza kweli?

Tumtumie huyuhuyu Tundu Lissu kama reference yetu...

Magufuli na serikali yake si walikuwa wanadhani kuwa Tundu Lissu ni "threat ya national security", au siyo?

The first thing, walipaswa waeleze ni kwa namna gani ni threat.

Kwa taarifa yako ni kuwa, tangu serikali ya Ben Mkapa, Jakaya Kikwete kisha Magufuli, kumbukumbu zilizopo zinaonesha kuwa Tundu Lissu ameshitakiwa several times kwa makosa ya "uchochezi" na mara zote serikali hushindwa kuthibitisha makosa hayo au huwa wanaamua kuzitelekeza tu hizo kesi.....

Na kama hujui ni kuwa, uchochezi, logically inatupeleka kulekule kwenye dhana nzima "threat to the national security...."

Na infact, majaribio ya mashitaka yote haya huwa wanatafuta mwanya wa kumtengenezea kosa kuu kuliko yote ktk makosa ya jinai, kosa la UHAINI ili afungwe maisha jela au anyongwe mpaka afe....

Kote huko ilishashindikana kwa sababu ktk harakati zote za kutetea haki, kukosoa serikali na watawala anazofanya Tundu Lissu hufanya kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi na kwa hiyo huwezi kukuta elements za uchochezi achilia mbali uhaini...!!

KUJIBU SWALI LAKO SASA, ni kuwa ili upate uhalali wa kisheria kuvunja sheria ya "privacy" ya mtu kuanzia mawasiliano yake na nyumbani kwake, nenda mahakamani, jenga hoja na mshitaki kwanza mtu huyo....

Iambie mahakama kuwa, mtu huyu ni hatari kwa usalama wa nchi/taifa kwa sababu 1, 2, 3 nk hivyo tunaomba "court order" ya kumfanyia uchunguzi wa mawasiliano yake...

Narudia tena kukuambia kuwa, watu wa aina ya Tundu Lissu wenye uelewa na ufahamu si tu wa sheria na katiba na haki zao mbalimbali bali pia uelewa mkubwa historia ya nchi na dunia kwa ujumla ni ngumu kuwanasa ktk mitego ya kisheria maana atakushinda tu...

Huyu bwana (Tundu Lissu) si threat ya national security bali ni threat kwa CCM na serikali yao. Na ndiyo maana walitafuta njia ya kijinga and barbaric ya kumwondoa iliyo kinyume na sheria za nchi na za kimataifa - political assassination & government terrorism act.....
 
Unanisikitisha kwamba hauko honest kwenye mjadala. Haya unayojitungia hayapo kwenye hija yangu.
Am I not honest..?

What exactly do you mean...?

Kwani hoja yako wewe uliyoianzisha mwenyewe msingi wake ni nini...?

Swali nililokuuliza lina ugumu gani wewe kujibu...?

Wewe ndiye ambaye hauko honest, unatumia ulaghai wa hoja kudanganya wasio na uelewa na ufahamu wa ABC za sheria zetu...
 
Kwanini umechagua ujinga just to
Justify ujinga ?
 
Umeshindwa swali ukaamua kujitungia la kwako.
 
KYC.
KNOW YOUR CUSTOMER.
Hii ndio inatumaliza.
Walishawahi kunichorea ramani.nikafuatwa mpaka nilipokaa.
Unashangaa tu gari hilo.
 
Unaweza kutupa mfano wa kesi za kupata court order ili kuweza kupata mawasiliano ya mtu
 
Unaweza kutupa mfano wa kesi za kupata court order ili kuweza kupata mawasiliano ya mtu
Huhitaji kuchimba historia ya kesi za nyuma...

Mojawapo ni hii inayoendelea sasa ya Ex Mayor Boniface Jacob wa CHADEMA vs Polisi...

Boniface Jacob amekataa kuwapa acces polisi ku - intrude privacy ya mawasiliano yake ya simu....

Police wameiomba mahakama itoe amri ya kisheria (court order) kumtaka Biniface Jacob atoe access ya simu zake ili zichunguzwe...

KUMBUKA: Amri hii haitolewi tu kwa kuwa polisi wametaka hivyo simply tu kwa sbb wao ni polisi. Amri hii hutolewa kwa kujenga hoja za kisheria na mahamkama ikiona hoja zako zina make sense, inaweza kutoa amri hiyo....

Hata polisi wanapokuja ku - search nyumbani kwako, lazima wawe na amri aidha ya mhakama au afisa fulani mkubwa wa polisi kwa cheo chake anayetambuliwa na sheria...

Hata kwa Tundu Lissu mwaka 2017 utaratibu huu wa kisheria ndiyo ulipaswa ufuatwe...

Lakini cha ajabu Magufuli, mtu mzima kabisa na akili zake timamu, msomi na Rais wa nchi aliyeapa kuilinda katiba akaamua kufanya ujinga na upumbavu ule kutaka kuua mtu kwa interests zake binafsi za kisiasa tu kwa kisingizio cha "usalama wa nchi..."

Huo ulikuwa ni ujinga na wehu kwa 100%...
 
Cabinet Office files released in 2013 show that on or before 5 December 1936, the Home Secretary, Sir John Simon, had ordered the General Post Office (which controlled British telephone services) to intercept "telephone communications between Fort Belvedere and Buckingham Palace on the one hand and the continent of Europe on the other"
 

Moderator tunaomba post hii iwe ya kwanza ktk uzi.

..Posti hii inatoa ELIMU kubwa na ufafanuzi mzuri kuliko post ya mtoa mada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…