Vyombo vyetu vya habari mmeshindwa kufafanua hii?

Vyombo vyetu vya habari mmeshindwa kufafanua hii?

pombe kali

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
312
Reaction score
616
Barua inayotoka ZARA yaani mamlaka ya kodi ya mapato Zambia ambayo nami naiambatanisha haijakusudia kufunga mpaka wala haina mamlaka ya kusimamia ulinzi mipakani, one border post maana yake ni kituo Kimoja cha forodha, na Ndicho kilichofungwa, wakati uhamiaji wakiendelea na shughuli zao za ulinzi wa mipakani.

Sababu ya malori kulundikana ni kwa sababu yana mizigo ambayo inatakiwa ipitie taratibu za forodha na ofisi za forodha zilizopo mpakani kusitisha huduma nashangaa kuna vituo vikubwa vya habari wametumia barua hii kwa tafsiri ya kuwa Zambia wamefunga mpaka ina maana TRA wakifunga ofisi ya mpakani maana yake ni kwamba mpaka umefungwa?

Shughuli za kibinadamu ziko pale pale zilizositishwa ni shughuli za forodha na kama mpaka ndio ungefungwa hilo ni swala la kidiplomasia ambapo wizara ya nje ya Zambia ingewasiliana na mamlaka au barua inayozunguka mitandaoni ingekuwa imetoka kwa msemaji wa serikali na sio mamlaka ya mapato yaani ZARA

View attachment 1450496
 
Sijui nikagongee nyagi au nikagongee banana.....

KONI NGUZA MBOCHI
 
Back
Top Bottom