Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Wakuu,
Mtu analipia basi luxury kupata huduma extra, nzuri na bora, asafiri akiwa anajisikia huru. Inakuaje unalipia kusafiri basi luxury halafu unakutana na choo kama hiki? Choo hiki ni kwa huduma ya haja ndogo pekee na hauruhusiwi kuingiza tishu/toilet paper na haiwekwi kabisa chooni lakini unaruhusiwa Kwenda na yako, ukitakiwa kuiweka kwenye chombo cha taka chooni humo.
Choo hakina maji, koki haifanyi kazi kama mnavyoona kwenye picha, mlango ni wa kujiegesha; yaani inabidi uushikilie muda wote ambao unatumia choo hiko la sivyo unaweza kufunguka muda wowote wakati unafanya mada zako ukaaibika. Na kutokana na Malalamiko ya watu huduma hii iko hivi muda mrefu, sasa abiria wanalipia pesa ya luxury ya nini kama huduma haziboreshwi?
Mmewafikiria wanawake kwenye huduma hii? Wanawake hasa wakiwa katika vipindi vyao mwezi wanahitaji sana kuwa na maji kwenye huduma ya choo. Sasa ndio yuko kwenye kipindi chake akaenda kutumia hiko choo kuna usalama hapo?
Ni uchafu wa hali ya juu, unaingia mzima unaondoka na U.T.I sugu
Choo katika Basi la Kidia One Express wanakutoza Tsh. 45,000/- kwa huduma ya luxury
Kwa wenye uzoefu na mabasi Luxury/V.I.P kutoka kampuni nyingine hali ikoje?