Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Hoja ya awali ~ Abiria Mwendokasi-Kivukoni walazimika kutumia korido kujisaidia haja ndogo kutokana na vyoo kutofanya kazi
Kama ilivyokawaida kutumia kituo hicho, leo majira ya asubuhi nimepita katika kituo hicho na kushuhudia ukarabati wa vyoo hivyo umeanza. Ndani ya vyoo hivyo kuna mafundi wanaoendelea na kazi ya kufanya maboresho.
Kwa kweli, litakuwa jambo jema huduma hizo zikirejea, kwani abiria wengi tumekuwa tukipata usumbufu mkubwa pale tunapobanwa na haja ndogo.
Maana ni dhairi ilikuwa inaonekana kabisa uwepo wa uzembe wa wazi kwa baadhi ya watendaji kutowabijika ipasavyo kushughulikia jambo hilo ambalo ni kilio cha muda mrefu.
Wito wangu ni kwamba ukarabati huo uharakishwe ili huduma zirejee haraka, kwani kero hiyo imekuwepo kwa muda mrefu bila kutatuliwa jambo ambalo limesababisha usumbufu mkubwa, ikiwemo kuwalazimu baadhi ya watu kujisaidia katika mazingira yasiyo salama kiafya kama mdau alivyodai kwenye andiko lake.