Vyoo maeneo ya stendi na sehemu za wasafiri kulia chakula havikidhi vigezo. Mamlaka ziingilie kati

Vyoo maeneo ya stendi na sehemu za wasafiri kulia chakula havikidhi vigezo. Mamlaka ziingilie kati

christeve88

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2018
Posts
3,333
Reaction score
5,490
Kwanza kabisa nianze kwa kumpongeza Mh. Rais kwa kuteua kuiongoza hii wizara, hakika Mh. hajakosea kukupa hii nafasi kutokana na uwezo wako mkubwa wa kiuongozi uliouonesha ndani ya hii wizara ndani ya muda mfupi. Wengi tulikuwa hatukufahamu hivyo Mh. Rais kukuibua wewe imeonesha ni jinsi gani Mh. anajua kuibua watu makini hata kama hawapo kwenye mifumo ya kisiasa. Sina mashaka na kasi yako hasa ukizingatia kina mama wa Singida hasa wanyiramba na wanyisanzu huwa ni wanawake wa shoka haswa tuliolelewa na hawa wamama tunalielewa hili.

Mh. Waziri kero yangu ni hivi vyoo vya Halmashauri hasa vilivyopo maeneo ya stendi na vile vilivyopo kwenye vituo vya kulia chakula hasa kwa wasafiri wa mikoani. Kwa kweli sehemu kubwa ya hivyo vyoo havikidhi taratibu za kiafya, hali ya hivi vyoo kwa baadhi ya mikoa kwa kweli ni mbaya na nirahisi hata kupata magonjwa ya kuambukiza kama UTI.

Hali ya usafi wa vyoo Mh. Waziri ni mbaya hasa mikoa ya nyanda za juu kusini ni kama hakuna ma bwana afya huku, sio jiji wala halmashauri vyoo vyao havirizishi, kibaya zaidi kuna watu wanakusanya pesa na wanazuga na mashine ya EFD ukidai risiti wakati mwingine wanasema mashine mbovu au watakusubirisha hapo kama dakika mbili, maajabu ni juzi hapa katika wilaya moja ya Tabora ni Sikonge kama sikosei tulilazimika kuchangakia matundu ya choo wanawake na wanaume hii kwa kweli ilinitisha sana tena choo chenyewe hakikuwa na ubora hata kidogo.

Ombi langu kwako Mh. Waziri kama ikiwezekana wizara yako itoe muongozo wa ujenzi wa vyoo vya kulipia, ambao kila Hamashauri na vituo vya kulia chakula kwa abiria vitautumia katika kujenga vyoo vyao, vyoo ambavyo vitazingatia na walemavu pia. Viwe ni vyoo vya kisasa vyenye huduma zote za msingi, choo ambacho hata mtoa risiti atapewa chumba chake humo ndani, tofauti na sasa ambapo mkata risiti anajifacha unakuja kumuona saa ya kudai pesa tena anakuja kutoke Kaskazin au mashariki wala hana hata sare na risiti hajaziandaa.

Nchi yetu imeingia kwenye uchumi wa kati ni vyema na huduma zetu zikawa za kisasa tuwe mfano kwa wageni wanaoingia na kutoka ndani ya nchi yetu. Kufanya hivi tutapunguza magonjwa kama UTI na mengine megi yatokanayo na uchafu.

Natanguliza shukrani.
 
Back
Top Bottom