KERO Vyoo vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar vinahitaji maboresho, angalia hali ilivyo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Licha ya kuwa Viongozi wengi wa Kiserikali wamekuwa mstari wa mbele katika kusisitiza usafi kwenye mazingira ya ofisini na hata kwenye makazi ya watu lakini upande mwingine wapo ambao huwa wanasahau kujitazama wao.

Hivi ndivyo hali ilivyo katika Vyoo vilivyopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, vyoo hivi vinatumiw ana wageni na hata Watumishi mbalimbali, vipo eneo la nje katika jengo la Ofisi hiyo.

Nadhani ni vema RC na timu yake wakalitazama hili, suala la usafi ni muhimu, hapa nimekuta mabomba mabovu, vyombo vilivyomo kwenye Vyoo havina mazingira mazuri ya usafi, maji kwa nje hakuna licha ya kuwa kuna masinki ambayo yalianza kutumika wakati ule wa Corona.

Hakuna taa na inaonekana usafi unaofanyika ni ule wa juujuu.

Your browser is not able to display this video.




 
Rekebisha, "vyoo vya public" siamini mkuu wa mkoa anatumia hivyo vyoo!
 
Kata gogo kwenuuu ... hahaaaaa

Umuhimu wa choo utautambua ukipatwa tumbo la kuvurugikaaa ama kojo la mara kwa mara
 
Hayo ni matunda ya kuwa na wakuu wa mikoa wapumbavu ndiyo maana mji wa dar es salaam unanuka sikuizi toka JPM aondoke kama mkuu wa mkoa haoni tatizo hivyo vyoo unategemea nini ....kwa mkoa
 
Havina shida ,umetumia kigezo gani kuhusu usafi.
Kama vichafu dawa moja tu kulipia awe mfanyakazi au wa nje haendi ofisini kunya au kukojoa awe mkuu wa mkoa au yeyote walipie kama kweli vichafu awepo msafisha vyoo wa kulipwa
 
Hawa ukiwakuta wanakamata vyoo visivyo na viwango mtaani ni wakali kama chui
Ila Sasa vyoo vya ofsi zao ni majalala
 
Bora kubaki nayo nyumbani kuliko kutumia vyoo vya public,utaishia kubeba magonjwa kama UTI etc.
Mimi huwa nazunguka nayo mpaka nonprofit home.
Mkuu hujawahi kushikwa na tumbo la kuhara ukiwa kwa public ?πŸ’
 
Na hiyo ni sehemu nyingi TZ zipo hivyo, angalia na watu wenyewe Sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…