BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Licha ya kuwa Viongozi wengi wa Kiserikali wamekuwa mstari wa mbele katika kusisitiza usafi kwenye mazingira ya ofisini na hata kwenye makazi ya watu lakini upande mwingine wapo ambao huwa wanasahau kujitazama wao.
Hivi ndivyo hali ilivyo katika Vyoo vilivyopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, vyoo hivi vinatumiw ana wageni na hata Watumishi mbalimbali, vipo eneo la nje katika jengo la Ofisi hiyo.
Nadhani ni vema RC na timu yake wakalitazama hili, suala la usafi ni muhimu, hapa nimekuta mabomba mabovu, vyombo vilivyomo kwenye Vyoo havina mazingira mazuri ya usafi, maji kwa nje hakuna licha ya kuwa kuna masinki ambayo yalianza kutumika wakati ule wa Corona.
Hakuna taa na inaonekana usafi unaofanyika ni ule wa juujuu.