KERO Vyoo vya Stendi Kahama ni mfano jinsi vyoo vingi vya public visivyo salama na hatari kwa afya za watumiaji

KERO Vyoo vya Stendi Kahama ni mfano jinsi vyoo vingi vya public visivyo salama na hatari kwa afya za watumiaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
12,463
Reaction score
27,556
Habari za Leo Waungwana.

Ni hivi nimezunguka karibia ya 96% ya mikoa ya Tanzania lakini ajabu ni kwamba Vyoo vya stendi zote hadi pale Dodoma ile Stendi Kuu ya kisasa kabisa ni pachafu na si salama, licha ya kuwa tunatoa hela kupata huduma ya kujisaidia.

Ukiingia kwenye Vyoo hivi ukakaa hata kwa dakika 3 utatoka unanuka halafu mbaya.

Vyoo kama vya Kahama Cdt na Kahama mabasi ya mkoa, hivi vyoo vinatakiwa vifungwe maana si salama kabisa ni vichafu ambapo unaweza kutoka na magonjwa ya kuambukiza!!

Hiki nisemacho ni kweli na nina ushahidi nacho, hizo stendi kila nikipita mambo ni yaleyale.

Stendi za mpanda Katavi havifai pananuka vibaya.

Nauliza hela hizi zinapelekwa wapi yaani kununua dawa na sabuni zenye malashi mnashindwaje?

KERO nyingine ni kupaki hapohapo ombaomba ili hali eneo lile si salama pananuka na pachafu mwataka hao walemavu waugue na magonjwa mengine tena?

Kahama, Mpanda na Igunga na kwingineko acheni tamaa na upumbavu wenu mnasababisha tuondoke na magonjwa ya kuambukiza kwenye vyoo vyenu.

Mbaya zaidi hata zile choo tunazopitishwa na wenye magari nazo ni chafu unakuta maji hakuna pananuka hakuna mfano!

Hii KERO yangu iwafikie wahusika wote. Naomba ipostiwe na kwenye mitandao ya kijamii mingine.
PXL_20260215_072235145.jpg
PXL_20260214_141931312.jpg
PXL_20260214_141904412.jpg
PXL_20260214_141909483.jpg
 
Naunga mkono hoja. Hali inatisha. Geita, Biharamulo, Ngara ni kiboko tena ktk hali hiyo nilikuta mtu ameuchapa usingizi hatari!

Nenda Kakonko au Kasulu utashangaa kuna watu wanaitwa bw/bi Afya na wanalipwa mishahara!
 
Back
Top Bottom