A
Anonymous
Guest
Vyoo vinavyotumiwa na abiria pamoja na watu mbalimbali ndani ya Stendi ya Mabasi ya Nyegezi Jijini Mwanza, havina huduma ya maji safi na salama kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja, taarifa ikiwa ni kwa mujibu wa wafanyakazi na Wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao ndani ya stendi hii ya kisasa.
Watoa huduma wa vyoo hivyo, wanalazimika kununua maji ya madumu kutoka maeneo jirani na kujaza baadhi ya vyoo, lakini kwa sababu ya wingi wa abiria, maji hayo yanaisha baada ya muda mfupi na hivyo kuathiri huduma zote katika vyoo hivyo, na hali inakuwa mbaya zaidi nyakati za usiku ambapo wauza maji wanakuwa wamefunga.
Uongozi wa Jiji la Mwanza utafute kiini cha tatizo na kutatua ili kuhakikisha usalama wa afya ya watumiaji wa vyoo hivyo.
Pia soma ~ MWAUWASA: Kulikuwa na hitilafu katika Stendi ya Mabasi Nyegezi (Mwanza), huduma ya maji imerejea