Nyegezi yote kero tupu! Hususani mitaa ya Nyegezi stendi yote !! Jamii forum njooni mjionee wenyewe kero hii imekua ikisemwa sana humu na hakuna utatuzi, mamlaka ziko kimya! Na wanakuja kutoa majibu simple sana kwa uhai wa watu. Nyegezi na mitaa yake yote maji yakitoka siku Moja mnakaa mwezi na kitu bila maji alafu wanajibu kirahisi sana Hitilafu ! Hitilafu Kila mwezi!!!!!!!!
Kama wanaona hawawezi tatu shida hii hapa mjini tene Nyegezi na mitaa yake je huko vijijini!?? Kwakweli mamlaka ya maji Jitafakarini haiwezekani Kila wiki itokee hitilafu mnakaa mwezi mzima bila maji alafu hakuna taarifa.
Au tangazieni watu maji yanauzwa basi tuanze kukodi matorori kunua maji kuliko huduma hii mbovu!
Wasitujibu kirahisi wakati mitaa wanayo ishi wao maji yapo hakuna hitilafu, au isikike kiongozi mkubwa anakuja maji yanatoka Kila mahala mpaka unashangaa au mwenge upite uone maji yanavyo toka.