KERO Vyuo havi-update kwa wakati taarifa za Diploma kwenye Mfumo wa NACTE. Ukiomba ajira Serikalini, mfumo haukutambui

KERO Vyuo havi-update kwa wakati taarifa za Diploma kwenye Mfumo wa NACTE. Ukiomba ajira Serikalini, mfumo haukutambui

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni Mwanafunzi wa Chuo kimoja hapa Dar es Salaam, ninasomea Stashahada Mwaka wa Pili..... nilikuwa na changamoto au kero kuhusiana na usajili wa Vyuoni na NACTEVET ambapo hata mimi nimekutwa na hiyo changamoto na mpaka sasa haijafanyiwa kazi.

Vyuoni humu wanatabia ya kutusajili Wanafunzi wa Diploma katika system ya chuo tu bila kupandisha taarifa zetu NACTE kitu ambacho kinakuwa changamoto kwetu, baada ya kumaliza Diploma na kutaka kuomba kazi hasa katika mifumo ya Serikali inakuwa inakutema kwa sababu NACTE hawakutambui au pale unapotaka kuendelea na Shahada (Bachelor Degree) inakuwa changamoto kupata AVN Namba.

Tunaomba tafadhali Waziri wa Elimu na Mamlaka nyingine zinazohusika kufanyia kazi suala hilo ili changamoto ifanyiwe kazi haraka.

Wazazi wanajinyima kutulipia ada kisha mwisho wa siku unakuja kukutana na changamoto kama hizi wakati ada ulilipa kwa wakati.
 
Back
Top Bottom