Vyuo Vikuu vya Tanzania vinazalisha zaidi wahuni kuliko hata wasomi

Vyuo Vikuu vya Tanzania vinazalisha zaidi wahuni kuliko hata wasomi

Tafsiri nyepesi ya chuo kikuu ni sehemu inayotoa elimu huru. mwanafunzi anakuwa huru katika masomo yake na usimamizi wake binafsi.

Yaani hapa mwanafunzi anaenda kusoma pasi na usimamizi mkubwa kutoka kwa walimu wake.

Lakini kwa nchi yetu hii elimu ya vyuo vikuu naona kama haipo sawa na inaenda kutuzalishia single mother, wadada wanaojiuza mitandaoni wengi.

Msichana ambae tunamtoa mtaani akiwa na heshima zake akifika chuoni anabadilika mazima. mwanzo tulikuwa na mtoto ambae anajistili anavaa vizuri nguo za maadili lakini akifika chuo anakuwa mtu wengine kabisa.

Na ubaya wa mambo tumeshindwa kujitofautisha kati ya sisi na wazungu. wenzetu wazungu walishatengeneza mfumo wa maisha ambao unaenda kumuandaa mtoto akifikisha miaka 18 atakuwa mutual kwa kujielewa na kujitegemea.

Lakini sisi Afrika mtu akifikisha miaka 18 huyu bado ni mtoto na sio mutual afrika mutual tunaanza kumpata akifikisha miaka 26+ .

Sasa mtu anafika chuo anaenda kuachiwa huru kwa imani kuwa anajielewa . anaenda kupewa condom eti ajikinge hapa huyu mtu aendi kujikinga tunaenda kutengeneza mazingira kuwa ngono aone ni kitu cha kawaida kama kunywa maji tu.

Hatimaye leo hii wanawake wengi wanaojiuza mitandaoni ( Telegram Groups & WhatsApp Groups).

Ni wanafunzi wa chuo leo hii single mother wengi tunawapata kutokea chuo. Sasa kuna mda tunashindwa kuelewa kuwa tunatengeneza wasomi au kizazi cha ovyo ambacho tutakiita wasomi.

Leo hii tuna imani kuwa mtoto wako ili afaulu vizuri zaidi nadhani kila mtu atatamani mtoto wake akae na msomi lakini wasomi wetu ndio hawa ambao wanajiuza mitandaoni.

Leo hii ukitaja chuo kama IFM nadhani kila moja anajua wanafunzi wake wana sifa gani. sasa hili swala alienda kulichafua chuo tu ila linaenda kuwa kubwa mpaka linaenda kuichafua nchi. baada ya miaka 10 baadae.

Kama hakuna mabadiliko yatakayochukuliwa basi sifa ya vyuo vikuu vya Tanzania vitasifika kwa sifa za ovyo.

i. Kuna haja ya kuwa makini na wanafunzi tuuwe huu utaratibu wa kuwaachia hawa wanafunzi huru sana. tuwe kama kile chuo cha kule Zanzibar ( Suza).

ii. Kuna haja ya kuwa na somo maalum la ushauri na saa. ili swala la ushauri tusikichukulie dogo.

Akili ya binadamu ufanya kazi pale inapokumbushwa kumbushwa mfano rais wa nchi yoyote lazima awe na washauri wa raisi.

Kwa sababu ishajulikana kama akili ya binadamu ajakamilika na anaitaji ushauri na kukumbushwa kila baada ya mda.

Leo hii nchi hii ina uhaba wa watoa ushauri.

Tuna namba kubwa ya madkatari na walimu lakini hatuna washauri . Leo hii matatizo mengi yanatokea uwenda ni kwa sababu ya kukosa ushauri tu.

Serikali inaenda kupambana na kufungua Soba houses nyingi ili kupunguza waathirika wa madawa ya kulevya wakati serikali ilitakiwa kwanza kudhibiti kizazi kipya cha watumiaji wa madawa. kwa kupewa ushauri .

Leo hii tuna waarifu wengi na kesi ni zilezile zinazofanana . je kuna mtuhumiwa hata moja aliyewahi kukamatwa na kuulizwa au kushauriwa zaidi yake atapigwa tu basi.

Je, kumpiga mhalifu ndio njia ya kumfanya aache uhalifu ?

Serikali na wizara ya elimu iweke somo la maalum linatakuwa linatoa ushauri kwa wanafunzi japo kwa week mara moja tu wanafunzi asijisahau chuoni kafata nini

iii. Sheria na ugakuzi wa mara kwa mara.

Hapa lazima tuwe wakali tu kama tunataka kutengeneza kizazi ambacho kweli kitatunufaisha baada sheria lazima ziwe kali. kwa wanafunzi wote ambao watafunja sheria za chuo.

Wanafunzi wasipewe uhuru sana kiasia ambacho hata huko makwao hawana uhuru uo mbele ya wazazi wao. lazima awe chini ya usimamizi afrika afrika mtu hata awe na miaka 50 lakini akiitwa wanafunzi / wanachuo basi anaitaji uangalizi tu .

Uwekwe utaratibu maalum wa kuwa kuwakagua wanafunzi afya zao kila baada ya mda fulani. ( vipimo vya ujauzito na magonjwa ya ngono ).

Ili jamii yetu ikuwe na tuendelee basi kwanza lazima tuishi kwenye mfumo wetu halisi wa maisha yetu hatuwezi kucopy mifumo ya maisha ya Marekani na Ulaya alafu tujisifu tumeendelea, tunaenda na wakati .

Hatuwezi kuendelea kwa kucopy mfumo wa watu wa maisha afrika au waswahili mfumo wetu wa maisha hauruhusu watoto wa kike kuvaa nguo fupi kuvaa nguo zinazobana . huku ni kupotea na athari zake ni kubwa tunaenda kuzalisha kizazi kimoja cha ajabu sana huku baadae.

Tukiendelea hivi hivi tujiandae kuona namba kubwa ya single mother , watoto wengi wa mitaani , mateja , mashonga na wauni wengi tu ambae tunaenda kuwapa nchi tukiamini kuwa wameelimika kumbe wamehitimu tu elimu ya juu.

Asanteni .
Nawasilisha.
UMESEMA VEMA SANA, Ally.

Lakini:-
Unadhani hata wahusika wakisoma andiko lako kuna mtu anajali?????
 
UMESEMA VEMA SANA, Ally.

Lakini:-
Unadhani hata wahusika wakisoma andiko lako kuna mtu anajali?????
kuongea jengine na kutendea kazi swala jengine ila acha nitimize wajibu wangu wa kuongea . wenye kuzingatia watazingatia wenye kupuuza watapuuza
 
In countries like Lebanon it's not normal Kila mtu anakula kivyake na kwa muda wake nooope familia lazima ikae dinner mom here daddy here brother there, unawaona watoto wako if they have problems they will share with you and it's where family love beggings in case Kuna changes za watoto utaona.
Ndio maana nasisitiza Kila kituo kinaanzia nyumbani.
ni wazo zuri sana na nakubaliana na ww
 
ni kwel tuanzie kweny family level coz hapa ndo kwenye shina ila chuo pia kinachochea mabadiliko kwa wanafunzi hakun sheria inayomkea wanachuo kwa kitu chochote kile.

ngono vyuon linaonekana ni jambo la kawaida tu
Approximately kwa Tanzania mtu alieabza la kwanza miaka 7 anaingia degree na miaka 20 huyo tayari ni mtu mzima chuo anapita TU kufanya finalizations Professor can't tell him or her nothing.
 
Solutions

1.Vyuo viache kuajiri malecturer wenye matokeo mazuri darasani mwalimu anatakiwa kuwa na skills kama

. presentation skills
. Good communication skills
. Creativity
. Well informed

unaajiri mwalimu ana GPA ya 4.5 hana skills zote hapo juu alafu anapenda ngono balaa whad you expect

2. Toa kitu inaiwa General study (GS) na Development study (DS) ingiza kitu inaitwa Moral study from early child hood to chuo kikuu

3. Encourage Courses that reflect real life experience toa hayo makozi ya hovyo

4. Not everyone deserve a bachelor degree fanya screening ya maana kwa watu waingiao vyuoni
 
Approximately kwa Tanzania mtu alieabza la kwanza miaka 7 anaingia degree na miaka 20 huyo tayari ni mtu mzima chuo anapita TU kufanya finalizations Professor can't tell him or her nothing.
hizi ni nadharia kuwa kwa tz mtu akifikisha 20 years anajielewa. lakini reality kuwa bado huyu mtu sio mutual hawez kujilewa wala kujitegemea wenyewe coz hajatengenezewa mazingira tokea hapo mwanzo.

ndo maana thamani ya mwanaume Tanzania inaonekana kuanzia miaka 25+ hapa ana uwezo wa kujitegemea 95%
 
Solutions

1.Vyuo viache kuajiri malecturer wenye matokeo mazuri darasani mwalimu anatakiwa kuwa na skills kama

. presentation skills
. Good communication skills
. Creativity
. Well informed

unaajiri mwalimu ana GPA ya 4.5 hana skills zote hapo juu alafu anapenda ngono balaa whad you expect

2. Toa kitu inaiwa General study (GS) na Development study (DS) ingiza kitu inaitwa Moral study from early child hood to chuo kikuu

3. Encourage Courses that reflect real life experience toa hayo makozi ya hovyo

4. Not everyone deserve a bachelor degree fanya screening ya maana kwa watu waingiao vyuoni
Perfect chief 🤜🤜🤜
 
hizi ni nadharia kuwa kwa tz mtu akifikisha 20 years anajielewa. lakini reality kuwa bado huyu mtu sio mutual hawez kujilewa wala kujitegemea wenyewe coz hajatengenezewa mazingira tokea hapo mwanzo.

ndo maana thamani ya mwanaume Tanzania inaonekana kuanzia miaka 25+ hapa ana uwezo wa kujitegemea 95%
I concur with you, It's for some of them ambao at the age of 23 they can come with a business idea and implementation
 
Ukipewa chakula unakula
Sasa ina maana wewe chuo kama ulipitia ukapewa unga utatumia sabb tu umepewa
tafsiri yangu ukipewa condom wakat kuna kishawish cha kike mbele akili yako utawaza kuitumia na sio kuiweka ndan swala la sex sio swala la akili ni swala la emotional zaidi unawez kumwaga ndani alafu ukajuta baada.

swala la unga unaweza kutumia kutokana na mood uliyokuwa nayo mfano ukiwafata watuamiaj weng wa unga watakwambia sababu za kutumia ni vishawishi na msongo wa mawazo.

sasa unampa unga mtu wenye mastress kichwan alafu unamwambia ukitumia hii kitu uta feel G unategmea nn
 
I concur with you, It's for some of them ambao at the age of 23 they can come with a business idea and implementation
Thank you for understanding me, except for this concept that a child who reaches 18 years old is an adult.

haipo tunaitaj km miaka 10 mbele kuifikia
 
hizi ni nadharia kuwa kwa tz mtu akifikisha 20 years anajielewa. lakini reality kuwa bado huyu mtu sio mutual hawez kujilewa wala kujitegemea wenyewe coz hajatengenezewa mazingira tokea hapo mwanzo.

ndo maana thamani ya mwanaume Tanzania inaonekana kuanzia miaka 25+ hapa ana uwezo wa kujitegemea 95%
Sio kweli bruh
Labda kwa shule zetu hizi za kayumba ambapo mtt anaenda tu shule na kurudi hana timetable yoyote yeye ilimradi kengele ilie arudi na nyumbani hakuna ufuatiliaji
Ila shule nyingine mazingira na timetable za pale zinamjenga mtt kuanza kufikiria kama mtu mzima akifikisha 10 12 yrs tayari anajielewa
 
Labda vyuo vimetofautiana.

Tatizo la wanafunzi kujiuza halipo kama watu wanavo taka kulielezea hapa. Nimesoma SUA na kuona jamii ya pale inavoishi.

Wanafunzi wengi hawajiuzi, kuna mahusiano kati ya wanafunzi kwa wanafunzi(sehemu kubwa), Wanafunzi na watu wazima(staffs na nje ya chuo) - hawa ndo mnawaita wadangaji.

Makundi yote hayo mawili yapo kwenye jamii yeyote ile sio tu jamii ya wanafunzi, hivyo sio kitu cha kustaajabu.

Hili jambo watu wabalikuza sana na kufanya jamii iamini kika binti alieko chuoni ni ana jiuza/Danga. Kitu ambacho sio kweli.

Ova.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
ndani ya watu million 61 . asilimia kubwa ni masikini kuna interview moja ya Jk kikwete aliojiwa akaulizwa unasikitika kitu gani ambacho umekiona akijabidilika ndani ya awamu yako.

alisema nasikitika kuacha nchi ikiwa bado ina masikini wengi sana.

mkuu huku darasa moja lina wanafunzi 400- 450.

watoto hawa 400 inawezekana 10 tu ndo wanatime table nyumbani kwao.

ukweli ni kwamba tunapeleka chuo watoto wengi wa kimasikini ambao bado hawajielewa pia hawawezi kujitegemea na wengi wao wanasoma kwa ada kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu
 
Labda vyuo vimetofautiana.

Tatizo la wanafunzi kujiuza halipo kama watu wanavo taka kulielezea hapa. Nimesoma SUA na kuona jamii ya pale inavoishi.

Wanafunzi wengi hawajiuzi, kuna mahusiano kati ya wanafunzi kwa wanafunzi(sehemu kubwa), Wanafunzi na watu wazima(staffs na nje ya chuo) - hawa ndo mnawaita wadangaji.

Makundi yote hayo mawili yapo kwenye jamii yeyote ile sio tu jamii ya wanafunzi, hivyo sio kitu cha kustaajabu.

Hili jambo watu wabalikuza sana na kufanya jamii iamini kika binti alieko chuoni ni ana jiuza/Danga. Kitu ambacho sio kweli.

Ova.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
Shukrani mkuu kwa kuanza na neno

"Labda vyuo vimetofautiana"..

swala la kujiuza kwa watoto wa chuo halipo wazi sana kama hawa dada zetu ambao unajua ukienda sehem fulani kama TEMEKE SUDAN, UWANJA WA FISI, RIVER SIDE utawakuta wamepangana wanasubiri wateja.

Swala la watoto wa chuo biashara zao zinaenda kwa akili aidha kuna agent au huyu mwanafunzi ana mahusiano na mbaba mtu mzima wenye maisha yake.

tafisri ya ndani kabisa huyu mwanafunzi ana date na mbaba wenye family yake inakuja kuwa huyu bint ana mapenz ya kwel na huyu bwana ila bint yupo kwa ajili ya kupata pesa.

Sasa hili ni swala laa wazi kuwa huyu dada anajiuza maana yake anatoa penzi ili apate pesa
 
Walimu wanaoomba rushwa ya ngono ni wahuni.
Wanafunzi wezi wa mitihani ni wahuni.
Wanafunzi wanaotoa rushwa ya ngono ili wafaulu ni wahuni.
Wanafunzi wanaoandika xaxa badala ya sasa ni wahuni.
Wanaoandika xaxa badala ya sasa ni janga kubwa sana siku hizi, huwezi kutofautisha mwandiko wa graduate na darasa la tano
 
Hii nchi inakumbana na changamoto nyingi zinazosababishwa na utandawazi. Hivyo mtu conservative kama ndugu Ally Nasoro unayeona kwamba kuvaa nguo ndefu zisizobana ndo maadili ya kupigania, huwezi kuelewa vijana wanaograduate.

Wadogo zenu wanavaa mijuba na kutoa shkamoo za kutosha ila laiti ungewahi “kusocialize” vizuri na hao vijana wa kike by the time wanahitimu sekondari, basi ungejua kwamba hamna chocho ya ‘uhuni’ as you put it ambayo hawaijui. Wanawaektia tu huko nyumbani.

Wakija chuo wanapata uhuru wa kufanya mambo ambayo wamekuwa wakitamani kuyafanya muda mrefu tu.
 
Back
Top Bottom