Vyuo vya Kati kuna ubabaishaji mwingi, mfano malipo ya ‘Sup’ yamegeuzwa kitega uchumi

Vyuo vya Kati kuna ubabaishaji mwingi, mfano malipo ya ‘Sup’ yamegeuzwa kitega uchumi

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Mimi ni Mzazi wa Mwanafunzi anayesoma mojawapo ya chuo cha Kati Ngazi ya Diploma ya Udaktari, moja ya changamoto kubwa katika vyuo hivi ni matumizi mabaya ya malipo yanayofanyika kwa ajili ya kurudia mitihani ambayo Mwanafunzi amefeli.

Ukifuatilia katika mamlaka ya NACTE wao maelekezo yao Mwanafunzi anatakiwa kulipia kati ya Shilingi 140,000 hadi 145,000 lakini vyuo vingi vya kati gharama zao za kulipia Sup ni kuanzia Shilingi 200,000 hadi 400,000 kwa Mwanafunzi mmoja, jambo ambalo linawaumiza Wanafunzi wenyewe na wale ambao tunawalipia.

Natoa wito kwa NACTE kuwa wanatakiwa kutambua malipo ya Sup kwa sasa yamekuwa yakitumika kama kitega Uchumi cha chuo kuingiza fedha, ikiwa hivyo inamaanisha kuwa Mwanafunzi anaweza kufelishwa ili tu chuo kipate fedha.

Moja kati ya chuo chenye changamoto kwenye masuala ya Sup kwa kulipisga gharama kubwa ni Nyaishozi ambacho kipo Kinondoni.

Changamoto nyingine ni mifumo ya uendeshaji kuanzia usajili wa Wanafunzi, matokeo na utoaji vyeti kuna ubabaishaji mwingi, pia hata huduma kwa wateja namba zao nyingi zinazowekwa kwenye matangazo ama hazipokelewi au hazipatikani kabisa.
 
Kiufupi vingi vinaumiza sana mm ni mhanga wa hayo mambo usidanganywe hasa vinavyoendeshwa kwa mgongo wa dini ni balaa utajiraumu kwa nini umeenda kupata elimu hapo
 
Back
Top Bottom