DOKEZO Vyuo vya Kati vya Afya kuna ufelishaji Wanafunzi kwa makusudi?

DOKEZO Vyuo vya Kati vya Afya kuna ufelishaji Wanafunzi kwa makusudi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Vyuo vingi vya Kati vya Afya na Sayansi Shirikishi kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za wanafunzi, wapo wanaofelishwa makusudi katika mitihani yao ya practical.

Walimu wanatumia nafasi hiyo hasa kwa wanafunzi waliotofautiana nao au waliowatongoza wakawakataa, matatizo binafsi ya Walimu na bifu kwa wanafunzi wanaotambua haki zao, Serikali ifuatilie hili kwa umakini hasa katika vyuo inavyovimiliki hali hii imekithili sana.

Kuna Wanafunzi walifelishwa makusudi katika mitihani ya practiclal ilikuwa ni Mwaka 2023 Semester ya pili, Mwalimu mmoja wa kiume akiwa kama external examiner alipewa jukumu la kusimamia mitihani ya vitendo, siku hiyo aliyokuwa akisimamia ilikuwa ni siku ambayo mchumba aliyepanga kumuoa alikuwa anafunga ndoa na Mwanaume mwingine.

Hali hiyo ilipelekea afelishe Wanafunzi wengi wa kike kwa makusudi bila kujali hatima yao, hata Examiner mwenzie hakuweza kumkabili kutokana na hasira aliyokuwa nayo.

Wizara ya Elimu na Wizara ya Afya ziweke mazingira wezeshi hasa wakati wa mitihani ili vitendo hivi vya kikatili Psychologically visiendelee kuwepo kwa Wanafunzi.
 
Someni sana Janja.
Shida inaanza vijana wanachukulia poa masomo ya Afya.
Haiwezekani Afya imekua ya D—4.
Kuhusu walimu kufelisha pambaneni nao.
 
Aisee! Hiyo ishu ya mwalimu kusimamia practical, halafu wakati huo huo mchumba wake alikuwa anafunga ndoa na mhuni! Haijakaa poa hata kidogo.

Kwa hiyo hasira zake zote aliamua kuzihamishia kwa wanachuo wa kike siyo!!
 
mAmbo yamekuwa tofauti,wakat zaman hv vyuo vilikuwa vinapitisha watu tu mitihan ilikuwa inavujishwa na walimu walikuwa fair
 
Kweli kabisa hawataki madogo wafike walipo wao utafikili watapunguziwa mishahara yao,Yani unakuta inshu ndogo tu mtu kasharudishwa mwaka ,halafu hata wao wenyewe utendaji kazi wao ni wa kawaida hawana uwezo hata wa kupata nafasi Katika nchi zilizoendelea,tatizo roho mbaya,tamaa,chuki za ovyoovyo ,kisasi ni vitu ambavyo vinachangia Hawa jamaa kuwa wakatili ,ilihali wanajua mtu bado yupo kwenye mafunzo na si mwajiriwa,na hata akiajiliwa bado atahitaji kujifunza zaidi,Kwa walimu wote waliofelisha wanafunzi Kwa makusudi au Kwa kosa dogo wote ni maskini mbwa.
 
Back
Top Bottom