Wa mwisho ndiyo mshindi

Kuwaangazia popote pale walipo lala mbele za haki

Hakika mimi natembea ni marehemu
Natembea ni marehemu, ama kwa hakika.

Kwanini basi nijikweze? kwanini nimuonee mtu? kwanini nivimbe mbele za watu wengine?

Yafaa nini mimi kuwa chanzo cha maumivu, mateso na huzuni kwa mwanadamu mwenzangu?

Mungu atupe kukumbuka KILA SIKU kwamba;-

Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke, siku zake za kuishi si nyingi,

Naye hujaa taabu, yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa,

Hukimbia kama kivuli,wala hakai kamwe.


Tukiisha kuyajua haya na kuyazingatia, Dunia itakua sehemu nzuri sana kuishi.
 
Kuishi kwingi kuona mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…