Wa Tz Tutakufa Maskini Kwa Kimbilia Kuchimbia Pesa (Kujenga) Badala ya Kuizungusha Izae Zaidi

lara 1

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2012
Posts
15,700
Reaction score
29,164
IGWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Watanzania wengi haswaaa vijana wa sasa na vijana wa zamani wengi watakufa maskini ama kuzeeka maskini kwa kuendekeza Ucommunist na sera za kizamani za utajiri ni kumiliki nyumba na gari.

Sikatai nyumba ni a very valuable asset, na ina appreciate in value with time lakini this is not necessarily the case always. Appreciation na returns za hio nyumba zinaweza zisiwe reasonable enough kujustfy wewe kufkia 40Mills au 30Mills leo hii. Hio initial investment inaweza kuchukua hata 20yrs kujirudisha tu bila kujilipa. Imagine hio 40Mills ungewekeza kwenye opportunity zingine zenye large returns, na kuhakikisha unachukua calculated risk in 20yrs si unweza kujikuta una 400Mills na mijumba ya kumwaga!

Sio kwamba wa tz wengi hatushiki mbesa, no! tunashika sanaaa sema priority ndo zinatuangusha haswaa waajiriwa wa white collar jobs. Ile breakthrough ya msomi kutoka maisha ya kawaida na kuwa mwekezaji anae ajiri watu asilimia kubwa hawaifikiii. Mtu akishika tupesa tudogo anakimbilia kutuzika mashambani huko!

Vijana wenzangu unashika tu 10mills unawahi kutuzika Mbagara kiburugwa sijui huko au Mbezi maramba mangapi sijui. Unaongezea kuzika mamilioni hadi yafike hata 50 in 4 yrs hadi umalize jumba hilo. Kisha kodi unapoke 100,000/= in 10 to 20 years haiendi mbali na hapo. Watu waliojenga Tabata in 1990's nyumba mpaka leo Tbt ni 200,000 kwa mwezi?????

Tubadilike tuwe capitalistic. Ukishika 10m ujipange izungushe ushike 50m. It all about opportunity and risk taking this is the only key kuwa billionea. Ruge keshasema fursa ziko nyingi mnoooo! Tabia ya kuzika tuiache. Nyumba ziko kibao Sinza, Masaki, Obay, Knyma kwanini uende porini? Hio 10Mills izungushe hadi ifike 300Mills ununue nyumba ya uhakika Kinondoni. This is the bigger picture!

Thanks you all!
 
HICHO ULICHOONGE AHAPO RED KIMENISIKITISHA SANA ,HIVI UNAJUA WATU WOTE WANGEKEWANA MENTALITY HIZO HAPA DSM KUSINGEKUWA NA TEGETA,BUNJU,HATA HIYO KINONDONI,??UKUAJI WA MJI NI WATU WENYEWE KUJIRUNDIKA SIO ISSUE SANA.

Nafikiri hujui aspects za maisha kila mtu ana mtazamo wake ,mtu aliyejenga nyumba 2008 ,huwezi mfananisha na 2012 japo ni ile ile na ramani ile ile .hali ya maisha inakuwa ngumu kadri siku zinavyoongezeka mtu huna bishara utaizungushaje hiyo hela alafu usione watu wanjenga nakununua viwanja ukadhani wanazika hela noooooooooooo ,wanavinunua nakusubiri viapriciate!!nayo ni biashara yenye faida japo inachukua muda.na ujue kwamba sio wote wenye knowlwdge ya biashara au kuzungusha pesa!!
 
Saivi nimekubaliana na shinikizo la Raisi la kutaka wananchi tujiletee maendeleo wenyewe lasivo tukimngojea yeye na serikali yake tutangoja hadi kurudi kwa Mwana wa Adamu. Kwa kuanzia nimejiunga rasmi na MKURABITA!!!!!!!!

hongera kwa kutambua hilo mumiiiii!!!!, never too late to do a right thing!!!!
 

Hahahaaaaaaaaaaaaa! Exatly the mentality NAYOIPIGA VITA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Watu wenye surplus capital ndo wajenge coz wako na pesa mingi sanaaa hadi watafute kwa kuinvest! Ila Mtu una ka 20Mills unakachimbia chini. Then unaanza upyaaa kusave na kudunduliza. Ukifikisha 5M unakachimbia tenaaaa. SAD!

Hili limesababisha watu wengi wastaafu na 2 houses, 2 cars basically tunasema kastaafu Masikini!!!!!!!!!!! Ila laiti ile 20m angeiwekeza vizuri story ingekuwa ingine kabisaaaa. Mtu anaishi tegeta leo nyumba kaijenga 1990's kodi kwa nyumba standard nzuri ni 300,000/= sasa anafaidi nini wakati hilo banda ndo lifetime savings zake. Hata hakuwahi kwenda Dubai for holiday, coz hakuwa na uwezo!

Mawazo mgando yanakimaliza kizazi hiki Tz. Mji upanuliwe na waliojipanga sio kukurupuka. Nyumba moja unaijenga 10yrs afu mashambani huko!

Tuwe kama ulaya wenzetu walijua mapema sio ishu hii!
 
ITS TRUE LARA1 SIONI MANTIKI MTU ANAPATA 10m anakimbilia kuzizika kwa kujenga badala ya kuzizungusha nitakupa mfanoaangu binafsi nilikuwa na 7m mwaka 2010 nikafungua biashara ya genge la kuuza fresh products na nafaka mchele, maharage ndani ya mwaka 1 nikawa nina 5m faida. nikafungua saloon ya kiume. sasa nimewaajiri vijana 4 pale wananiletea 15,000 kwa siku so 15,000 x4 = 60,000 ukitoa matumizi kidogo hapo saloon nabaki na hela ya maana, nimefikiria kuanzisha saloon ya kike japo si mtaaalamu sana mambo ya saloon ya kike (madawa, mitindo) nataka niongee na sista wangu ndie awe msimamizi sasa nina plan ya kutafuta gari/pick up kuu kuu ili niwe nabebea mizigo yangu ya sokoni. Fikria ile 10m ningejidai kwenda kununua kiwanja kisha nianze ujenzi ningefika popote? kijana usijenge kwa kufuata mkumbo utaumbuka.
 

EXACTLY!!!!!!!!!!!!! Ungekimbilia kuizika ungekuwa mmiliki wa maana wa gofu la mjengo wa L kibaha kwa matiasi! (Perdon my sarcasm) Sasa tuseme leo ukiamua kujenga paaaah! Si utajenga nyumba ya maana zaidi na neighbour hood nzuri zaidi kuliko ungekurupuka kufukia pesa kipindi kile!

People its time to change!
 
nafikiri usiwkatishe watu tamaa wacha waende taratibu hivyo hivyo au unataka waibe ,huwezi kopa benk kiasi kikubwa ch ahela kuinvest kama huna dhamana kubwa ,nashindwa elewa unataka watu wafanyaje ,ni uelewa mdogo kuifananisha tz na ulaya !!taratiibu tu tutafika
 
Usimamizi wa biashara unahitaji muda na mpangilio, pesa zapatikana kwa shida sana, punde mtu apatapo kiasi fulani, hufikira njia salama zaidi ya kuhifadhi au kuizungusha ili kupata zaidi.
Sasa swali rahisi ni kuwa ni ipi njia rahisi ya kuizungusha 10M into 300M ambayo itakufanya uendelee na kazi uliyonayo huku ukitegemea returns kubwa ya 290M, hapo unaona hakuna, Ni bora kununua kiwanja kwa uwezo huo.

Sasa wakati mtu akiendelea na shughuli ile ile ambayo humnyima muda wa kusimamia kazi zake binafsi huamua kujenga moja kwa moja.

Kumbuka hizi 10M unazozizungumza nyingi zinapatikana kwa mikopo na mshahara unakuwa ni dhamana.
Hivyo basi swala si kukumbilia kujenga bali ni usalama wa investient ukichagiwa na muda wa kusimamia shughuli za kuwekeza.
kumbuka unjenzi hauitaji kukaa kuanzia asubuhi mpaka jioni, hauitaji kusafiri, hauitaji networking.

Kuzungusha 20M into millions of Tshs kama hauna muda utaingia chaka, usimamizi wa mtaji ni muhimu sana, embu fikiria mfanyakazi wa benki unaingia saa 2 unatoka saa 11, jumatatu mpaka j1, unawezaje?.

Ikiwa utajitoa mhanga unaachana na kazi then unaamua kabisa kudeal na mambo yako binafsi hapo unakuwa na walau uhakika. Kingine TZ hii bishara nyingi ni kichaa tuu, unaweza kupeta miaka 5 to 10 years, then suddenly things turn upside down. Tunaona watu wakifilisika wanakuwa kama hawakuwahi kushika pesa, wanauza kila kitu.

Hapa namaanisha kuwa kinacho badili 10M into 300M leo may not be the same in the next 5 years.

nadhani umenipata shosti
 

Aaaaaaaaaaah! Wanione bure! Neno langu sio sheria! Im just talkin of the bigger picture! Mtu akimua kubakia on the smaller picture ni choice yake! After all pesa ni yake! Mtu hakunyimi neno bwana! Mi hili neno nimelimwaga hapa litakaemfaa haya! Litakae mkwaza aniwie radhi!

Watu pesa wanashika daily kwa namna moja au nyingine. Nimewaremind tu if and only if wakizifumania huto tumilioni kadhaaa, they should make the correct choice!
 

Swala la Investment salama that is a topic for another day, nitakuja humu humu na True Life stories za wabongo walivotoka kimaisha! But mind you RISK is always constant! Na returns unayopata ni reward yako ya ku overcome risks.

THE HIGHER THE RISK THE HIGHER THE HIGHER THE RETURNS!!!!!!!!!!!! Hii haikwepeki! Ukiogopa risk then you made a choice to remain poor! It doesnt matter its your life anyways. Ingekuwa rahisi kila mtu angekuwa tajiri! Huu ndo mtihani wenyewe!.

Na jambo lingine SUCESS IS ALL ABOUT GRABBING OPPORTUNITIES BY THE BALLS AT THE RIGHT TIME. Mfano dada mmoja alikuwa na 8m za urithi kipindi Twiga wametoa IPO yao ya shares za twiga. Akajitosa mzima mzima akatumbukiza whooping 8m! Paaah! Yote akanunua hisa kipande 200. Only ten years after kipande alichonunua 200 kinauzwa 2000 na kinakaribia 3000. Je leo akiamua kuuza shares zake atakamatika? ITS ALL ABOUT SPOTTING THE OPPORTUNITIES N GRABBING THEM BY THE BALLS!

10M kwa mishahara ya kampuni binafsi za Dsm ni saving ya mwaka tu na pungufu, kwa watu bachelor wasiolipa ada ama kutegemewa na wazazi.
 
kweli mkuu,tatizo mazingira ya biashara tanzania sio rafiki kabisa!na zinataka wewe mwenyewe uwe msimamizi kila process vinginevyo wafanyakazi wezi
 
una maana wakati huo hao waliospend (let say) 40m by then kujenga nyumba Tabata wakiamua kuziuza hizo nyumba leo zitakuwa bei gani?
Na unavyoongelea ktengeneza pesa then upate 200m uje kununua nyumba Kinondoni hizo unazonunua hazina watu bali wana kaa panya? Na kama wanakaa watu ina maana watahamia wapi kama sio Tabata, Tegeta, Mbezi Maramba mangapi nk ili wakupishe wewe?
Unaonekana kuwa akili yako umeinarrow na kufikiria maeneo machache tena ya Dar es Salaam ambayo ndiyo yamepimwa na kwa kiasi fulani huduma za jamii zinapatikana lakini ukasahau kuwa Tanzania ni kubwa. Na unacho focus ni kuwa pesa zinapatikana Dar es Salaam tu ambapo wengi wenye mawazo hayo ni ya kifisadi zaidi maana dsm ni ujanja mwingi badala ya kazi. Ni kwa nini usiseme kuwa upate 200m ukaanzishe kilimo cha maharage kasulu ambayo sasa kilo moja inafikia 1800/-?
Any kind of entrepreneurship depends much on the culture of that involving area. Sasa maisha ya Dar es Salaam au hata Tanzania nyumba ni kitu ambacho ni very significant tofauti na Ulaya au US ambapo mtu anaweza kupata kazi mji mwingine akauza nyumba ya mji anaoishi na akaenda kununua nyingine huko anakoenda. Tanzania ukishauza kama nyumba ndio imetoka tena na mara nyingi huwezi kuinunua tena. Ndio maana nikamsikia yule kijana diamond akisema "hakuna baba mwenye gari bali kuna baba mwenye nyumba"!
Conclusion ya haya yote ni kuwa wataalamu wanasema Tanzania ni vigumu sana kufanya biashara ya aina yoyote kwa sababu ya rushwa na uchumi uliojaa rushwa it is not easy to predict what tomorrow will bring basing on a fact that many business here do not have perfect information kwa hiyo ni kutegeshea tu. Unachosema ni sawa na kuangalia mbele tena sana lakini bila kujua kuwa inabidi uwe na sehemu uliyosimama ili uweze kuona huko mbele.


 
Mkuu:nimekupata wazo laki nimelikubali.Mimi nimetumia muda mwingi kujenga Nyumba yangu yenye thamani ya sh.50m na nina kiwanja cha sh.20m na nina shamba la heka 10 la thamani ya sh 5m, mpaka sasa sina chochote zaaidi ya hizo aseti tu!!
Mkuu naomba msaada wako nifanyeje ili nianze upya ili niweze nifikie huko? Msaada tafadhali na kama kuna mengi ya kunijuza niandikie alicesali@ymail.com thanx
 

Mimi ni mwana Darisalama mzaliwa wa Kinondoni ndo maana hoja yangu imebase Dsm. All im sayin is WATU WAJENGE BAADA YA KUJIJENGA KIUCHUMI! Pesa ndogo wanayoipata kwanza waitumie kujijenga kiuchumi then wakisimama kiuchumi ndo wafukie mahelaaaa!

Lasivo it doesnt make sense mtu alieweza kujenga jumba la 60mills in eraly 2000's leo hii awe anaishi kwa kudunduliza kadi! That is a bad investment strategy.

WATU WADHUBUTU SIO KUENDEKEZA WOGA WA KUTAKE RISK!
 

Hapa ndo nimeanzisha MKURABITA humu JF,we fatilia tu series za post zangu jukwaa hili, nitakuletea Mambo Mazito ya Watz walioanzia 0, step by step na kufikia u billionea. Logical facts! Hakuna ndumba wala magendo. Stay tuned. Lazima tutokomeze umasikini! Tunaanza kutokomeza wa Fikra kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…