Kumbuka haya mabasi yanapita kwenye barabara zilizokuepo, tofauti ni kwamba ndani ya barabara hizo kuna lane za BRT, hakujajengwa barabara tofauti za BRT, pia sehemu iliyojaa maji ni jangwani na hakuna daraja wala barabara iliyozolewa na maji, ila maji yalijaa karibu Dar yote ilikumbwa na mafuriko yaliyodumu kama saa mbili hivi, pale jangwani ni mto unaoingia baharini kwa hiyo maji yalijaa sana, na hili tatizo ni la miaka yote hata kabla ya Tanzania kupata uhuru, ufubuzi wa Jangwani ni kujenga barabara ya juu toka Magomeni hadi fire, ambayo ni ghali sana kwa sasa sio rahisi kwa nchi kugharimia huo mradi, ila baada ya massa mawili, maji yalikwisha na hakuna daraja wala barabara iliyozolewa, hiyo inaonyesha uimara wa ujenzi wa sehemu ile.