Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,256
- 44,597
Na. M. M. Mwanakijiji
Inashangaza na inakera kwa wakati mmoja. Mojawapo ya mambo yanayoshangaza sana ni kwa jinsi gani wapinzani uchwara wa CHAUMA wanajitahidi sana kufuatilia mambo yanayoendelea CHADEMA na kutaka CHADEMA ifanye usafi na hasa wakijitahidi kutaka Jabari John Heche aondolewe ili waingie watu watakaokubali maridhiano ya kupigishwa magoti na watawala walioshindwa.
Toka John Heche aweke msimamo wa chama chake kuwa hakitaingia kwenye maridhiano wakati mwenyekiti wake akiwa ndani, na kukiwa hakuna dalili yoyote ya serikali kuwajibika kwa matukio ya Oktoba 29. Heche sasa amekuwa si tu mwiba bali pia kizuizi cha kile ambacho watawala wetu walidhania kingekuwa rahisi hasa baada ya kumbambikia Tundu Lissu kesi ya uhaini na kumuweka nguvuni kwa zaidi ya mwaka sasa. Misimamo hii ya Heche na hasa moto aliouawasha mikoani kumewafanya watawala kujiuliza kama yawezekana kuwa wat wenye misimamo ya mabadiliko ya kweli ni wengi huko CHADEMA.
Sasa, upande mmoja tunaona baadhi ya viongozi wa matawi ya CHADEMA mikoani ambao wamerukia tela la "apishe, achunguzwe, aondolewe" wakiimba wimbo wa CCM. Lakini upande mwingine ni hawa wapinzani uchwara ambao leo wanazungumza kwa uchungu kwa mambo yanadhaniwa kutokea CHADEMA kuliko mambo yaliyotokea Tanzania na ushahidi ukiwepo.
Ati watu wana uchungu sana na 'hela' za CHADEMA lakini hukuwasikia wakitaka viongozi wa serikali wajiuzulu kwa ufujaji na upigaji mkubwa ambao umeendelea na ushahidi ukikusanywa kila mwaka na CAG. Yaani, makada uchwara wa upinzani uchwara wenye masihara wanaguswa zaidi na michango ya CHADEMA kuliko na kodi za wananchi wote. Na bahati nzuri CHADEMA wamegeuza ule wimbo wa CCM
"Tuna imani ni John Hecheeeee,
Oyaaa, Oyaaa, Oyaaa
Heche kweli... kweli... "
Wanashangaa. Zipotolewa tuhuma walitarajia kuwa Watanzania wataikimbia CHADEMA lakini Watanzania wamesimama nao na kuwachangia kwa 'tone tone'. Hili linawashangaza. Inakuwaje wanaungwa mkono watu hawa; hawa Watanzania wenye imani hivi wanawezaje kuunga mkono chama ambacho hakina mbunge hata mmoja? Kwanini watu wana imani na upinzani wa CHADEMA? Ukweli ni kuwa Heche amejikuta akiwakilisha matamanio ya mabadiliko ya kweli nchini, akibeba kijiti cha uongozi wa upinzani nchini sasa hivi.
Ni kweli tunasikia kuna njama na jitihada za kumtisha (intimidate) na hata kumfanya afikirie mara mbili. Tukio la dereva wake kufariki katika mazingira ya kutatanisha ulikuwa ni ujumbe kuwa wanaweza kumkaribia sana. Sasa hivi wapinzani uchwara wana amani, wanakumbatiana na CCM na kwa uhakika hakuna atakayetiwa pingu, kuishia gerezani kwa ajili ya kuwatetea Watanzania. Watanzania wanaounga mkono upinzani wa aina hii hawana namna isipokuwa waamue tu kuvaa tisheti za kijani na njano!!
Upinzani usiojitofautisha na CCM, wenye misimamo ya kiCCM, si upinzani wa kupotezea muda wanaotaka mabadiliko ya kweli. Mvuto wake ni kama show ya wasanii wetu na kuleta burudani tu na si ushindani wa kweli. Ushauri wangu wa bure ni kuwa CHADEMA waendelee kujipanga kupambana na CCM na kuachana na hawa wapinzani uchwara.
Lakini kubwa zaidi ni kuanza kufikiria kujipanga kuwang'oa watawala wetu walioshindwa kwa namna yoyote inayowezekana mapema iwezekanavyo.
Tuwaache CHAUMA kiwe CHAUMWA!