National Anthem
JF-Expert Member
- Aug 9, 2022
- 19,177
- 56,121
Kuna mwamba mmoja kitaa, anasema mungu aliumbwa na wazungu.. hao wazungu walipo muumba ( wote walikuwa miungu ) ila wakaamua mchagua mungu mmoja kuwa mungu wa wote..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Upo sawa Mkuu, Hapo ndipo tukae chini tutafakari.Mimi kila siku nawaambia watu ,Waafrika hatuna dini. Kila race ina dini yake na imani yake, kasoro waafrika tu. Wazungu dini yao ni kristo, waarabu ni islam, wahindi ni hindu, wachina ni budha, Sisi waafrika imani yetu ni ipi? Waafrika tumepotoka sana.
Kipindi babu zetu wako utumwani huko Ulaya na Amerika, wale mabwana zao(Masters) wazungu walikuwa wanatumia vitabu kuwa dhoofisha na kuwa pumbaza watumwa hao. mfano.Mungu ni Mmoja tu kwa wote,
Hata hizi bibilia huenda ziliandikwa kuua tamaduni zetu tufate zao iwe rahisi kututawala
Kama unamjuaa - mtajeKama unamjua mtaje.
Ukweli mbona tunaufahamu mkuu..tunajizima data tu...Muafrika anaabudu Mungu kutoka arabuni na Middle East, hivi Mungu ana upendeleo kiasi hiko ashukie arabuni na Middle East pekee?
Wazee wetu walipokuwa wakitoa kafara ya wanyama wageni wakawaambia huo ni uchawi na ni dhambi, lakini kwenye biblia agano la kale kafara zilikuwa zinatolewa na wanasema wana muabudu Mungu.
Mungu wa Africa naamini yupo, ni vile mmesahaulishwa na wageni.
Hivi Maasai na Sandawe katika mila zao na desturi na hawafahamu kama kuna Bible na Quran wanapata dhambi kutoka kwa Mungu wa arabuni na Middle East kufuata mila zao na desturi ambazo zinakinzana na kukatazwa na dini za kuletwa? Mungu anae walaani anatumia vigezo vipi? Ana huruma huyo Mungu?
Umezaliwa porini, ukakulia porini, wazazi wako wamekuambia mila zetu ni kuoa wake 12, anakuja mzungu anakuambia ni dhambi oa mmoja na muarabu anakuambia wanne mwisho, wewe kosa lako hapo lipo wapi? hufahamu kama kuna bible wala quran, hio dhambi unaipata kwa vigezo vipi?
Africa tunaonekana gorilla tu mbele ya watu weupe, licha ya kujifanya mnakufa kwa ajili ya kutetea dini zisizokuwa na nyuma wala mbele, wengine wakijitoa mhanga kabisa, wengine wanakuambia nchi fulani ni wateule wa Mungu. Pumbavu kabisa.
Congo mauaji ya kila siku ni zaidi ya yanayoendelea Middle East, lakini kwa sababu Africa ni kama wanyama pori unaonekana huna thamani, hakuna double standards kwenye media,.
King Leopold II of Belgium aliua Congolese zaidi ya milioni 15, lakini story ya Hitler kuua jews 6 million ni habari kuliko Africans waliouawa kinyama na mzungu.
Tumedanganywa.
Sahihi mkuu, tamaduni zetu tunaitwa uchawi, lakini Africa tungekaa na kufuata tamaduni zetu, kuna nguvu isiyo ya kawaida.Hizi dini zimepotosha sana wazee wetu na hawa mabraza walioenda shule kidogo nakupata vipesa.
Wakirudi vijijini wanavunja mila na desturi na wanasikilizwa na wanafamilia kwasababu ya pesa alizonazo.
Ila bomu analotengeneza ni kubwa sana, ndo ile unashangaa familia fulani kama ina laana umaskini umetawala, vijana wamekuwa walevi hawana nyuma wala mbele.
Kumbe tatizo ni ile kuvunjwa kwa mila na matambiko ya koo imeleta shida, maagano yaliyofanywa baina ya wana familia na wazee waliotangulia yanawatesa vijana kizazi mpaka kizazi.
Tunaambiwa tunaabudu mizimu, wakati katika sala za katoliki unasema mt. Aloyce utuombee ambae ni marehemu je huyu si mzimu? Je anakujua?
Hizi dini tumepigwa sana, leo hii mchungaji ana maisha mazuri ya anasa yote ni kutokana na sadaka za waumini, mchungaji anakuambia toa sadaka ya kujiteketeza, misa ikiisha muumini anatembea kwa mguu kilometa za kutosha wakati mchungaji anawasha V8 yake.