Waafria tuamkeni kifikra

Kuna mwamba mmoja kitaa, anasema mungu aliumbwa na wazungu.. hao wazungu walipo muumba ( wote walikuwa miungu ) ila wakaamua mchagua mungu mmoja kuwa mungu wa wote..
 
Upo sawa Mkuu, Hapo ndipo tukae chini tutafakari.
 
Hizi dini zimepotosha sana wazee wetu na hawa mabraza walioenda shule kidogo nakupata vipesa.

Wakirudi vijijini wanavunja mila na desturi na wanasikilizwa na wanafamilia kwasababu ya pesa alizonazo.

Ila bomu analotengeneza ni kubwa sana, ndo ile unashangaa familia fulani kama ina laana umaskini umetawala, vijana wamekuwa walevi hawana nyuma wala mbele.

Kumbe tatizo ni ile kuvunjwa kwa mila na matambiko ya koo imeleta shida, maagano yaliyofanywa baina ya wana familia na wazee waliotangulia yanawatesa vijana kizazi mpaka kizazi.

Tunaambiwa tunaabudu mizimu, wakati katika sala za katoliki unasema mt. Aloyce utuombee ambae ni marehemu je huyu si mzimu? Je anakujua?

Hizi dini tumepigwa sana, leo hii mchungaji ana maisha mazuri ya anasa yote ni kutokana na sadaka za waumini, mchungaji anakuambia toa sadaka ya kujiteketeza, misa ikiisha muumini anatembea kwa mguu kilometa za kutosha wakati mchungaji anawasha V8 yake.
 
Mungu ni Mmoja tu kwa wote,

Hata hizi bibilia huenda ziliandikwa kuua tamaduni zetu tufate zao iwe rahisi kututawala
Kipindi babu zetu wako utumwani huko Ulaya na Amerika, wale mabwana zao(Masters) wazungu walikuwa wanatumia vitabu kuwa dhoofisha na kuwa pumbaza watumwa hao. mfano.

Waefeso 6:5 - 8 inasema '"5 Watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani, kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnamtii Kristo. 6 Watiini, sio tu wakati wakiwaona ili mpate sifa, bali mtumike kama watumishi wa Kristo, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo. 7 Toeni huduma yenu kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na sio watu. 8 Mkumbuke kuwa Bwana atampa kila mmoja tuzo kutegemeana na wema aliotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru."
 
Ukweli mbona tunaufahamu mkuu..tunajizima data tu...
 
Sahihi mkuu, tamaduni zetu tunaitwa uchawi, lakini Africa tungekaa na kufuata tamaduni zetu, kuna nguvu isiyo ya kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…