Nisaidiwe hapa. Huo ubaguzi wanaobaguliwa ni upi? Kuitwa manyani tu au kuna lingine. Sisi mablack ndio tunalialia. Tungewapuuza hizi kelele zisingekuwepo. Kwenye dimba tukiupiga mwingi kama pele, na Neymar, unadhani hata wakikuita nyani kuna shida. Maana nyavu zinawajua vizuri hawa miamba.
Kuhusu kutokuangalai soka la ulaya ni ngumu sana. Tangu uje ulimwengu wa setilite TVs, hii haiepukiki tena. Tuacheni sisi wanazi wa reds tuendelee kuona zile tackle anazopiga Fabinho Tabarezi, zile dribbling anazofanya Bobby akiwa fit. Yale magoli anayofunga king Salah na yale mashuti anayotandika Mane.
Zile nguvu anazotumia VvD na yale mashuti anayopangua Allison.
Siwezi kukaa nikaangalia mpira eti ihefu anacheza na mwadui😆😆 au mbao anacheza na biashara mara😁😁