Waafrika hatuwezi barikiwa mpaka tutakapo acha unafiki na ubinafsi.

Waafrika hatuwezi barikiwa mpaka tutakapo acha unafiki na ubinafsi.

kulagha nenga

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2026
Posts
690
Reaction score
1,375
Habari wadau Leo ngoja nitoe povu kidogo,
Mwafrika au mtu mweusi ni mnafiki, mbinafsi nani katili sana.

Wakati wa utumwa ni viongozi wakiafrika walishirikiana na wageni yaani wazungu na waarabu kuwakamata na kuwauza wenzao utumwani

Leo viongozi hao hao wana shirikiana na wageni kuwakandamiza na kuwaaibia waafrika wenzao kupitia mikataba mibovu na teni pasenti

Viongozi wa dini kupitia hizo dini zao wanawakandamiza waafrika wenzao na kuwaaibia kupitia michango na sadaka, wao wananeemeka waumini wao wanazidi kuwa masikini
Watoto wengi wameharibiwa Kwa ukatili wakingono kwakile kinachitwa dini, madrasa, Sunday school na seminary

Tulivyo wapumbavu eti Kuna watu wanashindana na kubishana mambo ya kidini Tena dini za kuletewa yaani jitu jeusi tii linagombana najitu jeusi jenzio na kuitana majina ya kijinga kabisa sijui kafiri sijui gaidi, haya ninyi mnaobishana nitajieni mtume mweusi alishushiwa hayo maandiko katika hizo dini mnazo bishania.
Yaani Bado hatujitambui kama binadamu. Mwizi akiwa muislamu mkristo mwiko kumkemea, mwizi akiwa mkristo muislamu mwiko kumkemea.ndo ichi ilipofikia Kwa sasa ni mwendo wakusapotiana TU hata Kwa maovu. Tena viongozi wetu wanaapa kwakutumia misahafu huo sio unafiki kweli

WAAFRIKA HATUWEZI BARIKIWA MPAKA TUTAKAPO ACHA UNAFIKI NA UBINAFSI, we endelea kudanganywa sijui ombea Taifa teule wachina na wajapani wamebarikiwa walimwombea nani?
 
Back
Top Bottom