Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
Ulaya ilikuwa inanuka. Tena inanuka sana.
Wazungu walikuwa wachafu, sema haya mambo hutokuja kuyasikia wakiyaandika kwenye vitabu vyao.
Unawajua watu walioitwa Moors? Hawa walikuwa watu weusi waliokwenda huko Ulaya.
Kuna ile nyakati Wazungu waliita Dark Ages, haikumaanisha kwamba jua halikuwa likiwaka, hell no bali walimaanisha kwamba Ulaya ilikuwa gizani.
Yaani walikuwa na ukungu kwenye kila kitu.
Mentally na Physically. So baada ya wao kuwa kwenye giza kubwa, ndipo hao Moors kutoka Afrika Kaskazini wakaingia huko.
Hao washikaji walikuwa watu wenye elimu kubwa. Kitu cha kwanza walichokipelekea Ulaya kilikuwa ni elimu kubwa kupitia vitabu mbalimbali.
Walikwenda na maktaba za vitabu kibao. Hawa majamaa ndiyo watu waliopeleka elimu ya kutengeneza sabuni, mifereji ya maji machafu, hospitali, taa za barabarani na vitu vingine.
Wao ndiyo waliwafundisha watu wa Ulaya jinsi ya kuoga.
Hawakuwa wakioga kwa kuwa waliamini kuoga ni dhambi kwa Mungu, hivyo walikuwa wakiishi hivyohivyo.
Wakatengeneza mabafu 600 ya mitaani, yaani walitaka Wazungu wote wawe wanaoga kwa sabuni.
Wakapeleka elimu yote unayoijua wewe, mashule, vyuo.
Walifundisha masuala ya hisabati, sayansi, unajimu, utabibu na mengineyo.
Mji wa Cordoba hapo Hispania ulikuwa na maendeleo makubwa kwa sababu ya watu hawa.
Wakati huo wa zama za giza nchi nyingine za Ulaya bado zilikuwa zinaendelea kuwachoma moto wachawi kila siku.
Baada ya miaka 700, Wazungu wakaamua kukiondoa kizazi cha Moors barani mwao.
Wakafuta historia ya Moors.
Wakafuta kila kitu na kuwaondoa kwenye vitabu vyote vya historia na kuweka vitabu vyao.
Na ndiyo maana leo huwezi kukuta vitabu vikiwa na historia ya hawa majamaa walioibadilisha Ulaya na kuwa hivi ilivyo sasa.
So ukisikia Dark Ages...inamaanisha zaidi ugiza uliokuwa vichwani mwa Wazungu miaka hiyo. Wakafuta historia za watu weusi, wakatupa historia zao na tunazisoma mashuleni.
Tafuta historia ya European Dark Ages, yani Kipindi Cha Giza Cha Ulaya... utaelewa nachomaanisha
Tunasoma wanachokitaka wao, na si tunachokitaka sisi.
Vilevile unaweza kugoogle Moors kuwasoma zaidi.