Hapana, hapana. Afrika hatuna adui yoyote na wala sio masikini.
Tatizo linaanza na wewe kudhani kwamba ni masikini "ukilonganisha" na hao wazungu. Je unajua kwanini unadhani hivyo? Sababu wazungu ndio wamekuaminisha hivyo bila ya wewe kujua, na wala wai kujua kutonana na tabia zao za kujiona wako juu.
Uhalisia ni kwamba, Waafrika tumekuwa tukiishi maisha ya kawaida kwa maelfu ya miaka bila ya kuhitaji vikubwa, hapo ni kabla ya washenzi kuvamia. Ni utamaduni wetu na aina yetu ya kuishi. Sio umasikini. Huku wengine waliishi maisha ya aina nyingine kabisa kwa mahitaji tofauti. Wapo waliohitaji kutawala wengine kwa nguvu, kumiliki vingi zaidi ya wengine, kutatua changamoto za kimazingira, etc.
Na mpaka leo hakuna kilichobadilika. Tatizo ni kuacha mitazamo ya watu wasiokujua kukwambia wewe ni nani na ukakubali. Afrika sio masikini, bali imejikuta kwenye ulimwengu wa aina nyingi za maisha ya watu washenzi wanaoamini uhalisia wa kweli ni wa kwao tu. Na kwakua historia ya utumwa imeshusha self esteem ya Afrika, wengi huamini huo ni ukweli.
Cha msingi ni kutambua kwamba kila kizazi kinakuja na mabadiliko yake na mitazamo yake. Kizazi cha 50-90 kina mitazamo yake na kizazi cha 2000 kilichokulia kwenye ulimwengu huu wa leo nacho kina mitazamo na kinakuja na mabadiliko yake ya kileo. Mabadiliko yenye exposure ya dunia, uchungu wa kuchukuliwa mali na ku-adapt aina mpya ya maisha na kuona dunia kwa uhalisia wake. Hivyo mabadiliko ni lazima.
Nakutanaga na wazungu wapuuzi wanaosema Africa ipo nyuma kimaendeleo na kuwauliza maswali magumu ambayo hawawezi kujibu. Naiita hii technique yangu "vunja uono" au "perception deconstruction."
Simple kama hivyo.