Waafrika Tunadharauliwa kabisa.

Waafrika Tunadharauliwa kabisa.

>MWAFRIKA akienda ulaya = mkimbizi
>MZUNGU akija afrika = mtafiti

>KUNDI LA WAAFRIKA wakiwa ulaya = magaidi
>KUNDI LA WAZUNGU wakiwa afrika = wat0a misaada

>KUNDI LA WAAFRIKA katika mbuga za wanyama = wajangili
>KUNDI LA WAZUNGU ktk mbuga za wanyama = watalii

kama wajua udharilishwaji mwingne 0ngezea
asante yangu ni hayo
Nadhani nategemea umeendaje huko Ulaya. Kama umeenda kwa kupitia kujiita au kuwa mkimbizi wa kweli utaitwa mkimbizi....lakini ukienda kwa ajili ya masomo hasa ya shahada za juu utaitwa mtafiti. Na si kila mzungu ni mbaguzi, wapo wengi tu wasio wabaguzi na wanasumbua vichwa vyao kuhakikisha wanatatatu changamoto za waafrika ikiwemo ujinga, njaa, maradhi n.k.
 
Nadhani nategemea umeendaje huko Ulaya. Kama umeenda kwa kupitia kujiita au kuwa mkimbizi wa kweli utaitwa mkimbizi....lakini ukienda kwa ajili ya masomo hasa ya shahada za juu utaitwa mtafiti. Na si kila mzungu ni mbaguzi, wapo wengi tu wasio wabaguzi na wanasumbua vichwa vyao kuhakikisha wanatatatu changamoto za waafrika ikiwemo ujinga, njaa, maradhi n.k.
umemalza au bado
 
>MWAFRIKA akienda ulaya = mkimbizi
>MZUNGU akija afrika = mtafiti

>KUNDI LA WAAFRIKA wakiwa ulaya = magaidi
>KUNDI LA WAZUNGU wakiwa afrika = wat0a misaada

>KUNDI LA WAAFRIKA katika mbuga za wanyama = wajangili
>KUNDI LA WAZUNGU ktk mbuga za wanyama = watalii

kama wajua udharilishwaji mwingne 0ngezea
asante yangu ni hayo
Tupige kazi na tuongeze bidii ktk ubunifu ndo heshima itakuja .hata mbuyu ulianza kama mchicha
 
1. KUNDI LA WAAFRIKA ULAYA- WAKIMBIZI
2. KUNDI LA WAZUNGU AFRIKA - WATALII
3. KUNDI LA WAAFRIKA MSITUNI- MAJANGILI
4. KUNDI LA WAZUNGU MSITUNI- WAWINDAJI
5. WEUSI WAKITEMBELEA ULAYA - WAGENI
6. WAZUNGU WAKITEMBELEA AFRIKA- WATAALAM
MILANGO YETU YA UFAHAM SIJUI ILISOMBWA NA MAFURIKO.
 
Usife moyo timu ya mpira wa miguu ya Ufaransa wengi Wafrika na hâta waliwahi kuwa na waziri pia
 
Nakupa 10/10.
Kumzindua Mwafrika ni Ibada.
Ni ibada kubwa sana maana Unamtatetea Kiumbe kilichoumbwa na Mwenyezi Mungu. Viumbe vinavyodharaulika. Viumbe vinavyonyanyasika.

Hii ndio lugha zinazotakiwa kuzungumzwa katika mitandao ya jamii katika karne moja inayokuja.

Mwenyezi Mungu hakufanya makosa kumuumba Mwafrika. Na Mwafrika hakuja duniani kupata shida.

Historia inaonyesha "Civilization" imeanzia Afrika. Kusema Mwafrika hawezi ni makosa.
Wazungu ndio wametuigiza Utamaduni wetu. Elimu waliokuwa nayo historia imetokea Afrika. Hizi sio simulizi.

Angalieni Timbaktu, kulikuwa na elimu na maendeleo kabla hata Ulaya hajajulikana. Ndio maana Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Bwana Thabo Mbeki katika Utawala wake na harakati zake za kufufua hadhi na utu wa Mwafrika ali "adopt" rasmi Timbaktu na kuahidi kufufua historia yake.

Mifumo inayotawala imetengenezwa kumkadamiza Mwafrika. Fikra zetu zimepigwa mnada na tumewekwa kwenye giza na hawa hawa viongozi wetu wa sasa

Nini maana ya "Mapinduzi", kwanini Mwalim Nyerere alitumia neno hili? Ni neno zito sana. From "Oppression to Liberation", does this word or this theory "Revolution" applies anywhere in Tanzania?? Come back to us with a correct answer and stimulate this debate on a political matured lever and humble African traditional and respected manner.

Mwafrika hana damu ya manjano. Ni Binaadamu kama mtu mwingine.

Mwaka jana, Waafrika wakiwa kwenye mfuko wa bahari huko Afrika Kusini wakati wakisheherekea sikukuu yao ya Krismas. Mama mmoja wa Kizungu ambae yuko katika chama cha Upinzani Afrika Kusini, aliandika kupitia mtandao wake wa "Twiter" kuwa Waafrika waliojazana ufuko wa Bahari ni kama Manyani.
Wazazi wa Kiafrika na watoto wao wanatukanwa.

Atakomboleka tuu Mwafrika.
Thanks sana Mkuu ubinaadamukwanza .

You think beyond the normal thinking, That is how we supposed to be.Siyo kuwa MASHABIKI na kujiona INFERIOR mbele ya ngozi nyeupe.

Inabidi tusaili.Kusaili ni kuuliza mambo ya msingi juu ya chochote tukionancho, tukisomacho, tukisikiacho nk.Hivyo ndivyo walivyofanya kina Ngugi waThion'go,Chinua Achebe,Shaaban Rober,Mobutu Sese Seko wa Zabanga Zaire,Mwalimu JKN,Nkurumah nk.Hawakupenda kuumbatia uzungu na kuuacha Uafrika.Leo mtoto wa kiafrika hajivunii kuwa Mwafrika.Ni aibu sana.

Ni lazima akili isitulie,Lazima uwe RESTLESS.Hii ndiyo hatua ya mwanzo kabisa ya kuondokana na huu utumwa Mamboleo.Si kuiga kila kitu cha mtu mweupe na kuona vyetu si halali.

Kusaili ndiyo Mwanzo wa ukombozi mpya.

Mungu ibariki Afrika,Mungu ibariki Tanzania.
 
Uhakika nilionao, hila na chuki haziwezi kufanikiwa kwenye ukweli, badala yake zinaweza kuirudisha nyuma HADHI ya mtu mmojammoja na kuliangamiza taifa. Mi nafikiri tukianza kujithamini sisi kama sisi kwanza, ndipo heshima kutoka kwa wenzetu itakuja, lakini waafrika wa leo hasa sisi watanzania tumekuwa wanafiki, tunaombeana mabaya, hatutakiani mema, kikubwa pia hatupendani ni nani atakayetuthamini? Charity starts at home guys..period
 
>MWAFRIKA akienda ulaya = mkimbizi
>MZUNGU akija afrika = mtafiti

>KUNDI LA WAAFRIKA wakiwa ulaya = magaidi
>KUNDI LA WAZUNGU wakiwa afrika = wat0a misaada

>KUNDI LA WAAFRIKA katika mbuga za wanyama = wajangili
>KUNDI LA WAZUNGU ktk mbuga za wanyama = watalii

kama wajua udharilishwaji mwingne 0ngezea
asante yangu ni hayo


Swali langu kwako, anayetoa toa hayo majibu ni nani? Mzungu au Mwafrika? Yaani ni nani aneyesema hivyo? Na tunadharauliwa na nani? Na Mwafrika au Mzungu?
 
Kwanza niseme tu kuwa mimi naamini katika uwepo wa Mungu aliyeumba vitu vyote.

Mungu ndiye anayewapanga hawa viumbe vyake viwe kama vilivyo.
Mungu angewafanya Tembo wawe kama simba na chui basi wanyama wengine wangekua katika hatari kubwa ya kutoweka mara kwa muda mfupi au angemfanya nyangumi wawe wengi kama dagaa bahari ingekua ni eneo tishio kwa uhai wa viumbe wote.

Mungu ndiye aliyeamua Muafrika awe kama alivyo na kamwe mwafrika hatakuja tena kumtawala mzungu na haitakuaja kutolea.
Hata huyo anayeitwa mwafrika wa Misri alimtawala Myahudi tu na mwarabu lakini sio Mzungu kwa maana ya Mchina, Mrumi na Mgiriki ambaye alikua ameshapata maendeleo miaka mingi sana iliyopita.

Mwafrika ni mtu katili sana na mwenye roho mbaya kuliko kiumbe chochote kilichoko duniani. Kwa hiyo ni wazi kuwa Mungu kama muumbaji wa viumbe wote hawezi kamwe kumruhusu huyu mtu katili kutawala viumbe wengine.
Iliwafrika awe angalau kidogo na utu ni pale tu anapokuwa amekaa au kujifunza hali fulani za wenzetu weupe.

Wengi watauliza 1000 digits unatuambia kitu gani!!
Chukuwa mfano: Mwafrika akiachwa aingie kuishi kwenye msitu mkubwa wenye maji na kila aina ya matunda na wanyama. Baada ya miaka 10 utakuata amehama na kutafuta eneo lingine kwani atakua amefyeka na kuchoma miti yote na kuacha ardhi ikiwa jangwa.
Hana muda wa kuthamini wanyama wala vyanzo vya maji wala misitu iliyopo kwa ajili ya kuendeleza vizazi vijavyo.
Huyo ndio mwafrika wakati wenzetu waarabu wanabadili jangwa kuwa bustani yenye madhari nzuri na miti mwafrika anabadili msitu kuwa jangwa.

Mfano mwingine halisi ni pale unapoona vijana wa kiafrika wakiwa wamekaa kijiwene halafu mbwa au paka akakatiza mbele yao; atapondwa mawe balaa.Kiumbe wa watu amepita bila hata kubweka tena akiwa amefyata mkia wake lakini anaishia kuhukumiwa kwa kupigwa mawe bila kujali maumivu wanayompa kiumbe huyo. Wenzutu wamefikia mahali pa kufuga mpaka wanyama wa porini kwa gharama kubwa kuonyesha kuwa binadamu ni kiumbe pekee kinachoishi kwa akili.

Sisemi kuwa wazungu,waarabu ,wachina sio katili la hasha lakini mwafrika ni katili kwa mwafrika mwenzake bila sababu . Mwafrika ni katili kwa mazingira na viumbe wengine. Mpaka leo wakulima na wafugaji wanakatana mapanga. Karne hii ni nadra sana kumwona muingereza anamkata mwingereza mwenzake kwa panga au mkuki kwa sababu tu ya kutumia kilimo na ufugaji usio na tija. Vita na vurugu za mwafrika zinatokana na ujinga tofauti na mzungu ambapo vita na vurugu zinatokana na uelewa na kutaka maendeleo, uhuru na haki zaidi.

Mapaka leo wakati wenzetu wanakimbia kwa kasi mwafrika bado anafikiri kuwa anauwezo wa kupata maendeleo kwa kubaguana kwa itikadi za kisiasa. Yana mpaka leo wafrika wanapigania madaraka badala ya sera au mifumo.
Hata waarabu vita zao sio za madaraka bali ni za kudai mifumo fulani.
Watu wanaogombana kudai mifumo ni rahisi sana kuendelea lakini watu wanaogombania madaraka wanataka kushibisha matumbo yao tu wakishapata hawana cha kuwaza tena zaidi ya kugandamiza wenzao.
Mzungu alipomfundisha mwafrika na kuelimika na kujua maana ya uhuru miaka hiyo ya 1920 mpaka 1961 waasisi wetu ambao walipata elimu ya mzungu walikua wanaladha bado na fikra kama za mzungu na hadhi zao pia, ndio maana wao walikua hawapiganii madaraka; Wao walikua wanapigania UHURU. Leo mwafrika anapigania madaraka wakati hata uhuru wake bado upo mashakani.
Leo hii hatuwezi tena kuwa na watu kama akina Chinua Achebe, Ngugi wa thiong'o kwani ukitunga vitabu vya kukosoa watatokea watu watakunyamazisha na kukuita mchochezi na kutokana na maisha yalivyo ya ubinafsi wa mwafrika hakuna mtu atakayejali na utaonekana mchekeshaji na mtu anayejitakia matatizo.
Kwa hali hii kwa nini tusidharauliwe na mzungu?

Karne hii tuna wasomi wa kila namna lakini bado tunaaminishwa kuwa huyu mkoloni mpya anayeitwa mchina ndiye mkombozi wetu. Anatufundisha mpaka kuchoma mahindi na mihogo. Bado kidogo watahamia kule uchagani kwenda kuchoma ndafu. Utasikia ndafu ya kichina. Hapo kwa nini tusidharauliwe?


Waafrika tupo kama tulivyo kwa sababu ya roho mbaya.
Hebu tuangalie tu Mpaka leo hii watu wananakimbizana na wauza mkaa kwa gharama kubwa kwenye nchi yenye akiba kubwa kabisa ya gesi bila kupunguza bei ya gesi na kuwaambia watu wapande miti na kila anayeomba kibali cha kuchoma mkaa ni lazima aonyeshe kwanza shamba la miti kabla.

Mwafrika ataendelea kudharauliwa kutokana na matendo.

Tunaweza kujisifu kuwa na sisi tumo lakini ukiangalia na kutafakari kwa umakini wenzetu walipo na yale wanayoyafanya utaona kuwa DUNIA ni ya MUNGU na vitu ni vya MZUNGU.
 
Back
Top Bottom