Waafrika tunapambana kujionesha bora na kutaka sifa na validatio kutoka kwa watu weupe

Waafrika tunapambana kujionesha bora na kutaka sifa na validatio kutoka kwa watu weupe

Infropreneur

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2022
Posts
14,578
Reaction score
31,662
Waafrika hatupambani kuwashinda wengine.

Tunapambana kusindikiza wengine.

Waafrika tuna hali ya unyonge(inferiority complex).

Yaani hatuamini kwamba tunaweza kufanya mambo yetu wenyewe, kwa nguvu na akili zetu wenyewe bila kutaka recognition na validation kutoka kwa watu weupe.

Sisi waafrika ni kama hatujui nini tunafanya humu duniani!

Waafrika sisi, Badala ya kupambana na kuboresha maisha ya vizazi vyetu. Tunapambana kutaka credit na kutafuta attention na pongezi za watu weupe.

Unakuta tunafanya mambo si kwa sababu tunataka kujikwamua tulipo. Bali kutaka sifa na kuionyesha dunia kwamba na sisi angalau tumo.

Tunafanya mambo kwa kujaribu jaribu tu. Sio kwamba tuna ile nia na ari ya kuwashinda wengine.

Wewe angalia tu, Maraisi wa Afrika wakisha chaguliwa, wana tegemea kupewa pongezi na mwaliko kutoka kwa viongozi wa America, China, Russia na Ulaya.

Waende wapongezwe, waitwe ikulu, wawekewe gwaride la heshima, waende kujionesha kwa watu weupe kwamba ndio wameshinda uraisi.

Halafu wakirudi huku Afrika hakuna kitu wanafanya!! zaidi ya ufisadi na ahadi za kusadikika kwamba tutafanya hiki, tutafanya kile. Mwisho wa siku hakuna kinachofanyika zaidi ya wizi na ubadhirifu wa pesa za umma.

Unakuta watu weupe wakija huku Afrika, wanapapatikiwa na kupewa heshima na attention sana.

Ila waafrika tukienda nchi za watu weupe. Hakuna mtu ana time na sisi.

Wachina wanapambana kwa kasi ya ajabu wakitaka kupambana na Mmarekani. Tena wana ile kiu ya kuwapita kasi.

Lakini sisi waafrika tunapambana kujionesha tu na kutafuta attention za watu weupe. Watuone kwamba na sisi tumo.

Yani tunasindikiza dunia tu!

I'm out.
 
Watu weupe wamesha tuacha mbali sana, kikubwa ni kujifunza waliwezaje kufika hapo walipo...
Hata wachina walikuwa wameachwa mbali.

Ujerumani nao baada ya first world war, walichakazwa vibaya na wakarudi back to square one.

Lakini walipambana kwa akili, jasho na damu kuwafikia wengine.

Sisi waafrika tunapambana kujionesha tu na kutafuta attention za wazungu.

Sisi tunasindikiza dunia tu!
 
Mbona
Afrika ndio kuna watu wapambanaji tunakwama wapi?
 
Wachina na waarabu wanaplan mambo ya miaka 100 mbele wakati sisi watu weusi tunaangalia leo tu mtu akipewa dhamana anatapanya pesa kununua majumba yake binafsi na V8s bila kufikiria wengine wataishi vipi kesho.
Mentality yetu haina utofauti na mentality ya nyani wakivamia shamba la mahindi wanayapopoa yote hata kama mengine watashindwa kuyabeba na hawafikirii kama kesho watahitaji tena
 
Mbona
Afrika ndio kuna watu wapambanaji tunakwama wapi?
Afrika hakuna wapambanaji.

Bali wapigaji na wachumia tumbo.

Ukitaka kujua Afrika kila mtu ni mpigaji, wewe sikiliza tu maongezi ya watu. Utasikia mtu anasema "Aisee huku nilipo ajiriwa nabanwa kichizi napambana niingie serikalini taasisi fulani ina mpunga mrefu". Lengo si kwamba, ni apate mshahara mkubwa. Bali akaibe pia.

Hatupambani kujali na kuboresha maisha ya vizazi vijavyo.

Tunajipambania wenyewe tu kwaku tafuna na kujuhumu rasilimali zetu wenyewe!
 
Wachina na waarabu wanaplan mambo ya miaka 100 mbele wakati sisi watu weusi tunaangalia leo tu mtu akipewa dhamana anatapanya pesa kununua majumba yake binafsi na V8s bila kufikiria wengine wataishi vipi kesho.
Mentality yetu haina utofauti na mentality ya nyani wakivamia shamba la mahindi wanayapopoa yote hata kama mengine watashindwa kuyabeba na hawafikirii kama kesho watahitaji tena
Kabisa mkuu.
 
binafsi sioni tatizo kujipendekeza kwa mtu ambaye amekuzidi kila kitu maadamu uko tayari kujifunza, hao wachina unaowasema ni kwamba tu labda hauelewi hata wao wanajipendekeza kwa wazungu tembelea china wewe na mzungu halafu uone kama mtapata treatment sawa, hata japani walikoendelea mzungu bado anapewa special treatment klk binadamu mwingine yoyote yule.

kwanza hayo unayoyapendekeza ndiyo moja ya sababu kuu kwa nini afrika na watu weusi tuko backward, ni ugonjwa ambao unauwa black americans, wengi wanafundishwa kukataa kushirikiana na wazungu ingwaje wamezaliwa USA wanaikataa USA na black american yoyote anayejitahidi kusoma kwa bidii anatengwa na wenzake wanamuita sell out i.e anajifanya mzungu matokea yake wako back ward na wanaishia gheto ...

huyo chini carlton (comedy ya fresh prince of bel air) alikataliwa kwenye black fraternity kwa sababu hafiti na kuwa black sasa kwa nini carlton hakufiti? ni kwa sababu carlton ni straight a student, he works hard and successful mambo ambayo ni kinyume na black american hivyo black americans wenzake walimuona ni sell out kwamba anajifanya mzungu ndiyo maana wakamkataa kwenye black fraternity na walimtaka Will ambaye anafiti i.e he is not intelligent, anapenda mademu na kuruka ruka not serious with life huyo ndiyo amekubaliwa black fraternity ...

View: https://www.youtube.com/watch?v=Azk4Br9-Luo
 
Afrika hakuna wapambanaji.

Bali wapigaji na wachumia tumbo.

Ukitaka kujua Afrika kila mtu ni mpigaji, wewe sikiliza tu maongezi ya watu. Utasikia mtu anasema "Aisee huku nilipo ajiriwa nabanwa kichizi napambana niingie serikalini taasisi fulani ina mpunga mrefu". Lengo si kwamba, ni apate mshahara mkubwa. Bali akaibe pia.

Hatupambani kujali na kuboresha maisha ya vizazi vijavyo.

Tunajipambania wenyewe tu kwaku tafuna na kujuhumu rasilimali zetu wenyewe!
Duh kazi ipo
 
Ndio maana waafrika hatufiki.

Hatupambani kuwashinda wengine.

Tunapambana kutaka recognition na kupongezwa na wazungu.
Tatizo ni kwamba tumeaminishwa kuwa wazungu ni watu bora duniani.

Ndiyo maana wanawake wetu hawachoki kujipodia na kutengeneza nywele ziwe kama za wazungu.

Labda siku tukigundua kuwa wazungu ni watu kama sisi tutabadilika.
 
binafsi sioni tatizo kujipendekeza kwa mtu amabye amekuzidi kila kitu maadamu uko tayari kujifunza, hao wachina unaowasema ni kwamba tu labda hauelewi hata wao wanajipendekeza kwa wazungu tembelea china wewe mzungu halafu uone kama mtapata treatment sawa, hata japani waikoendelea mzungu bado yuji treated better binadamu mwingine yoyote yule.

kwanza hayo unayoyapendekeza ndiyo moja ya sababu kuu kwa nini afrika na watu weusi tuko backward, ni ugonjwa mabo unauwa black americans wengi wanafundishwa kukataa kushirikiana na wazungu inagwaje wamezaliwa USA wanaikataa USA na black american yoyote anayejitahidi kusoma kwa bidii anatengwa na wenzake wanamuita sell out ...

View: https://www.youtube.com/watch?v=Azk4Br9-Luo

Bora mchina anaye jipendekeza kwa lengo la kujifunza na kutafuta maarifa. Arudi China kuboresha maisha ya wachina.

Waafrika tuna jipendekeza kutafuta sifa tu na hakuna maarifa yoyote tunayo chukua.
 
Tatizo ni kwamba tumeaminishwa kuwa wazungu ni watu bora duniani.

Ndiyo maana wanawake wetu hawachoki kujipodia na kutengeneza nywele ziwe kama za wazungu.

Labda siku tukigundua kuwa wazungu ni watu kama sisi tutabadilika.
Hata kama wazungu wametuzidi.

Tusi ishie kuridhika na kukubali kwamba, wao ndio final say yetu.

Tuibe maarifa na tujifunze. Then tuje tuboreshe Afrika.

Sasa shida yetu sisi, tumekubali hatuwezi. Kilichobaki ni kusifia tu na kutaka recognition ya wazungu.

We are doomed to remain poor forever!!
 
Bora mchina anaye jipendekeza kwa lengo la kujifunza na kutafuta maarifa. Arudi China kuboresha maisha ya wachina.

Waafrika tuna jipendekeza kutafuta sifa tu na hakuna maarifa yoyote tunayo chukua.

na ndicho nilichomaanisha hakuna shida ya kujipendekeza kwa ambaye amekuzidi kila kitu maadamu kujipendekeza kwako ni kwa ajili ya kujifunza, you just have to be clever na kujua unachotaka ...
 
Hata kama wazungu wametuzidi.

Tusi ishie kuridhika na kukubali kwamba, wao ndio final say yetu.

Tuibe maarifa na tujifunze. Then tuje tuboreshe Afrika.

Sasa shida yetu sisi, tumekubali hatuwezi. Kilichobaki ni kusifia tu na kutaka recognition ya wazungu.

We are doomed to remain poor forever!!
Ni hatari mkuu.
 
Back
Top Bottom