Waafrika Tunatia aibu, mpaka leo tunategemea misaada ya wazungu?

Waafrika Tunatia aibu, mpaka leo tunategemea misaada ya wazungu?

wastani kwa idadi

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
503
Reaction score
1,432
Ila Africa tunatia huruma, inatia sana haira hadi leo baada ya kupewa misaada mingi miaka nenda rudi bado tunangoja msaada wa ARV na condom 😣😣.

Kampeni ya kuelimisha jamii juu ya afya mpaka mzungu alete hela na kuna wapigaji watajilipa posho za laki 2 kila siku, hotel za gharama, magari ya bei mbaya, n.k.

Dawa nazo mpaka mzungu alete hela ?

Kinachosikitisha zaidi viongozi wetu na wasomi wanapenda kuambatanisha Dr Phd kwenye majina yao lakini wameshindwa kabisa kutengeza hizi dawa bado tunategemea misaada, inaumiza sana.😫

Nimemuona Profesa Tibaijuka (milioni 40 kwake ni pesa ya mboga ) akilalamikia usitishaji wa misaada ya dawa, Laiti tungekuwa na viongozi waadilifu sidhani kama tungefika huku.

Inasikitisha sana kwasababu watu bado wanaendekeza ngomo bila kinga kwa kudhani ni urijali ila dawa tunataka msaada 😪😪
 
Back
Top Bottom