Waafrika wanalazimisha mafanikio ya Morocco yawe ya Waafrika wote

Waafrika wanalazimisha mafanikio ya Morocco yawe ya Waafrika wote

Tunatumia nguvu nyingi kubishana vitu rahisi tu Morroco yupo pale kupeperusha bendera CAF against UEFA,COPA AMERICA,CONCAF etc.Hivyo Morroco imebeba bendera ya Africa.Hoja ya Uislam na Uarabu ni kihisia zaidi.Ipi faida ya Morroco kwa Africa? Hapa hakuna kingine zaidi ya kupanda hadhi kwa AFCON kwa kuwa Dunia itaanza kuitazama michuano ya AFRIKA sio kama little tornament kama Klop alivyosema.
Si hivyo tu bali Kwa kuongezea pia Kwa mashindano ya kombe la dunia yatayofata(2026) Africa itapeleka timu 11(thanks to Morocco) ambapo idadi hii imechangiwa na timu ya Morocco kufika nusu fainali. Je Kwa hapa ni vipi Africa haijanufaika? chance ya kushiriki michuano hii kwa kila nchi Africa imeongezeka kwa idadi ya timu kuongezeka. Wao kudedicate ushindi wao Kwa jamii Fulani haifuti uhalisia kuwa ushindi wao umeleta faida kubwa katika bara la Africa na umegusa kila nchi ya Africa yenye ndoto ya kushiriki michuano hiyo mikubwa duniani.
Wao wanaweza kusherekea ushindi wao kivyao na waafrika watasherehekea ushindi wa Morocco kwa namna walivyo guswa. by the way kauli Ile ilikuwa ya mchezaji mmoja (sio timu ) na aliomba radhi.
 
Back
Top Bottom