Waafrika wasipoondoa mfumo wa kuwakilishwa na Wabunge kamwe wasahau maendeleo

Waafrika wasipoondoa mfumo wa kuwakilishwa na Wabunge kamwe wasahau maendeleo

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
1,108
Reaction score
1,132
Habarini,
Ni wazi wanasiasa wa Afrika ndio maadui wa maendeleo ya Afrika kwa kuwaibia Waafrika mali na fedha kwa kujilipa mishahara na marupurupu makubwa huku waliwaachw wananchi wao wakiwa maskini wa kutupwa.

Nawaunga mkono Kenya kwa kulisambaratisha bunge na kuwasambaratisha wabunge wote huku waliharibu mali zao ambazo wamezipata kwa wizi.

Haiwezekani mwanasiasa alipwe mshahara na marupurupu makubwa kumshindaa daktari,asksri,nesi,mwalimu,nk na asilipe kodi kwa kazi gani anayoifanya?

Ni bora tuwakilishee na watemdaji wa kata na vijiji tunaoonana nao kila leo siyo mbunge ambaye hatumuoni hadi kipindi cha uchaguzi na wanajificha kwenye makanisa na misikiti ambyo ni kivuli cha wizi.

Waafrika tuwakatae wanasiasa i.e:madiwani,wabunge,nk kutuwakilisha na kutupangia maisha yetu kwani ni wezi na wapo kwa maslahi yao siyo Afrika.

Naungana na Wakenya kwa vita yao dhidi ya wanasiasa i.e:wabunge.
Mungu ibariki Afrika
 
Nadhani pia ndio maana maandamano ya kenya yanafanikiwa kwasababu hayana mlengo wa kisiasa. Uku kwetu wanasiasa wale wale leo wako chama iki kesho wako kule alafu ndio wanakushawishi eti uandamane wakati ukifuatilia wote ni kizazi kile kile.
Mtwara wamewahi kuleta vurugu wakati wa gesi na kweli wananchi walijitoa kuonyesha malalamiko yao na ilo lilifanikiwa kwasababu hakukua na shinikizo la kisiasa. Ndio ule msemo wa Roma waliopo hatuwataki, na tunao wataka hatuwaamini.
 
Kuna dikteta wa kike nimemuona hapo juu, Tanzania kubadilika ni kazi sana mana kama wazazi wenyewe ndo hao juu
 
Nadhani pia ndio maana maandamano ya kenya yanafanikiwa kwasababu hayana mlengo wa kisiasa. Uku kwetu wanasiasa wale wale leo wako chama iki kesho wako kule alafu ndio wanakushawishi eti uandamane wakati ukifuatilia wote ni kizazi kile kile.
Mtwara wamewahi kuleta vurugu wakati wa gesi na kweli wananchi walijitoa kuonyesha malalamiko yao na ilo lilifanikiwa kwasababu hakukua na shinikizo la kisiasa. Ndio ule msemo wa Roma waliopo hatuwataki, na tunao wataka hatuwaamini.
Yes shida kubwa katika kuisaka haki ni DIVIDE AND RULE. Yani tumegawanywa sana kikanda na kisiasa. Hivyo hatuwezi kuwa na common goal.

Mpaka siku tukiachana na hivi vyama tukaamua kuitafuta haki bila kutumia siasa za vyama ni ngumu kufanikiwa.
 
Hatuwezi kusonga, bongo tuna matatzo mengi. Kubwa kabisa ni SISI WENYEWE
 
Attachments

  • FB_IMG_17186935862077137.jpg
    FB_IMG_17186935862077137.jpg
    405.7 KB · Views: 4
Back
Top Bottom