Waafrika wawajia juu wanaopendekeza chanjo ya COVID-19 kufanyiwa majaribio Afrika

Waafrika wawajia juu wanaopendekeza chanjo ya COVID-19 kufanyiwa majaribio Afrika

Sasa mkuu tumesaidi tafiti gani za kisayansi? Kifaa unayotumia kufanya mawasiliano na kukuwezesha maisha yako kwenda kwa wakati wameleta wao na hapo bado unawadharau.
Unaonekana kama.wewe ndo mjinga kama hauna shukrani kwa wazungu.
Wanapaswa kudharauliwa,mambo wanayofanya ni ya aibu sana.Hata hii wanayoita Corona ni aibu tupu.
 
Kuna mpango unaoendelea wa kutengeneza chanjo dhidi ya virusi vya corona, wazungu wanataka kufanyia majaribio ya chanjo hiyo Afrika kwa waafrika! Maajabu

Kwanini chanjo hiyo isifanyike huko duniani kwenye wagonjwa na vifo vingi vya corona? Kwanini isifanyike huko ilikoanzia?

Tangu kale, wazungu hawajawahi kuwa na nia njema na Afrika, Tusikubali. Magonjwa mengi yameletwa na wazungu kama vile UKIMWI.

Wananchi wakosoa mpango wa kufanyia majaribio chanjo ya corona DRC
Screenshot_20200405-154540.png
 
chanjo anapewa mtu ambaye bado hajaathirika, na kwa kuwa virusi vya korona bado havijaathiri bara la Africa,nadhani Africa pamoja na sehemu zingine chache ambazo bado hazijaathiriwa na korona ndio mahara sahihi kwa kufanyia majaribio ya chanjo dhidi ya korona
 
Chanjo zimeanza siku nyingi Ulaya , Marekani na Australia. Tena maelfu ya madaktari wamejitolea kushiriki bila malipo yoyote.

Nyie kimbilieni mambo ya ubaguzi. Sio kila jambo ni ubaguzi. Mambo mengine ni common sense tu.
Sasa hiyo dawa ikifanyiwa majaribio Ulaya tu, tutajuaje itafaa pia kwa mazingira ya Afrika?

Tambueni ya kwamba kuna mtego ktk hili na tunapaswa kuikataa hiyo chanjo,labda kwa mtu asiyekua mchunguzi wa kina juu ya ugonjwa husika na ugumu wa miili ya waafrika

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
NA MOHAMMED ABDULRAHMAN

Kizaazaa, taharuki, hofu na majina mengine mengi ndiyo unayoyasikia yakitumiwa kuelezea hali inayojikuta dunia wakati huu kuhusiana na janga la virusi vya Corona au COVID-19. Ugonjwa huu ulianzia China tangu mwanzoni mwa mwaka huu, lakini sasa hali ni mbaya zaidi Italia, Uhispania na Marekani baada ya hapo kabla Iran na Korea Kusini kuwa nchi zilizofuata baada ya China.

Hadi hivi karibuni bara la Afrika halikuwa limethirika kiasi cha kutia wasiwasi, lakini sasa Corona imeshaingia katika nchi kadhaa na kuanza kusambaa nchi za jirani. Wataalamu wanasema umetokana na watu walioingia kama watalii au raia waliorudi nyumbanio kutoka mataifa ambayo yameathirika. Vyovyote iwavyo, Corona limegeuka janga la dunia.

Tahadhari kubwa inachukuliwa na hasa kwa sababu ya idadi kubwa ya vifo katika baadhi ya nchi nilizozitaja kama Italia na Uhispania na Marekani ambako maelfu wamepoteza maisha.
Miongoni mwa hatu za kinga zinazochukuliwa na kuwataka watu wafuate muongozo uliotangazwa na serikali zao, ambazo baadhi zimeweka utaratibu wa watu kubakia ndani majumbani mwao , wakitoka tu pale inapolazimika.

Kuna nchi nyengine hatua hizo ni kama za hiyari kwa sababu watu kwa sababu mbali mbali wamelazimika kutoka kutafuta njia za kuweza kukidhi maisha yao ambayo tangu hapo ni magumu yakitegemea kipato cha siku ili angalau kuweza kupata mlo mmoja kwa familia. Mazingira ya aina hiyo yako zaidi katika nchi zetu za Kiafrika. Lakini kwa wa Ulaya sana sana wanaokiuka utaratibu uliotangazwa hufanya hivyo zaidi kwa kutojali zaidi ingawa mwamko kuhusu kitisho hiki cha Corona ni kama kwengineko.

Kuna wanasiasa na wataalamu ambao kila kukicha wanazungumzia janga la Corona na jitihada za kuhakikisha vifaa mbali mbali vinapatikana kwa ajili ya idadi ya walioambukizwa na wagonjwa inayozidi kuongezeka na mahospitali yaliofurika. Sambamba na hayo ni jinsi madaktari na wauguzi wanavyojitolea usiku na mchana , wengine wakiwa wahanga wa janga hili na kuathirika wakiwa makazini. Wengi wamepoteza maisha.

Miongoni mwa juhudi zinazoendelea ni kutafuta tiba ya virusi vya Corona. Hata hivyo tiba kwa gharama ya nani?

Hivi majuzi katika mjadala kwenye stesheni moja ya televisheni ya Ufaransa, madaktari wawili maarufu wa Ufaransa Jean-Paul Mira na Camille Locht walisababisha mjadala mkubwa mitandaoni walipopendekeza majaribio ya chanjo mpya yafanywe Afrika. Hoja yao eti kwasababu waafrika hawana vifaa na dawa za kutosha.
Mira alipotoa matamshi hayo akaungwa mkono na daktari mwenzake Locht aliyesema, “ Kwa hakika tutalizingatia vilivyo pendekezo lako.”

Hapana shaka yoyote ni matamshi ya kibaguzi na hoja yao isiyo na mantiki hata kidogo , ilioibua maswali kadhaa. Kwanini majaribio yasianzie kwanza kule ambako hali kwa sasasa ni mbaya bila kiasi na ukiliweka kando hilo kwanini yasiwe majaribio ya wakati mmoja duniani kote kwa kuzingatia hili ni janga lililoukumba ulimwengu kwa jumla ?

Miongoni mwa waafrika wa kwanza kukemea matamshi hayo ni wachezaji nyota wa kandanda wa zamani Didier Drogba kutoka Cote d´Ivoire na Samuel Etoo wa Cameroon, na Msenegal Demba Ba. Wote waliyakosoa vikali matamshi hayo kuwa ni ya kibaguzi na kusikitishwa na mtazamo wa waulaya wenye misingi ya kibaguzi kwamba Afrika ni maabara ya majaribio ya kitabibu.

Ba aliandika katika mtandao wake wa Twitter kwamba bara zima la Afrika kuanzia Kaskazini hadi Kusini lilikuwa na maambukizi ya watu 6,700 na Ufaransa pekee karibu 60,000, hivyo Ufaransa kingekua kituo bora kwanza, cha majaribio yoyote yatakayofanywa

Kama kawaida wengine tukisubiri viongozi wetu watakuwa na msimamo gani kuhusu kadhia hiyo ninayoiita ya dharau, ubaguzi , unyanyasaji na kulitusi bara la Afrika. Nikitarajia Umoja wa Afrika ungezungumza , lakini haikuwa hivyo. Pamoja na hayo sikushangaa hata kidogo,kwani moja huo umezidi kuwa dhaifu. Bado kuna hali fulani ya baadhi ya watendaji wakuu katika Halmashauri kuu ya Umoja huo kuyatii zaidi mataifa yaliotutawala . Rais wa Halmashauri kuu Moussa Faki Mahamat ni kutoka Chad na aliwahi kuwa Waziri mkuu na waziri wa mambo ya nchi za nje.

Historia ya kisiasa ya Chad inafahamika sawa na nchi kadhaa zilizokuwa makoloni ya Ufaransa barani Afrika. Nilikaa nikatafakari na mwishowe sikushangaa tena , kwa sababu yaliomfika aliyekuwa Balozi wa Umoja wa Afrika mjini Washington Dk.Arikana Chimbori-Quao. Bibi Chimbori aliondolewa katika wadhifa wake, alipodiriki kuikosoa Ufaransa inavyoendeleza aina ya ukoloni mambo leo katika baadhi ya nchi ilizozitawala Afrika, ambapo nchi 14 zinawajibika bado kwa Ufaransa chini ya mkataba unaozishurutisha kuweka 85 asilimia ya pato lao la akiba ya kigeni kwenye benki kuu ya Ufaransa.

Inasemekana Ufaransa ilikuwa na mkono wake katika uamuzi wa Mahamat ambaye nchi yake Chad imo katika orodha hiyo.
Ufaransa ina kituo kikubwa cha wanajeshi mjini Ndjamena na mara kadhaa imemnusuru Rais wa sasa Idris Deby dhidi ya waasi , ambao waliwahi hata kukaribia Ikulu kabla ya kukandamizwa kwa msaada wa ndege za kijeshi za Ufaransa. Dola hilo mkoloni wa zamani limekuwa na mkono wake katika misukosuko ya Chad tangu baada ya kuangushwa Rais wake wa kwanza Francois Tombalbaye na migogoro ya wa tawala waliofuata Jenerali Felix Malloum, Goukuni Wedei, na Hissene Habre.

Kwa muda mrefu kumekuweko na minon´gono na tetesi kwamba maamuzi ya Umoja wa Afrika huwa yanajulikana Paris na miji mengine mikuu ya magharibi hata kabla ya waafrika kuyajua au hata kabla ya tamko la mwisho kutolewa.

Lakini tukitathmini kadhii ya madaktari hao wa kifaransa si Umoja wa Afrika peke yake tunaopaswa kuukosoa , viongozi wetu pia wamekuwa kimya kama walivyo kuwa kimya bara hilo na waafrika walipotukanwa na Rais Donald Trump wa Marekani.

Msimamo wa viongozi tuliokuwa nao miaka mingi ya nyuma, wa ujasiri na kujiamini ( ingawa sio wote ) hauko tena. Wakati ule angalau Afrika ikizungumza kwa sauti moja na kusikika licha ya tafauti za kinadharia na ushawishi wa wakoloni wa zamani kwa baadhi ya nchi. Miongoni mwa masuala ambako ulionekana msimamo wa pamoja ni mapambano dhidi ya ukoloni, Ian Smith kujitangazia uhuru na utawala wa wazungu wachache nchini Rhodesia 1965 na utawala wa kibaguzi Afrika Kusini.

Afrika ilikuwa na sauti iliosikika katika Umoja wa Afrika , Umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote
( Non-Aligned Movement ) na hata katika Baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Kisa hiki cha chanjo ya majaribio ya Corona sio cha kwanza. Kulikuwa na majaribio ya chanjo ya Polio na Ebola . Afrika pia imegeuzwa jaa la zana za vifaa vibovu vya elektroniki visivyotumika tena Ulaya , Taka za sumu na nguo zilizotumiwa ( mitumba) ambazo awali zikipelekwa kama misaada lakini sasa zimekuwa biashara.

Umewadia wakati wa kusimama kidete kuilinda utu wetu na kuwakumbusha madaktari Mari , Locht na wote wenye fikra kama za kwao kwamba,”Afrika sio Shamba la Majaribio, bali bara linalostahili heshima kama Ulaya.”
Nasi pia tujiulize nani hasa wa kulaumiwa na kwasababu gani kuna udhaifu miongoni mwa mataifa yetu na vyombo vya kulisimamia na kulizungumza bara hili, ukiwemo Umoja wa Afrika ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Virusi vya corona: Afrika sio uwanja wa majaribio ya chanjo ya corona - WHO
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

amelaani kauli alizoziita za "kibaguzi" kutoka kwa madaktari wawili wa Ufaransa ambao walitaka chanjo ya virusi vya corona kufanyiwa majaribio barani Afrika.

"Afrika sio na haitakuwa uwanja wa majaribio wa chanjo yoyote," amesema Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Matamshi ya madaktari hao waliyoyatoa kwenye mjadala wa runinga yamezua ghadhabu, na wametuhumiwa kwa kuwachukulia Waafrika kama "nguruwe wa kufanyiwa majaribio ya maabara".


Mmoja wa madaktari hao ameomba radhi kwa kauli yake.

Alipoulizwa kuhusu matamshi ya madaktari hao kwenye mkutano na wanahabari juu ya hali ya virusi vya corona ulimwenguni, Dkt Tedros alionekana Dhahiri kuwa mtu mwenye hasira, na kukiita kitendo cha madaktari hao kama "mning'inio kutoka kwenye ulevi wa fikra za kikoloni".

"Ni fedheha, jambo la kushtusha kusikia katika Karne ya 21 kutoka kwa wanasayansi wakitoa kauli kama zile. Tunalaani hilo kwa nguvu zote, na tunawahakikishia kuwa hilo halitatokea," ameeleza Dkt Tedros.


Kadri ya namba ya watu wenye virusi vya corona inavyopanda barani Afrika, baadhi ya serikali barani humo zinachukua hatua ngumu na kali za kujaribu kupunguza kasi ya maambukizi.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta hapo jana alipiga marufuku safari zote za kutoka na kuingia Nairobi pamoja na miji mingine mikubwa mitatu kwa kipindi cha wiki tatu.

Madaktari hao walisema nini?
Katika mjadala kwenye runinga ya ufaransa ya channel LCI, Dkt Camille Locht, mkuu wa utafiti kutoka shirika la utafiti wa afya la Inserm alikuwa akiongelea juu ya majaribio ya chanjo barani Ulaya na Australia.

Dkt Jean-Paul Mira, mkuu wa kitengo cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Cochin ya jijini Paris, kisha akasema: "Nichokoze kitu, siyo kwamba tunatakiwa kufanya utafiti huu Afrika, ambako hakuna barakoa, hakuna matibabu wala huduma ya nusu kaputi?

"Kama inavyofanyika kwengineo kwenye taffiti za ukimwi. Kwa kutumia machangudoa tunajaribu vitu kwa kuwa tunajua wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi na hawafanyi kitu kujilinda."

Dkt Locht akatikisa kicha kwa kuashiria kukubalina na pendekezo hilo, kisha akasema: "Upo sahihi. Tupo katika mchakato wa kufikiria utafiti sambamba bararani Afrika."

Dkt Mira awali aliuliza iwapo utafiti huo utaendelea kama ilivyopangwa kwa wahudumu wa afya Australia na Ulaya kwa kuwa wanavitendea kazi vinavyowawezesha kujikinga na maambukizi wakiwa kazini.


Mkuu wa shirika la Afya Duniani Dkt Tedros amesema kwamba bara la Afrika halitakuwa uwanja wa majaribio ya chanjo ya corona
Kipindi hicho kilisababisha hasira kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo nyota wa zamani wa kandanda Didier Drogba, ambaye aliyaita matamshi hayo kuwa "yamejaa ubaguzi ". Akaongeza: "Msiwafanye waafrika kuwa binaadamu wa majaribio ya maabara! Ni jambo linalochefua".

Nyota mwengine wa zamani wa kandanda Samuel Eto'o aliwaita madaktari hao kuwa "wauaji".

Matamshi ya madaktari hao yanakuja wakati ambao tayari kuna khofu barani Afrika kuwa watu wa bara hilo watatumika kama majaribio kwa chanjo mpya ya virusi vya corona.

Vituo vya kutibu virusi vya corona katika nchi kadhaa Afrika vimeshambuliwa, tukio la hivi karibuni zaidi ni kuvunjwa na waandamanaji kituo kimoja kilichokuwa kinajengwa jijini Abijan, Ivory Coast.

Picha za video mtandaoni zinaonesha watu wakikiharibu kituo hicho kwa kutumia mikono yao huku wakimwaga chini vifaa vya ujenzi.


Chanzo: BBC
 
Na nyie waafrica mnaotaka mfanyiwe majaribio hayo.......nawaambia hivi...Muache mawazo ya kinguruwe na kipanya panya.......utakuta jitu linapelekwa pelekwa kama joka la kwenye simu ya nokia torch......
 
Kama dawa za malaria wanazijaribu sana kwetu,mara Krolokwini,Orodar,sasa hivi Mseto kesho sijui watatuambia tunywe dawa gani.

Wazungu wanatuumiza polepole,ila ndio vile miili yetu ishazoea matatizo na shuruba,bila kusahau Mungu anatupenda na kutupigania.
 
A French doctor apologized after suggesting that Africa should become a testing ground for a COVID-19 vaccine, remarks that sparked public outcry on social media.

Jean-Paul Mira, head of the intensive care unit at the Cochin Hospital in Paris, made the comments in an interview that aired last week on the French television channel LCI with Camille Locht, the research director at the French National Institute of Health and Medical Research, Inserm.


“If I could be provocative, shouldn’t we do this study in Africa where there are no masks, treatment, or intensive care, a little bit like we did in certain AIDS studies or with prostitutes?” Mira asked.

“We tried things on prostitutes because they are highly exposed and do not protect themselves.


 
Back
Top Bottom