Waafrika weusi ni 15% tu ya idadi ya watu duniani, ni ushenzi kusema tuna overpopulation!

Overpopulation haipimwi kwa kujilinganisha na wengine. Inapimwa kwa kuangalia resources zako.

Tanzania kwa kasi ya sasa ya kuongezeka watu, ina double population kila miaka 23.
Unajua kila kitu ni relative, i mean really relative. Mtu mnene ni mnene kwa sababu tu wapo wembamba, that is all. Mtu tajiri, ni tajiri tu kwa sababu wapo masikini wa kufanya comparison. Population iwe ina-double au ina-tripple its irrelevant, fact is bado resources zinatosha as it stands currently, ni kiasi cha kuzi-utilise tu.
 
Tatizo kubwa si resources kutosha au kutotosha.

Resources ambazo watu hawana economic access nazo hazina tofauti na resources ambazo hazipo.

Tatizo ni, kama resources zinatosha, watu wana access nazo in an economic way?

Kwa sababu kama sasa hivi na population yetu ya milioni 60 hatuwezi/hatujui kutumia vizuri resources zetu, ambazo nyingi ni fixed/non-renewable, tukija kuwa milioni 120 baada ya miaka 23 tutawezaje kuzitumia vizuri? Tuna mkakati gani tumejiwekea wa kuweza kuzitumia vizuri?

Kwa sababu, kama hatuna mkakati, hata kama tukikuza uchumi kwa 8% mfululizo miaka yote hiyo 23, ongezeko la uchumi litamezwa na ongezeko la watu.

Hili si jambo la kinadharia tu. Baada ya Uhuru, serikali ilipanga mipango mizuri sana ya maendeleo ya jamii. Lakini mipango ile ilishindwa kukidhi mahitaji ya jamii kwa sababu moja ndogo tu.

Mipango ilipangwa kwa kuangalia population ya wakati wa kupanga mipango, haikuangalia projections za population increase.

Matokeo yake mipango ikatekelezwa kama ilivyotakiwa, lakini kwenye jamii pengo likabaki kuwa kubwa tu.

Kwa sababu mipango ilikuwa haijaangalia projections za population increase.

Sasa, kama tumeshindwa kuwapa Maisha bora watu milioni 60 wa leo, tuna mkakati gani wa kuweza kuwapa Maisha bora watu milioni 120 wanaoweza kuwepo ndani ya miaka 23 ijayo?
 
Mimi sikatai kuhusu ongezeko la watu na uwezo wa kuwamudu, tatizo langu ni inakuwaje watu wanye historia ya kutojali watu weusi leo hii wajali ongezeko lao?
 
Nimekuelewa sana
 
Resources ambazo hazitumiki si sawa na resources ambazo hazipo, maana ambazo zipo na hazitumiki ni kwamba kuna potential ya kutumika given the proper push, sasa amabzo hazipo kabisa hata ufanyeje.ni hazipo. Fact is, ratio ya population kwa rasilimali (zinatumika/hazitumiki) bado ipo infavor ya kufyatua, tufyatue zaidi na tukiwa wengi tutapata msukumo wa kuzitumia, unajua demand is the mother of all inventions, hakuna overpopulation Africa.
 
Baba yaishe
 
Your assertion is rather too general, hayo unayosema yangekuwa kweli, tungekuwa tushaendelea sasa hivi.

Nimekuuliza na kukupa nafasi utuoneshe tumejipanga vipi kutumia hizo resources ambazo hazitumiki kwa namna ambayo itatusaidia kiuchumi kabisa, hujafanya hilo.Unasema tu vaguely kuhusu "proper push". Any Jock can say that. Guess what? It ain't that simple.

Unachofanya ni kushindwa kupanga.

Kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa.
 
Ukweli Mtupu
 
Watu Weusi wengi ni Wajinga wajinga sana, Wana wivu na Majungu, wabinafsi na wenye chuki wasiopendana wenyewe wala kupenda maendeleo ya wenzao.
 
Jamaa Kama ange bahati kusoma idadi ya mito ilikuwep tz iliyokuwa inatililisha maji mwaka mzima kabla ya 1995, Kama leo hii bado yote Inakuwa maji tena mwaka mzima.....

Simiyu Shinyanga Kahama Lunzewe Nyakanazi Kakonko na maeneo ya Nzega Tabora kwa mtu aliye pita maeneo yao 1990 kushuka chini akipita Leo lazima Alie, miti mapori karibu yote yamefyekwa, na sababu miti/mapori hayo Ni ile ya asili ya ukame iliota taratibu for over years and years, kwa hiyo kuota/kuzaliana tena/replacement yake ni ngumu. Sahivi hiyo mikoa yote/hayo maeneo leo hii yana uhaba wa mvua hatari.

KWA MTU YEYOTE MWENYE MIAKA 35+ ALIYEKULIA MIKOA YA MAGHARIBI YA TZ LAZIMA AKUBALIANE NA MIMI KWENYE ATHARI ZA UHARIBUFU WA MAZINGIRA NA TABIA NCHI..

JANA WAZIRI KIGWANGALA KASEMA ZAIDI YA HEKARI 350K ZINAKATWA KWAAJILI YA MKAA TZ KILA MWAKA.
 
Nashukuru kwa kunipa tena nafasi ya kukuonyesha namna tutakavyotumia resources ambazo hazitumiki.
1.) Najua unafahamu potential kubwa ya kuzalisha umeme pale Rufiji, na TUMEJIPANGA kuzalisha MW 2100 as soon as mradi utakapokamilika, na ile gorge ina room for expansion ya kuzalisha hadi MW 6000 at full potential.

1.1) Licha ya kuzalisha umeme, maji yatayokuwa yanajazwa kwenye hili bwawa yanaweza kutumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ambacho tunatarajia kuongeza uzalishaji wa chakula nchini mara kadhaa ya ilivyo sasa, kiasi tutaweza kulisha hata bara lote ikibidi.

1.2) Nadhani unafahamu domino effect itakayoletwa na umeme nafuu na wa uhakika, viwanda vingi vitakavyohitaji malighafi mbalimbali vitaanzishwa ma hibyo rasilimali watu ambayo haitumiki sasa itatumika, tena itakuwa haitoshi, hivyo kuna haja ya kifatua zaidi.

2.) Kuna rasilimali muda ambayo tumepanga kuitumia efficiently, TUMEJIPANGA kuhakikisha rasilimali muda haipotei kweye mafoleni ya kijinga, tumejipanga kujenga flyover zaidi ya 7 jijini Dar tumeanza TAZARA, tunaendelea ubungo ma kwingine kutafuata, pia kuna Selander bridge.

Don'y be a pessimist, think positive.
 
Nadhani hiyo ni athari ya micro overpopulation ya pocket husika, nadhani sababu ya wakimbizi, tunaongelea Africa as a whole.
 
Halafu mtu anakwambia suluhisho ni kuzaliana tuongeze watu!
 

You are starting to make me think that this entire thread is one big sarcastic joke.

Ukishindwa kutumia potential kwa watu milioni 60, utawezaje kutumia potential kwa watu milioni 120?

Utakachobadili mpaka uweze ukiwa na watu 120 ambacho huwezi kufanya ukiwa na watu milioni 60 ni kipi?
 
Hata hapa wameshaanza kazi yao, kwa kuwatumia baadhi ya watu wenye tamaa za madaraka kuhadaa watu nia ikiwa ni kumaliza amani yetu tuliyokuwa nayo kwa miongo kadhaa, mmoja wao yupo huko ulaya kwa mafunzo zaidi ya kuja kututeketeza.
Nonsense
 
Tulichobadili ni very obvious, or rather tuliyembadili. Nadhani unaweza ukaona tofauti ya awamu ya 5 na awamu zingine, this time tuna a genuine push ya maendelea toka juu kabisa, JPM. Awamu zilizopita ilikuwa ni ubabaishaji zaidi, tofauti na sasa ambapo tunaona dhamira ya dhati kabisa, hasa kwenye suala la usafirishaji ambapo SGR inaendelea vizuri mno, kwahiyo ni dhahiri kwa kilichobadilika ni uongozi, na ndio maana tulishindwa huko nyuma, ila tutaweza mbeleni. No how is it a joke, unless you are joking.
 
Now I know this is either a big sarcastic joke, or you are smoking something non-kosher.
 
Now I know this is either a big sarcastic joke, or you are smoking something non-kosher.
Sasa huku ni kukosa hoja, i'll give you another chance to give sensible response, otherwise tap out.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…