Waafrika Tujitafakali, Maana si kwa Matusi Haya!
Denis Mpagaze
___________________
Tangu Wazungu wakutane na sisi kwa mara ya kwanza mpaka leo bado hawajaamini kama na sisi ni watu! Bado kabisa!
Charles Robert Darwin alipokutana na mtu mweusi kwa mara ya kwanza alisema tunaukaribu sana na nyani🫢🫢🫢.
James Watson, Mtaalamu wa Tiba na Mshindi wa Tuzo ya Nobel mwaka 1962 alisema mtu mweusi ana akili ndogo kuliko mtu mweupe.
Mwaka 1985 Kabulu Pieter Willem Botha alisema watu weusi wanaofanana na binadamu na kutenda mambo kama binadamu hayawahalalishii wao kuwa watu wenye akili timamu na binadamu aliyetimia.
Botha akaendelea kusema katika upeo Wazungu ni bora kuliko Weusi hilo halina ubishi kwani limejidhihirisha kwa miaka mingi iliyopita kwa maana hiyo mweusi ni malighafi kwa mweupe.🫢🫢🫢
Mzungu mwingine nimemsahau jina lake, yeye alisema kadili mtu mweusi anavyozidi kuwa mweusi ndivyo anavyozidi kupungukiwa akili! Jamani jamani😌😌.
Donald Trump anasema nchi nyingi za kiafrika zilitakiwa ziendelee kutawaliwa kwa miaka 100 kwa sababu hawajui lolote kuhusu utawala bora.
Comte Joseph Arthur Gobineau miaka ya 1800 aliwahi kusema Waafrika ni watu wasiokuwa na ubunifu wowote wa kisanyansi na kisiasa badala yake wanafaa zaidi kwa kazi ya kucheza, kuvaa na kuimba.
Huyu bwana aliwahi kusema duniani kuna, race tatu tu- weusi ambao ni wajinga na washamba; wanjao ambao ni dhaifu na weupe ambao wana akili na wazuri.🏃🏃
Anasema kati ya races zote tatu, weusi wamejaaliwa nguvu nyingi pasipouwezo wa kufikiri.🫢🫢🫢
George W. F Hegel aliwahi kusema Mwafrika halisi hana akili, hana maendeleo, hana utamaduni, hana dini pia hana maadili na adabu. Mwafrika kwa asili ni mdhalimu na mkatili.🙈🙈🙈
Lester Thurow anasema njia nzuri ya kuliokoa bara la Afrika ni kumrudisha tena Mzungu kuitawala Afrika maana Mwafrika ameshindwa kujitawala.
Sir Richard Burton alisema, Mwafrika anapofikia utu uzima, akili yake hudumaa na kuanzia hapo hukua kurudi nyuma badala ya kwenda mbele; anaweza kuiga na kuigiza kama nyani, lakini hawezi kuunda kitu chake.
Tracy Zille anasema isingekuwa Wazungu midomo yetu ingekuwa inanuka kama panya aliyeoza kwa sababu hadi leo tumeshindwa hata kutengeneza dawa ya meno.
Wao wanazalisha dawa za meno sisi tunazalisha Manabii Matajiri, Wachungaji na Maaskofu, wao wanazalisha dawa za meno sisi tunazalisha mafuta ya upako na maombi!
Hata Wamisionari walipofika Afrika waliona bara limemejaa washenzi waliotakiwa kuokolewa ili waende mbinguni.
Wazungu hadi kesho wanaamini wao ndo wateule wa Mungu wenye wajibu wa kuikoa Afrika.
Afrika tumeitwa majina yote mabaya; Bara la giza, bara lisilo na matumaini, kovu la dunia, pori la washenzi, bara lenye viumbe waliolaaniwa na waliokata tamaa; bara la watu wanaohihitaji kuokolewa na Mzungu.
Kabla ya kuwajibu Wazungu, Tujitafakari kidogo!
1. Gari linauzwa milioni mbili Japan, likiletwa Afrika linauzwa million 12! Yaani mtoza ushuru anakula nyingi kuliko mwenye mali, na anayeliwa na ndugu yake mtoza ushuru. Yaani Mwafrika anamla Mwafrika mwenzake. Sasa katika suala kama hili unaachaje kuwa na wasiwasi na akili ya mtu mweusi Afrika?
2. Tuna mafuta kila Bahari ya Afrika lakini tukitaka kuyachimba tunamwita Mzungu aje kutuchimbia na wakati tunazalisha mainjinia kila mwaka. Hapa kuna akili kweli? Ipo lakini imelala. Imelala au imelazwa? Sijui!
3. Malaysia walikuwa wanakwenda Ghana kujifunza kilimo cha mawese, leo hii Ghana wanakwenda kujifunza kila kitu Malaysia hadi kilimo cha mawese. Hapa nani hana akili? Nakupa mji!
4. Kila kitu kinachoonekana ni bora tunakiita cha kizungu yaani mpaka kuna panzi wa kizungu, kuku wa kizungu, nyoka wa kizungu, mapera ya kizungu, mahindi ya kizungu na nzi wa kizungu na wakati nzi ni nzi tu. Sasa hapa tofauti yetu na unyani iko wapi?
5. Juhudi za vijana wa Kiafrika kuanzia usanii, teknolojia, ubunifu haziungwi mkono, ila za wazungu zinaungwa mkono hatari. Huwa nashangaa Mwafrika mwenzangu anachukia nikitangaza kitabu changu kwenye kundi lake la Whatsapp lakini likipita tangazo la movie za kizungu na kichina na kifilipino hasemi. Hapa tukiambiwa sisi ni watu wa hovyo tutakataa?
6. Leo hii mwafrika hata chakula chake mwenyewe kimefutika, anakula chakula cha ng'ambo, chakula cha kwenye makopo na mvinyo wenye majina ya kizungu. Hii ndiyo fahari ya mwafrika. Kujenga uchumi wa kigeni! Hapa ukiitwa mjinga utachukia?
7. Unamunulia mkeo wigi la kizungu ili tu aonekane kama mzungu. Kwakweli hawezi kuonekana kama Mzungu, sana ataonekana Mzungu bandia. Au tuseme Mzungu kichaa. Tunashindana kuukataa uafrika kwa shilingi na dolali. Bure kabisa!😄🫲
8. Angalia elimu wanayofundishwa watoto wetu leo, unadhani wataweza unda hata radio hata ukiwapa miaka elfu ijayo? Thubutu! Hapa napo nani hana akili? Serikali au wewe unayesomesha?
9. Tukija kwenye suala la muda ndo utakutana na wagonjwa wa kutosha. Utadhani wakati Mungu anatuumba alisahau kuweka kipengele cha muda kwenye bongo zetu. Tunachelewa kila sehemu mpaka kwenye mazishi!😌😌
10. Sasa kama tunauana kwa sababu za kidini na wakati Mungu hakuumba dini unafikiri zinajitosheleza kichwani?
11. Afrika tupo chini kiutendaji,kiimani,kifikra na kiteknolojia na wakati mali zote ziko Afrika na teknolojia zote zilianzia Afrika.
12. Afrika imejaa Wachawi lakini wajinga tu. Kazi kutesa na kuua watu tu! Hivi kwanza unaelewa maana uchawi? Wagiriki wanakwambia uchawi ni kujua na kutenda kuliko pitiliza ndo maana ukaitwa witchcraft. Wit ni neno la Kijerumani yaani wise! Kwa kingereza cha kale neno uchawi uliitwa “wicca” yaani "craft of the wise.” Sidhadi hata kama ulijua wizard limetokana na wise. Sasa Wachawi wa Afrika wanatumia uwezo huo uliopitiliza kudhalilishana na kuumizana. Fikiria mtu anaingia ndani ya nyumba usiku wa manane, imefungwa vizuri kabisa, anambeba mwalimu hadi chooni, mnaamka asubuhi mnakuta mwalimu amelala chooni,unadhani hiyo ni knowledge ya kitoto?
13. Wagiriki walijifunza uchawi Misri wakaondoka nao hadi kwao wakaupa jina zuri, Sayansi. Lakini kanuni za utendaji ni zilezile! Wachawi wetu wanatumia uwezo huo katika kuua na kuharibu badala ya kutumia uchawi huo kuwashughulikia wezi wa rasilimali za Afrika.
14. Afrika ukitaka huduma nzuri lazima uinunue hata kama unalipa kodi. Wakati Wazungu wameamua maisha yao yawe mazuri kwa sababau ya kodi.