sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Inasikitisha sana na inaumiza.
Waafrika weusi katika hizo nchi yani hata uwe chotara wao watakuweka kundi hilo hilo,
nchi za Ulaya mashariki zikiwemo Ukraine na Russia ni wabaguzi sana wa rangi hakuna mfano.
Huwa nashangaa sana kwa sasa mtu yupo kushabikia Ukraine au Urusi maana sisi tukipata matatizo hao hawanaga muda kabisa na sisi maana wanatuona kama viumbe dhaifu.
Majuzi tu hapo video ilisambaa waafrika wa huko Ukraine wanazuiwa kupanda treni, kwamba maisha ya waafrika yana hadhi ya chini kuzidi wao ?
Wao wanashangaaga sana wakijaga huku kwetu vile wanavyo jizolea attention, kupewa heshima na kuabudiwa kama miungu mtu , akipita sehemu watu wengi wanamshangaa positively, watu wanampungia mkono na kumpa salamu, watu wengi wanatamani kumuongelesha, akifika ofisi za serikali anashughulikiwa chap chap, akifanya hata upuuzi jamii inaweza kuona kawaida na kumsamehe kisa ni mzungu, kwenye mapenzi huwa ni kama wanachagua maana wanaginbaniwa, n.k. mwafrika akienda huko kwao inakuwa kinyume.
Sijui ni ukosefu wa akili au ni kitu gani, huku ni kujidhalilisha wazi wazi.