Waajiri watakiwa kuwa na Ubinadamu kwa Wazazi Wanaojifungua Watoto Njiti

Waajiri watakiwa kuwa na Ubinadamu kwa Wazazi Wanaojifungua Watoto Njiti

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waajiri watakiwa kuongozwa na ubinadamu wa Mamlaka waliyopewa kwa kuwaongezea likizo Wazazi wa watoto Njiti ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kwa mtoto ikiwemo kifo kwa kukosa uangalizi wa karibu wa mama yake.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati akijibu Maswali Mawili ya Nyongeza ya Mbunge wa Newala Vijijini, Mhe. Maimuna Salum Mtanda aliyouliza kuwa.

“Je? Serikali haioni haja ya kubadilisha sheria iliyopo ambayo inawanyima haki watoto Njiti kwasababu, wanaachwa wakiwa bado ni wachanga sana kiasi ambacho kinaweza kuwapelekea vifo kwa kukosa uangalizi wa karibu wa mama? swali la pili “Serikali haioni kumnyima haki mama huyo wa siku za nyongeza kunaweza kumsababishia matatizo ya afya ya akili?" - Mhe. Maimuna Salum Mtanda.

Akijibu Maswali hayo Naibu Waziri Kikwete amesema “Sheria zipo, Miongozo ipo na taratibu zipo changamoto inayotokea ni kutokana na baadhi ya waajiri ambao kwa roho mbaya tu wanaamua kuwanyima, Nitoe maelekezo kwa waajiri wote inapotokea mama amepata mtoto njiti ni Wito wangu kwamba waongozwe na ubinaadamu katika yale mamlaka ambayo wamepewa ili waweze kuwapa nafasi Wazazi wakawalea watoto wao,” Mhe. Kikwete.

“Sisi kama serikali inawajali wakinamama na Watoto Watanzania na inatambua na kuheshimu afya za akili za Watanzania hivyo inapotokea hali hiyo ni kuwaonea huruma wazazi hawa na kuwapa nafasi ili walee watoto wao ambao wamezaliwa kwenye mazingira magumu kama hayo,” Naibu Waziri Kikwete.

Aidha Kuhusu suala la kuongeza siku za likizo pale mtumishi anapojifungua mtoto njiti, suala hili halijawekewa utaratibu wa kikanuni kutokana na taratibu za uendeshaji wa shughuli za Serikali bali mtumishi (Mzazi) anaweza kuomba ruhusa ya kawaida kutoka kwa Mwajiri wake inapotokea changamoto kama hiyo, majibu haya yakiwa ni kutoka katika swali la Msingi Lililoulizwa awali na Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Agnes Elias Hokororo alilouliza kuwa “Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza siku za likizo kwa Wazazi wanaojifungua Watoto Njiti?” - Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Agnes Elias Hokororo.

“Serikali inatoa likizo ya uzazi kwa watumishi kwa mujibu wa Kanuni H.12 ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka 2009 ambapo Kanuni 2 ya Kanuni H.12 inabainisha kuwa muda wa likizo ya uzazi kwa mtumishi mwanamke ni siku 84 ambazo hutolewa mara moja katika kipindi cha miaka mitatu,” Mhe. Kikwete.
 

Attachments

  • tuhhbbb.jpg
    tuhhbbb.jpg
    35.5 KB · Views: 7
  • drrdert.jpg
    drrdert.jpg
    49.2 KB · Views: 5
  • maxresdefault_13-k0CFDI4Oo-transformed.jpeg
    maxresdefault_13-k0CFDI4Oo-transformed.jpeg
    61.4 KB · Views: 7
Back
Top Bottom