Nilitaka kuanzisha uzi kuhusu hili pia!
juzi nikiwa halmashauri moja wapo nliwauliza hiki kitu! nkaambiwa hela ya kujikimu ni "LABDA" mpaka mwezi ujao! nkawauliza sasa katika hiki kipindi chote mtu unaishije!? wakasema hiyo hawajui ni kutafuta alternative! nikawaambia sasa kama ni hivo vipi kuhusu salary!? ntapata mwezi huu!? nayo wakasema LABDA mpka mwezi ujao nlichoka sana!
nkawaambia sasa nataka kuchukua 14 days ntafute pesa mwenyewe na kujiandaa maana huu mkoa sijawahi fika! wakakataaa kua mwisho ni seven days!
nkajiuliza ina maana wanaajiri watu ilihali hawajajiandaa kuwapa angalau hiyo posho ya kujikimu!? nakumbuka yule bwana shemdoe wakati anatangaza alisema watakaochukua ila wasiripoti watashughulikiwa kumbe ilikua siasa tu kuonesha inawahi kutoka ilhali hakuna!?
nimeamua nirudi kwenye biashara yangu na kwa heshima ya kizalendo nataka serikali itafute mtu wa kuni replace, nimerejista kila kitu siku ntakayoona wameweka hyo hela ndo ntaenda! wasipoweka watafute mtu mwingine!
japo nna shida ila nisigeuzwe punda!
asanteni!