Tetesi: Waajiriwa wapya wa afya na elimu hawapewi hela ya kujikimu

Bro,

Kafanye kazi kwa MASLAHI MAPANA YA TAIFA, wewe Ni miongoni Kati ya laki uliebahatika kupata kazi.

Kafanye kazi
Posho ya kujikimu ni haki ya mtumishi. Acha kuwafanyia mzaha watu wengine. Ingekuwa wewe ungesema hivyo?
 
Tufundishwe mind set kujiajiri aseee huko mbele watoto wetu wasije dhalilika maana ajira zinazidi kuwa finyu.,...tujiajiri
Huyu keshaajiriwa. Haki zake ziheshimiwe.
 
Kuwa na subira mzee. Sometimes huwa inachelewa, ila utalipwa. Fanya kazi.
 
Labda pesa za kuwalipa hazipo, vinginevyo ongeeni na waajiri wenu huko halmashauri waone ni namna gani ya kuwawezesha kabla ya kupata hiyo pesa na mshahara wenu kuanza kulipwa...
 
Mwaka 2015 nina mwanangu alichaguliwa mkoani ualimu hakupata chochote hata mshahara wa mwezi wa kwanza hakupata kwa hiyo wajue hilo kwa tahadhari.
 
Halmashauri haiwezi kuandaa pesa ya kujikimu,ukaikuta unapoenda kuripoti kwani haifamu ni yupi ataripoti au hatoripoti....kuna siku 14 za kwenda kufunga mizigo ndio uende kuanza kazi ....nenda kaage familia ukirudi utaikuta ipo.......
You try to think correctly,thing again accurately.
 
Maigizo mengi mno hizi serikali zetu.
 
Kwani yeye ndo alilipa kwa wakati? Tulioajiriwa enzi za JPM tulipata hiyo pesa after 2/3 months. Yeye akafanye kazi pesa atalipwa tuu
Akafanyeje?wlwaelekeze namna Kama unafahamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…