Waajiriwa wote sio matajiri?

Wananipa kuwaza sana. Kuna ma mtu yameajiriaa na makampuni na mashirika makubwa yanakuja almost 5m+ kwa mwezi, sasa najiuliza hawa sio matajiri? Au utajiri unaanzia mol ngap?
Daaah uliposema tu wanakunja 5m+, nikajua bado ndio umetoka chuo au unamalizia chuo..umeona hiyo 5m+ nyingi sanaa?

ila matajiri wa kuajiriwa hawapo, ila wapo wengi wenye uchumi wa kati, middle class..ila ukwasi wa kuitwa matajiti hawapo.
 
Kuajiriwa uwe katika top position ukijiongeza unaweza kuwa tajiri ila ualimu,uaskari, udaktari,karani ? Sahau kitu kinachoitwa utajiri
 
Matajiri WANAAJIRI, HAWAAJIRIWI.

matajiri pesa hufanya kazi kwa ajili Yao, hawafanyi kazi kwa ajili ya kupata pesa.

Hakuna TAJIRI ALIYEAJIRIWA.

TAJIRI hupanga maisha yake kwa asilimia kubwa na hapangiwi.

Matajiri wana Financial freedom.. unapataje hivyo kama Kuna watu au mtu ndio anaamua wewe ulipwe Nini?

Anyway... Hakuna tajiri ALIYEAJIRIWA.
 
Ishu ni kwamba kupitia ajira yako unaweza vip kuwa tajiri yaani labda uwe na side hustling unatoa pesa ya huku unapeleka huko.

Ni jinsi gani wanafeli kufanya ajira zao kuwa kama mtaji wa kufika mbali..
 
Ukiona mwajiriwa tajiri ujue ni fisadi au mwizi kwa lugha nyingine.
Ukimwambia akupe mchanganuo wa mishahara yake aliyopokea imemsaidia vipi kuwa tajiri hatoweza kukupa
 
Ishu ni kwamba kupitia ajira yako unaweza vip kuwa tajiri yaani labda uwe na side hustling unatoa pesa ya huku unapeleka huko.

Ni jinsi gani wanafeli kufanya ajira zao kuwa kama mtaji wa kufika mbali..
1. Earning income to

2. Passive income to

3. Portfolio income to

Hizo transition zinahitaji muda wa kutosha na elimu, ambayo ni wachache Sanaa wataweza kumudu.

Kutumikia mabwana wawili ni changamoto..

Finally wanaweza kufika hatua ya tatu wanaacha kazi walizoajiriwa nazo (kuwapa mtaji) na kufanya kazi zao...

Sababu ya kufeli ni ukosefu wa elimu...
 
Ila ajira Inadumaza na vile unapta pesa bila ya kutumia nguvu basi akili inalala kabisa huwezi fikiria nje ya box inakuja shangaa una majukumu kiboa haya kusave pesa mda haitoshi.
 
Naomba kujua kwa sheria izi level inachukua mda kazini kwa experience kazini mpaka uzifikie.

1.principal officer
2.Manager
3. Kuwa katika board of directors
 
CEO wa Google Sundar Pichai
ana utajiri $1.3 billion,huyu Ni maskini?
 
Hapa ulichoongea kiko sahihi lakini umetoka nje ya mada kidogo.
Mada yetu haisemi kwamba mtu aliyeajiriwa hatokuwa tajiri akiset mipango yake ya baadae.
Mada yetu inasema hakuna tajiri ambaye ni mwajiriwa,kwa maana ya kwamba unaweza kutumia ajira kupata mtaji ukaanzisha biashara zako kisha ukaachana na ajira ukaenda kusimamia biashara zako na baadae kuwa tajiri hii inawezekana na hakuna anayepinga hili.
 
CEO wa Google Sundar Pichai
ana utajiri $1.3 billion,huyu Ni maskini?
Yeah..

Ni mtumwa tu

Halafu Mtu kutofit vigezo vya kuwa tajiri jaimaanishi Mtu huyo masikini..

Otherwise kama utafanya comparison
 
Sijui hoja yako nini ila ipo wazi huko kwenye siasa kwa sasa ni biashara watu wanatumia pesa nyingi kupata kuungwa mkono
 
Tatizo ni hiyo ajira ya kukupa utajiri, na je itakuchukua muda gani na kujitoa kiasi gani kufikia huo mshahara mnono.

Matajiri wa ajira wapo nchi za wenzetu huko, hedge fund managers and CEOs of big companies
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…