"Huwezi kuwa tajiri kwa kuajiriwa" kauli hii imekaa Kimotivational zaidi na mara nyingi hutamkwa na watu wanaojaribu kusisitiza suala la kujiajiri binafsi kupitia Ujasiriamali lakini kitu watu wengi wasichokijua nikwamba ajira ina mahusianano makubwa sana na kujiajiri binafsi na vitu hivi viwili hutegemeana kwa kiasi kikubwa. Kutajirika siyo lazima mtu uanzie chini kabisa na bishara ya genge au kuuza karanga. Matajiri wengi wamepata utajiri wao baada ya kuajiriwa na kupata mitaji yao kupitia hizo ajira wakaja kufungua mamiradi ya maana.
Huwezi kufungua biashara ya uhakika pasipokuwa na mtaji na haijalishi mtaji umeupata kwa kudunduliza biashara ya karanga na ubuyu ama umeupata kutoakana na mshahara wa kazi ya uhandisi, vyote hivyo ni vyanzo vya mtaji na mtu anaweza kuwekeza na kuwa bilionea.
Kwahiyo si sahihi kusema eti, mtu hawezi kutajirika kwa kazi ya ajira kwani utajiri ni mchakato unaohitaji uwekezaji iwe ni pesa za mshahara au faida kutokana na biashara. Ni kitu hutaamini lakini walioajiriwa wana fursa kubwa zaidi ya kuwa matajiri maanake wana access kubwa zaidi ya kupata mtaji kuliko mtu anaye hustle na biashara ndogondogo, mwajiriwa ana uwezo wa kukopa kiurahisi na akakopesheka wakati huohuo akiwa na uhakika wa mshahara kila mwezi, akijinyima kidogo tu tayari ana mtaji kwasababu mradi wake hatagusa faida itakayopatikana bali mshahara wake.