Waalimu, madaktari, wasomi na watu wa sekta nyingine tujifunze kwa wafanyabiashara wa Kariakoo kuzungumzia kero zetu.

Waalimu, madaktari, wasomi na watu wa sekta nyingine tujifunze kwa wafanyabiashara wa Kariakoo kuzungumzia kero zetu.

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Wafanyabiashara wa Kariakoo wameonesha weledi mkubwa katika kuelezea kero zao mbele ya waziri mkuu Kassim Majaliwa. Wengi wa wafanyabiashara hawajasoma sana kama waalimu, wahadhiri, madaktari, nk. Wasomi tunashindwa wapi!

Waalimu wana kero nyingi lakini hawathubutu kuzungumzia kero zao. Madaktari mishahara kiduchu lakini wapo bize tu na makoti yao meupe.

Tunakwama wapi wasomi?! Tunashindwa hata kugoma? Tufunguke watu wa sekta zote kwani kudai haki zetu ndio mwanzo wa kuzipata.
 
Ukiajiriwa tu, wewe ni mtumwa wa fikra. Jikomboe leo, anza kuuza mayai mtaani, mdogo mdogo, Mungu atakufungulia milango ya baraka.

Potentiality yako duniani haiwezi kuonekana ukiwa mtumwa wa mtu mwingine. Kila mwajiriwa ni mtumwa wa tajiri wake
 
Back
Top Bottom