Nilishasemaga humu jf kuwa kuna timu imetenga fungu kubwa kwaajili ya kupata matokeo mazuri, haijulikani fungu hilo litatumikaje na kwa namna gani, Yanga wasiondoe uwezekano wa jambo hilo, kumfukuza Kaze inawezekana ni sehemu ya hizo pesa maana sioni ni kwa namna gani Kaze anahusika na mchezaji kukosa penaliti au kupoteza nafasi ya kufunga bao wakati amebaki yeye na kipa tu langoni au kushindwa kudaka mpira rahisi, au mchezaji kudai anaumwa, au dk wa timu kudai mchezaji hayuko fit kucheza mechi.
Katika timu kubwa kama Yanga Kocha kazi yake kubwa ni kuinganisha timu icheze kitimu na kutengeneza nafasi za kufunga magoli lakini sio kumfundisha mchezaji namna ya kuingiza mpira golini na kama yuko mchezaji wa aina hiyo hakuppaswa kusajiliwa Yanga. Timu ya Yanga chini ya Kaze inatengeneza nafasi nyingi lakini wachezaji wanashindwa wenyewe kuzigeuza nafasi hizo kuwa magoli.
Tunapomtafuta mchawi wa Yanga kwanza tusiache kuzimulika hilo fungu la pesa za ushindi zimetua kwa nani kwa kupitia nani, pili tuumulike uongozi wa juu wa club na mwisho ndo tuongelee wachezaji.