Waandamanaji Nairobi wavamia jengo la Bunge baada ya kuwashinda nguvu polisi, yasemwa waandamanaji 10 wameuawa kwa kupigwa risasi halisi

Waandamanaji Nairobi wavamia jengo la Bunge baada ya kuwashinda nguvu polisi, yasemwa waandamanaji 10 wameuawa kwa kupigwa risasi halisi

Waandamanaji 10 wanaripotiwa kuuawa na polisi baada ya kuvamia jengo la Bunge la nchi hiyo na kuwashinda nguvu polisi.

Hali kwa sasa ni shwari kidogo baada ya polisi kuongeza nguvu ya idadi katika eneo hilo.

Sehemu moja ya jengo hilo la Bunge imeshika moto na moto huo bado waendelea.

Tukio hilo limetokea mara tu baada ya Bunge hilo kupitisha mswada wa sheria ya kodi inoongeza kodi katika bidhaa mbalimbali nchini huo.

Raisi Ruto amesema kuongeza kodi huko kutathibiti kukopa mikopo ambayo itaiathiri nchi hiyo kiuchumi.

Yadaiwa kuwa wabunge wengi walopitisha mswada huo wamepokea mlungula ili kurahisisha kupitishwa kwa muswaada huo ambao utaathiri wakenya wengi walo na kipato cha chini, wafanyabiashara na wachuuzi.

Kuna majeruhi wengi ambao wamejeruhiwa kwa risasi ambapo polisi waliamua kutumia nguvu na risasi halisi badala ya risasi za bandia au "rubber bullets".
Hayo mambo ya uasi[Civil unrest] hatutaki, sisi Mh Samia anatupeleka nchi ya ahadi yenye maziwa na asali.
Kama mtu ana hoja, maoni atumie, Diwani au mbunge wake , Serikali ni sikivu, tuwe na uzalendo!
 
IMG-20240625-WA0019.jpg
IMG-20240625-WA0020.jpg
Ofisi za mamlaka ya mapato KRA Embu watu wamevunja na kuondoka na samani na vifaa huku wafanyakazi wakiingia mitini kujiokoa.

Madhara ya polisi kutumia nguvu watu wasingefika hapo.
IMG-20240625-WA0021.jpg
 
Tukio hili laonyesha jinsi serikali ya Kenya ilivyoshindwa kulinda jengo la bunge jengo la kistratejia na shughuli za serikali nchini humo ukizingatia maandamano haya yamechukua siku 7.

Hivyo kulikuwa na muda wa kutosha kwa serikali kuchukua hatua za tahadhari na kuongeza ulinzi katika majengo ya serikali likiwemo hili jengo la Bunge.
Ulinzi gani watumie rocket kupiga waandamanaji au we umeona wamefanikiwa kumkamata sniper aliyekuwa anawalenga wakampiga mpka akasema nani amemtuma kuuwa watu sasa kwa misingi ya sheria aliyemtuma mahakama si itamshitaki ni kosa kuuwa watu
 
Kitu ambacho wataniboa ni kuvunjavunja Maduka na Property za raia lakini so far 🫡
Vijana WA Kenya hawajielewi kuwa chochote wafanyacho pumbafu zao wanachofanya kinatakiwa kuwa na support ya business community sababu wao ndio walipa Kodi wakubwa ambao wakiwaunga mkono serikali lazima iwasikilize sababu ndio taxpayers wakubwa wanalipa Kodi kuendesha serikali sasa waki loot maduka Yao support watapata wapi!

Tanzania tuko vizuri wafanyabiashara wakubwa wameigomea serikali ya Tanzania kufungua maduka hadi serikali iondoe kero na serikali imekuja mbio kuwa ohhh tunaondoe

Hayakufanyika maandamano kama Kenya ku achieve objective

Wakenya wanaingia Tu vibaka mitaani wasiojua Ku achieve objective inahitaji support ya business community sio tu ku loot maduka Yao

Vijana WA Kenya shenzi zenu hopeless kabisa

Watanzania tunajielewa na strategy za kudai haki

Vijana WA Tanzania MSI copy huo ujinga WA vijana WA Kenya wapumbavu wasiohitaji support ya business Community ya Kenya wanaopora maduka yao
 
Hii iwe wake up call kwa watawala wanaowategemea polisi

Kwamba polisi nao hujilegeza kwa waandamanaji ili yatokee yaliyotokea na
Kutuma ujumbe kwa watawala
Kuwa hawako salama kihivyo
 
Hila viongozi wa nchi za africa huwa solution ya matatizo ya kifedha huwa wanaona kupandisha gharama kwa wananchi badala ya kupunguza matumizi ya serikali ya sio ya lazima unakuta nchi ina hali ngumu kifedha lakini hyo hyo nchi imetoa order gari za dhamani kubwa kwa ajili ya viongozi wakati wangeweza kununua gari nzuri kwa bei ya chini
Hawajioni kama wana shida, mzigo wote bebesha mwananchi, mkamue zaidi
 
Hii iwe wake up call kwa watawala wanaowategemea polisi

Kwamba polisi nao hujilegeza kwa waandamanaji ili yatokee yaliyotokea na
Kutuma ujumbe kwa watawala
Kuwa hawako salama kihivyo
Tatizo Kenya ajira za Polisi huenda kikabila sana shida inaanzia hapo

Mkuu wa Majeshi aliyefariki.kwa Helikopta alikuwa mjaluo alijaza wajaluo kama wote Kwenye majeshi ikiwemo Polisi

Sasa wanavuna walichopanda mazao yamekomaa

Ruto kazi anayo

Kenya inashangaza mno kuna wasomi wazito na waongea kingereza kuliko Tanzania lakini kumaliza ukabila kumewashinda

Hivi KAZI ya elimu ni nini kama sio kutatua changamoto za kijamii ikiwemo ukabila

Tanzania elimu yetu ndogo,akili ndogo kingereza kidogo cha kubabaisha ukabila tuliumaliza

How comes Hao wakenya wenye akili na usomi na kingereza na elimunna exposure kuliko watanzania wanashindwaje kumaliza ukabila hadi watanzania tuwazidi?

Shame on them
 
Back
Top Bottom